Part 1:- Kwanini baadhi ya wanaume hushindwa kuota ndevu

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
KWA NINI BAADHI YA WANAUME WANASHINDWA KUOTA NDEVU?
Kulingana na tafiti mbalimbali, baadhi ya wanaume hupoteza mawiki kadhaa wakijaribu namna tofautitofauti za kuotesha ndevu katika sura zao, lakini zaidi wakipatacho ni vindevu kidogo tu na labda zikaota kimakundi makundi na zisizo na afya.

Hali ni tofauti kwa wanaume wengine kwani huchukua kila muda kadhaa katika siku ili kunyoa au kuzipunguza ndevu zao.

Kitamaduni ndevu huchukuliwa kama alama inayotambulisha uwezo wa misuli ya mwanaume, nguvu na hekima.

Na ikitokea kwa wale wanao hangaika kuotesha misitu ya ndevu, hizi zinaweza kuwa msaada kwako kukusaidia kuotesha na kuwa mmiliki mwenye kujivunia mafuriko ya ndevu usoni. Lakini kabla ya kuangalia suluhisho ngoja tuone baadhi ya sababu ambazo zinaweza kuwa ni moja kati kikwazo.

1) MWITIKIO HAFIFU WA VICHEO DUME (TESTOSTERONE):
The Androgen Dihydrotestosterone ( homoni ya kiume) hii ndio inayowajibika katika mfumo mzima wa ukuaji wa ndevu. Ni moja kati ya homoni maarufu. Homoni hii huchochea mabadiliko ya mwanaume na muonekano wa kijinsia. Hivyo, kadri Wingi wa ndevu unavyozidi ndivyo pia hutegemea jinsi mwili unavyochochewa na testosterone. Ndio maana uwezo wa kukua kwa ndevu pia muda mwingine hujumuishwa na hali ya vijinasaba (genetics). Wanaume wengi walio na mwitikio mkubwa wa testosterone huwai pia kupata vipara mapema zaidi. Ndio, {DIHYDROTESTOSTERONE} husaidia kuzalisha ndevu pia inawajibika katika upoteaji wa nywele kwa wanaume.

2) ALOPECIA:
Huu ni ugonjwa ambao huacha watu wakiwa bila nywele au vipara katika sehemu sehemu vichwa vyao na sehemu nyingine ya mwili. Wanaume wqlio katika hali hii kawaida hawawezi kuota nywele za usoni. Lakini ni ngumu sana kugundua tatizo hili kwa haraka. Hata hivyo hadi sasa hakuna dawa yoyote ya kuweza kuponya ugonjwa huo.

3) UPUNGUFU WA KAZI ZINAZOSHIRIKISHA ZAIDI MWILI NA MICHEZO:
Michezo na kazi nyingi za kushirikisha mwili kwa kutumia nguvu husaidia sana katika kuongeza homoni za kiume (testosterone) kwa mwanaume. Lakini si kazi zote za nguvu na michezo yote husaidia hili, bali ni kadhaa tu kati ya hizo. Chaguo bora katika kusaidia kuchochea kiwango cha testosterone ni yale mazoezi ya kujaza misuli.

4) UPUNGUFU WA MADINI CHUMA/ ENEMIA:
Enemia husababisha kupungua kwa seli nyekundu zenye afya katika damu; na hasa seli nyekundu za damu zinazobeba oksijeni kwenda sehemu mbalimbali za mwili. Ndio maana mwanaume ambae hana kiwango cha kutosha cha seli nyekundu za damu, vichocheo vya nywele za usoni hushindwa kupata oksijeni ya kutosha kuweza kusapoti ukuaji unaoridhisha au kushindwa kabisa kuzalisha nywele za uso/ndevu kabisa.

images.jpeg
 
Genetics, mazingira? Havipo hivi?
 
View attachment 1997160
Ndevu hata kama ni 1 ni ndevu tu ipewe heshima [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Alopecia hakuna dawa j
Kweli?
Ndio alopecia haina dawa. Ama dawa yake ni kujikubali tu kwa kunyoa nywele zilizobaki. Ingawa unaweza kupunguza kasi ya tatizo kwa kutumia dawa kama minoxidil, steroids injection na hair transplant.
 
Noma Sana kwahiyo wasio na ndevu testosterone zinakuwa chini hivyo show hakuna?
kumbuka sio upungufu wa testosterone pekee ndio chanzo.

Unaweza ukawa na testosterone nyingi na bado ukashindwa kuwa na ndevu za kutosha au usiote kabisa.
 
Ndio alopecia haina dawa. Ama dawa yake ni kujikubali tu kwa kunyoa nywele zilizobaki. Ingawa unaweza kupunguza kasi ya tatizo kwa kutumia dawa kama minoxidil, steroids injection na hair transplant.
Hapana, Labda kama umerithi kipara, ila Alopecia sidhani kama ni permanent inatokea tu ukiwa under stress ama immunity ikiwa down,baadae zinaoota zenyewe, anyway I'm not a doctor ni vitu tu nimeona
 
Back
Top Bottom