Pascal Mayala: Nilitangaza Maalim Seif Ameshinda Urais Zanzibar, Tukapata Matatizo'

Pascal Mayala: Nilitangaza Maalim Seif Ameshinda Urais Zanzibar, Tukapata Matatizo'

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mwandishi wa habari mkongwe Pascal Mayalla amesema kuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, ambao ulikuwa uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi nchini, alitangaza kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ameshinda urais wa Zanzibar. Amesema baada ya taarifa hiyo, kituo chao cha DTV kilikumbwa na matatizo mbalimbali, ikiwemo kutozwa faini na kufutwa kwa kipindi chake.

Pascal Mayalla ameyasema hayo kwenye kipindi cha Nijuze akileeza safari yake ya miaka 30 ya Uandishi wa Habari

ZEC haikutangaza matokeo kwa siku tatu mfululizo (bila bila). Hatimaye, siku tano baada ya uchaguzi, ZEC ilimtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi, jambo ambalo CUF na watu wengine hawakuamini.

Kutokana na kutangaza matokeo hayo kabla ya tume, kituo cha DTV kilipigwa faini, na kipindi cha "Mada Moto" kilipigwa faini na kufungwa

 
Back
Top Bottom