Parker Solar Probe: Satelite ya NASA yenye speed kali kuliko kitu chochote kuwahi tengenezwa na binadamu!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Hawa jamaa tuwape maua yao kwenye R&D!
IMG_7018.jpeg

Mwaka 2018 NASA waliituma hii satelite kwenda kwenye space kufanya uchunguzi wa Solar corona (tuseme kama atmosphere kulizunguka jua, wataalamu wa Heliophysics hapa watasaidia)!

Kwahiyo hadi leo imekaa huko kwa zaidi ya miaka 7 ipo huko space, ikiwa powered mainly na solar energy (kwa kutumia sola solar panels).

Sasa kujishoot kuelekea kwenye jua hawatumii mafuta wala nyuklia, ila kuna teknolojia inaitwa gravity assist, yaani kama kombeo inavyofanya kazi. Probe inajizungusha kwenye sayari ya Venus then inajishoot kwenda kwenye jua.

Kwa uzito ni takribani kilo 685 tu, na dimension ya kama mita 3 kwa 1. Na ina sensors/radars/mitambo kama minne hivi kwaajili ya hii mission:

FIELDS: Inapima nguvu ya sumaku (magnetic fields) na mawimbi ya umeme yanayotoka kwenye Jua.
WISPR: Hii ndiyo "Kamera." Inapiga picha za corona ya jua na Solar winds.
SWEAP: Inapima chembechembe za moto (plasma) kama protoni na elektroni zinazotoka kwenye Jua.
IS☉IS: Inapima nishati ya juu ya chembechembe zinazoweza kuwa hatari kwa mawasiliano hapa Duniani.

Hii probe ndio satelite iliyowahi kufanikiwa kufika Karibu zaidi na jua. Mwaka 2024 ilisogea Umbali wa kilometa 6.9 million kilometers tu kutoka kwenye centre ya jua, ikifika speed ya 191 km/s (690,000 km/h)!
IMG_7019.jpeg

Kwakua ilisogea sana kwenye jua, ilibidi waiwekee solar shield yenye uwezo wa kuwithstand joto la 1,300 degrees, na huku ndani ikiacha joto kubaki 29 degrees!

Budget ya hii mission ni zaidi ya Trillion 3.8 za Kitanzania.
 
Good topic
Ninavyofaham, ukipita jua kwa juu yake utakutana na Solar system nyingine, na ukipita hiyo ya pili utakutana na nyingine na nyingine hadi zifike 7.
ILA kwa bahati mbaya binadam hajapewa hicho kibali hata cha kufika solar system (mbingu) ya pili,
Nimefanya reference kwenye Quran takatifu
 
Hawa jamaa tuwape maua yao kwenye R&D!
View attachment 3558538
Mwaka 2018 NASA waliituma hii satelite kwenda kwenye space kufanya uchunguzi wa Solar corona (tuseme kama atmosphere kulizunguka jua, wataalamu wa Heliophysics hapa watasaidia)!

Kwahiyo hadi leo imekaa huko kwa zaidi ya miaka 7 ipo huko space, ikiwa powered mainly na solar energy (kwa kutumia sola solar panels).

Sasa kujishoot kuelekea kwenye jua hawatumii mafuta wala nyuklia, ila kuna teknolojia inaitwa gravity assist, yaani kama kombeo inavyofanya kazi. Probe inajizungusha kwenye sayari ya Venus then inajishoot kwenda kwenye jua.

Kwa uzito ni takribani kilo 685 tu, na dimension ya kama mita 3 kwa 1. Na ina sensors/radars/mitambo kama minne hivi kwaajili ya hii mission:

FIELDS: Inapima nguvu ya sumaku (magnetic fields) na mawimbi ya umeme yanayotoka kwenye Jua.
WISPR: Hii ndiyo "Kamera." Inapiga picha za corona ya jua na Solar winds.
SWEAP: Inapima chembechembe za moto (plasma) kama protoni na elektroni zinazotoka kwenye Jua.
IS☉IS: Inapima nishati ya juu ya chembechembe zinazoweza kuwa hatari kwa mawasiliano hapa Duniani.

Hii probe ndio satelite iliyowahi kufanikiwa kufika Karibu zaidi na jua. Mwaka 2024 ilisogea Umbali wa kilometa 6.9 million kilometers tu kutoka kwenye centre ya jua, ikifika speed ya 191 km/s (690,000 km/h)!
View attachment 3558541
Kwakua ilisogea sana kwenye jua, ilibidi waiwekee solar shield yenye uwezo wa kuwithstand joto la 1,300 degrees, na huku ndani ikiacha joto kubaki 29 degrees!

Budget ya hii mission ni zaidi ya Trillion 3.8 za Kitanzania.
Duh hii speed sio poa 🙌
 
Hzo picha ni halisi...!!? au ndo story afu tunapewa picha za AI
 
Back
Top Bottom