JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 1,011
- 1,681
Mwandishi wa habari kutoka PPR Media, Pascal Mayalla ameiomba Serikali kuwapa posho waandishi wa habari pale wanapotekeleza majukumu yao kama ambavyo wabunge hulipwa posho kila wanapohudhuria vikao wakati wakitekeleza majukumu yao.
Aidha, Mayalla amesema baadhi ya posho wanazopewa waandishi wa habari wakati wakitekeleza majukumu yao (brown envelope) isichukuliwe kama rushwa kama ambavyo wengi huona hivyo, kwani kitu hicho hufanyika hata kwa watu wa taaluma zingine akitolea mfano wanasheria na wabunge ambao hupewa posho baada ya kushiriki vikao katika sehemu za kazi zao.
Mayalla amesema hayo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo Novemba 18, 2024, wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya habari kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ambapo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.
SOURCE TBC ONLINE