"Chama cha Mapinduzi ni adui wa kila mtu. Mwalimu Nyerere alikuwa anapambana na maadui wangapi? Watatu, sindio? Ujinga, maradhi, na nani? Na umaskini.
Leo Chama cha Mapinduzi ni adui namba nne. Chama cha Mapinduzi. Ni adui wa wakulima, ni adui wa wafanyabiashara, ni adui wa maaskari ambao pia kikokotoo kikiwapiga vibaya mosi, sindio? Ni adui wa kila mtu Chama cha Mapinduzi, sindio ndugu zangu?
Leo tunalalamika Lissu yuko ndani kwa sababu adui huyu namba nne aliyeongezeka, ambaye ni Chama cha Mapinduzi- Amesema Pascal Haonga Kada wa CHADEMA Jimbo la Mbozi