Part time lecturers wanauwa ubora wa elimu ya juu

bidam90

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2013
Posts
273
Reaction score
202
Kumekuwa na ongezeko kubwa la vyuo Tanzania ukilinganisha na idadi ya walimu wakufundisha kozi husika vyuon!

Hii inapelekea baadhi ya vyuo kuomba walimu kutoka vyuo vyengine kufundisha kama part time lecturers!Hiv kweli inawezekana lecturer 1 kufundisha vyuo zaid ya vi3 kwa semester moja!

Hebu fikiria darasa moja linawanafunzi zaidi ya 500 tena chuo kimoja!bado utakuta ndan ya hicho chuo kimoja anafundisha zaidi ya kozi moja!

Part time lecturers japo sio wote wanamatatizo mengi sana moja wapo ni ufundishaji mbovu lengo lao ni kumaliza kozi iishe bila kuangalia wanafunzi wameelewa vp kozi husika,pia wengi wao wamekuwa wakibeba wanafunzi hata kama wamefeli asionekane hajui kufundisha alinde kibarua chake!

Vile vile usahihishaji mbovu wakat mwengine anawapa watu wengine wamsaidie kusahhisha kutokana na majukumu alonayo!

Hivi TCU wanaliona hili kweli?
 
Mkuu toa mfano wa hivyo vyuo vitatu ambavyo huyo lecturer anaweza akawa anafundisha kwa wakati mmoja ktk semester moja!

Pia ukiangalia uhalisia na kimantiki je inawezekana lecturer mmoja kufundisha kama part timer ktk vyuo 3 tofauti ktk semister moja..?!
Niko tayari kujuzwa zaidi.
 
Nini mbadala wa part-time lecturers? Mi nadhani hapa kuna chuki zaidi kuliko uhalisia maana part-time lecturers wanapata nafasi hizo kutokana na uhaba wa wahadhiri. Vyuo ving sana (hata UDSM) vina uhaba wa wahadhiri. Kipi bora kati ya kumtafuta mtaalam wa course fulani kutoka chuo kingine au kumpa course mhadhiri fulltime ambaye sio mtaalam wa hiyo course? Mambo yote ni usimamizi tu, hata hao full-time lecturers wanaweza wakafundisha kwa kusuasua kama hawajasimamiwa vizuri maana wengne tumewahi kuwa na fulltime lecturers wa UDSM ambao darasani hawaonekani, lecture notes na assignments tunazipata kwa email.
 
Mkuu sitakutajia jina sina nia ya kuchafua chuo chochote!ila kukupa hint nenda mbeya ukajionee mwenyewe!!
 
Nakubaliana na wewe mkuu!hakuna njia nyengine ila usimamizi ndo unatakiwa!Tatizo kuna vyuo vyengine ilo halifanyiwi kazi!Sehem kama mbeya walimu wa shida sana nenda mwenyewe ukajionee!!nina uhakika na nilisemalo!!
 
mm kwa upande wangu naona hawa part time wanafundisha na kumaliza kuliko full time..mm kwa upande wng pale ardhi wapo walimu wanaotoka udsm wa part time but wanafundisha vzr na wanamaliza topics kuliko hao wa full time
 
Leo nimeshangaa kusikia eti 'part time lecturers' hawakamilishi majukumu yao ipasavyo. Siku nyingi nilikua nikipata taarifa za kusifu uwajibikaji wa 'part time lecturers', ukizingatia kua, wanakua wanalinda kibarua chao ambacho hakiko imara.
Ila nina wasiwasi na wewe mtoa mada. Huenda utakua ni mwanafunzi unaetaka kulishwa kwa kijiko kama mtoto wa darasa la saba.
 
Leo nimeshangaa kusikia eti 'part time lecturers' hawakamilishi majukumu yao ipasavyo. Siku nyingi nilikua nikipata taarifa za kusifu uwajibikaji wa 'part time lecturers', ukizingatia kua, wanakua wanalinda kibarua chao ambacho hakiko imara.Ila nina wasiwasi na wewe mtoa mada. Huenda utakua ni mwanafunzi unaetaka kulishwa kwa kijiko kama mtoto wa darasa la saba.
Mkuu wapo wanaojituma kweli wanakuwa wapo social mda wowote ukimpigia akufahamishe anakusaidia akiwa mbali!!Ila wengine dah msaada hana kabisa!Tena anakwambia kabisa nikiondoka usinipigie au kunitafuta kabisa!Sipo hivo umenifikiria tofauti mkuu
 
Mkuu toa mfano wa hivyo vyuo vitatu ambavyo huyo lecturer anaweza akawa anafundisha kwa wakati mmoja ktk semester moja!

