Parklands: Video yaonyesha Mwanaume akiporwa mchana kweupe, Maswali yazuka kuhusu usalama Nairobi

Parklands: Video yaonyesha Mwanaume akiporwa mchana kweupe, Maswali yazuka kuhusu usalama Nairobi

Wakaguongo

Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
95
Reaction score
38

Video inayosambaa mitandaoni ikionyesha wanaume watatu wakimvamia na kumpora mwanaume katika eneo la 6th Avenue, Parklands, Nairobi, imezua wasiwasi kuhusu usalama wa wananchi katika maeneo ya umma.

Tukio hilo linalodaiwa kunaswa mchana kweupe linaibua maswali kuhusu hatua zinazochukuliwa na polisi kukabiliana na wizi wa wazi jijini na kuhakikisha maeneo ya makazi na biashara ni salama kwa wananchi.

Wakazi na viongozi wa eneo hilo wanapaswa kupata majibu kuhusu iwapo tukio hilo limeripotiwa, kama uchunguzi umeanzishwa na hatua gani zinachukuliwa kuwawajibisha waliohusika.

Ikiwa mtu anaweza kuporwa mchana kweupe katika eneo kama Parklands, nani anapaswa kuwajibika kuhakikisha usalama wa wananchi? Je, polisi wanafanya vya kutosha, na ni hatua gani za haraka zinazohitajika?
 
Back
Top Bottom