Pascal ana hoja.
Hi tabia ya kuzuia kuambiwa naona imekithiri sana.
Ni kweli kuwa muhimili wa bunge unaingiliwa sana. Mfano halali ni pale mkuu wa kaya alipomwambia spika awashughulikie wapinzani ndani ya bunge, wakitoka nje ana deal nao. Ile ni kama amri na imeingilia madaraka ya spika.
Tanzania inapotea kidemokrasia
Wakati nikiwa Sekondari, kuna siku kulitokea ugomvi darasani kati ya mwl na mwanafunzi. Ilikuwa hivi: huyo mwl alikuwa akifundisha Chemistry, ila ki ukweli alikuwa mwl 'siyawezi'! Nadahni watu wazima wananielewa hapa. Sasa kuna mwanafunzi badala ya kumsikiliza mwl, akawa anaandika nukuu (notes) za somo jingine. Mwl alipomwona aling'aka, akafura, akamkwida shingoni. Baada ya yule mwanafunzi kukosa hewa, akajitetea na yeye akamkwida mwl.
Baadaye mwl. akatoa taarifa kwa Headmaster kuwa ameshambuliwa na mwanafunzi. Wote tukajua kuwa yule mwanafunzi atafukuzwa shule. Sasa siku moja tuliitwa ofisini kwa Headmaster kama mashahidi tulioshuhudia tukio hilo. Mwl husika hakuwepo ofisini. Baada ya ushahidi wote kutolewa, Headboy ambaye naye alikuwepo ofisini akamlipua mwl kuwa ni mwl 'siyawezi'! Wote tukajua atashughulikiwa. Cha ajabu Headmaster alimshukuru sana na alisema maneno haya:
'Umetusaidia sana kujua chanzo cha tatizo, kwa sababu Serikali ya wanafunzi ni jicho la tatu la utawala ambalo kazi yake ni kuona kule ambako utawala hauwezi kuona'.
Sasa hii kesi ya brother Paschal naifananisha na ile ya mwanafunzi na mwl. Ina maana hawa waheshimiwa sana hawataki kuoneshwa kule ambako hawawezi kuona, hawataki kukosolewa kwa kuwa wanadhani hawawezi kukosea. Sasa kama wanadhani wao ni wakamilifu hawakosei, huko makanisani na misikitini wanakoshinda tunawaona kwenye ma kamera wame
bow na kunyeyekea wanaenda kufanya nini? Wanamdhihaki Mungu? Maana kwa sisi Wakristo tunaamini kwamba sisi ni wenye dhambi, na hata Yesu alitumwa kutukomboa wakosefu, akafa msalabani kwa ajili yetu!
Lakini uzuri, Mungu hamfichi mnafiki. Jaribu kuangalia picha za hao wajumbe wa kamati. Hakuna hata mmoja ambaye amemwangalia usoni Paschal. Ni kama
their faces are guilt. Hawana
confidence na kitu wanachokifanya, kwa hiyo ni unafiki tu! Kwa sababu, kama wanavyodai mtuhumiwa amelidharau Bunge
which is a serious allegation. Nilitegemea wajumbe wote wam
face Paschal
squarely ili waone
Eye activity ya Paschal ambayo kitaalam itawapa dondoo kama ana hatia ama la! Hapa nadhani wataalam wa
interrogation watanielewa.
Lakini mwisho wa siku, haya yote yana mwisho. Kitu cha milele ni Mungu tu, lakini madaraka, cheo, pesa, utajiri ni vya kupita tu!