Pia ukiangalia uhalisia na kimantiki je inawezekana lecturer mmoja kufundisha kama part timer ktk vyuo 3 tofauti ktk semister moja..?!
Niko tayari kujuzwa zaidi.

inawezekana udsm wengi wanafundisha udom, st john, mzumbe wengine mpaka nje ya nchi hii hufundisha kwa njia ya extreme weeks each college/university.
 
Tatizo la vyuo ni kubwa kuliko hao part timers. . . . ..
1. We unaongelea darasa la watu mia tano unaona ni sawa??!!!!
2. Chuo kinasajiliwa na kinasajili course na kudahili wanafunzi huku hakina walimu unaona ni sawa??!!

Angalieni mfumo unavyopelekea matatizo yanayoonekana sio kuanza kunyoosheana vidole huyu hivi na yule ni vile. . . . .
 
Mkuu sitakutajia jina sina nia ya kuchafua chuo chochote!ila kukupa hint nenda mbeya ukajionee mwenyewe!!

Wewe ni sehemu ya tatizo au huna uhakika na data ya kutosha kuongea ndio maana unshindwa
 
PM maana yake ni Private Message. . . . . . .mimi na wewe tuna nini private juu ya wahadhiri part timers au mustakabali wa elimu ya juu??!!
mkuu mbona sikuelewi!umetaka majina ya vyuo nnavyovihamu we ka una shida navyo nitafute PM nikutajie!!lengo la kupost ni kutaka tu baadhi ya hao walim wenye tabia kama hizo wajirekebishe sio vizuri kutaja vyuo!!mbona hili suala lipo wazi tu wanafunzi vyuo tunalijua!!
 
Mkuu toa mfano wa hivyo vyuo vitatu ambavyo huyo lecturer anaweza akawa anafundisha kwa wakati mmoja ktk semester moja!

Pia ukiangalia uhalisia na kimantiki je inawezekana lecturer mmoja kufundisha kama part timer ktk vyuo 3 tofauti ktk semister moja..?!
Niko tayari kujuzwa zaidi.

Mbona inawezekana kabisa sisi tulikuwa n tunafubdishwa n lecturer mmoja the same course Udsm duce na muce
 
Leo nimeshangaa kusikia eti 'part time lecturers' hawakamilishi majukumu yao ipasavyo. Siku nyingi nilikua nikipata taarifa za kusifu uwajibikaji wa 'part time lecturers', ukizingatia kua, wanakua wanalinda kibarua chao ambacho hakiko imara.
Ila nina wasiwasi na wewe mtoa mada. Huenda utakua ni mwanafunzi unaetaka kulishwa kwa kijiko kama mtoto wa darasa la saba.

Sijauona uhalisia wa anachosekisema mtoa mada.
Nnavyoelewa part time lecturer ni yule ambae ana kazi permanent chuo fulani lakini anafundisha part time chuo kingine.
Kumbuka hawa watu wana responsibilities kule kwa mwajiri wao hivyo wanapangiwa madarasa ya kufundisha pia.
Nnachotaka Mbaruck atueleweshe hapa inakuwaje huyo lecturer anaweza akafundisha vyuo 3 au zaidi katika semester moja...., tukiamini pia anatakiwa afundishe ktk chuo alichoajiriwa! Je semester unayozungumzia ni ya wiki ngapi maana sielewi anajigawae ktk vyuo yote 3 au zaidi!!
 
mkuu mbona sikuelewi!umetaka majina ya vyuo nnavyovihamu we ka una shida navyo nitafute PM nikutajie!!lengo la kupost ni kutaka tu baadhi ya hao walim wenye tabia kama hizo wajirekebishe sio vizuri kutaja vyuo!!mbona hili suala lipo wazi tu wanafunzi vyuo tunalijua!!

A coward intellectual in making. . . ... hypocricy wont do you any good. . . . .facts will speak for themselves let the facts free and you will be free from subjectivity and mongering
 
Sijauona uhalisia wa anachosekisema mtoa mada.
Nnavyoelewa part time lecturer ni yule ambae ana kazi permanent chuo fulani lakini anafundisha part time chuo kingine.
Kumbuka hawa watu wana responsibilities kule kwa mwajiri wao hivyo wanapangiwa madarasa ya kufundisha pia.
Nnachotaka Mbaruck atueleweshe hapa inakuwaje huyo lecturer anaweza akafundisha vyuo 3 au zaidi katika semester moja...., tukiamini pia anatakiwa afundishe ktk chuo alichoajiriwa! Je semester unayozungumzia ni ya wiki ngapi maana sielewi anajigawae ktk vyuo yote 3 au zaidi!!
Nakubaliana nawe!huwa ni mwajiriwa wa chuo flan!Mkuu mfano mie ni lecturer wa udsm nimeajiriwa!nasafiri mpaka dodoma kufundisha wanafunzi wa udom kozi ya communication skills vitivo viwili bado nasafiri naenda morogoro kufundisha chuo chengine ndani ya hio miezi mi4 katika semester moja
 
Back
Top Bottom