Parking fee kamata kamata

Parking fee kamata kamata

Kwani deni lao lina riba..hii hela hata sijui imekujaje kujaje!
Wawe wanatupa notification basi,mtu utajuaje kama umeandikiwa?

Alaf walivyo wapuuzi mpka gari ikiwa gereji hizi za barabarani wao mbio mbio wanamulika!
Screenshot_2023-09-04-14-32-37-46_52bf3dea746c4f78d830cee1458ff403.jpg
 
Parking kando ya barabara ni wizi wa mchana kweupe, maana yake wanataka watu wawe wanabeba magari mgongoni wakitaka kuingia mahali kununua bidhaa au kupata huduma? nimekaa majuu kuna street parking, watu wanapaki magari kando ya barabara mitaani kwenye maeneo yalipo makazi yao hata mwaka mzima na hakuna wanacholipia. Utaratibu wa kulipia parking unatakiwa uwepo kwenye maeneo maalumu yaliyojengwa kama maegesho na halmashauri au watu binafsi kama ilivyo mlimani city, siyo kando ya barabara zilipo huduma na biashara.........watu wame park eneo la bar wanapata vinywaji, mtu anakuja kutoza parking, hii haiwezi kuwa haki.​
 
ila mbona ukiangalia online inaonyesha kuna ukomo wa tarehe ya kulipa. Je hiyo kamata kamata ni kwa wote ama wale waliovuka ukomo wa tarehe?

Ila hii nchi kila kitu kimekuwa fursa sasa. Na huu utaaanza kuwa usumbufu mwingine sasa na mwanya wa watu wa jiji kuchukua pesa za hongo.View attachment 2738650
Ungeficha na control number boss.
 
Mimi walishanisumbua sana.
Siku hz nkipaki namuangalia kwanza nijue alipo, then namchana wazi kua anisubirie tumalizane asihangaike kupiga hyo picha. Nkitoka nampa 200 au jero ya maji nasepa
 
ila mbona ukiangalia online inaonyesha kuna ukomo wa tarehe ya kulipa. Je hiyo kamata kamata ni kwa wote ama wale waliovuka ukomo wa tarehe?

Ila hii nchi kila kitu kimekuwa fursa sasa. Na huu utaaanza kuwa usumbufu mwingine sasa na mwanya wa watu wa jiji kuchukua pesa za hongo.View attachment 2738650
Wakikujia waonyeshe hiyo tarehe ya deadline halafu waulize imefika? Wakileta fujo na wewe wafanyie fujo.
 
Back
Top Bottom