Jana nimeona tbc wanasimulia maswaibu ya Jamaa aliyekimbiwa na Mke na kutelekezewa Watoto wadogo 2 huku hana uwezo wa kufanya kazi yeyote shida ikiwa ni ugonjwa wa Moyo kiasi kwamba tumbo limejaa mda wote,huruma sana.
Yaani si mzazi wake Wala Mke waliokuwa wako tayari kumsaidia ,Sasa badala hata wataje namba wakaishia hivyo hivyo Sasa wanategemea tutamfikiaje sie wenye vitu vidogo vidogo?
Mwisho hivi kiukweli inauma ikiwa watu wanapiga mabilioni ya umma huko harafu serikali inashindwa kuwahudumia watu hao wenye magonjwa makubwa makubwa ,walemavu na wazee na hapo hapo Ina kitengo Cha ustawi wa jamii nk..