Pascal Mayalla kazeeka haoni mbele

Nilikuwa namfatilia enzi hizo nikiaa youngster kabisa

Toka enzi za kitimoto sijui DTV au channel ten ile.

Then vipindi vya sabasaba TVT.

Nilipojiunga JF miaka 10 iliyopita nilivutiwa na mtu aitwa pasco hakuwa anapindisha ukweli na hakuw a mtu wa kuegemea upande wowote wa siasa. That's made he legendary kabisa na heshima yake iiikuwa kubwa maradufu.

Baadae nikaja ng'amua kuwa pasco ndio Pascal mayalla.

Sasa sense aanze kujiita oascal mayala humu amekuwa sio yule pasco tuliemjue .

Old version of pasco aliishia pale magogoni the day alipoambiwa mayalla kwa kizilanKENDE ni "njaa"

Aliitwa kule dodoma kwa yule mgogo ndio wakam-cement kabisa the new born again Pasco.

Halafu akaja kuwa pasco the shaman prophet of doom ambae bado anaamini kwa daudi albert bashite ni mtu sahihi kuwa mkuu wa kaya.just imagine [emoji15][emoji849] ndugu msomaji.

Ngomaa ikivutwa sana hupasuka, na grafu lazika i bend down haiwezi paa kila siku.

Unajua atakuambia "read between the line" mambo ya facts open atataka u storm akili uchanganyikiwe umuone ni yupe yule pasco the intellectual.

Apewe tu ukuu wa wilaya.

He is heading 60 soon na Hana pension serikali imkumbuke kilazima
 
Kitimoto ninayoikumbuka sana ni ile siku aliyokua anahojiwa Waziri wa Fedha Danieli Yona
Alipigwa maswali magumu sana, lakini Mheshimiwa Waziri alikua mzima kichwani naye anajibu vizuri sana. Au kwakua nilikua kidato cha kwanza hivo niliona ngoma droo hakuna mshindi.
 
ID nyingine ya Paskali wa JF
Ukiona vyaelea, vimeundwa. Humu JF tumetoka mbali, usisahau tulianza na pasco...
The Imp said:
Aliitwa kule dodoma kwa yule mgogo ndio wakam-cement kabisa the new born again Pasco.
Inaitwa induced axolotls metamorphosis kwa lugha ya kitaalam!
Watu waliomjua Pascal Kupitia JF pekee poleni sana.
Tuliomfahamu toka wakati wa KITIMOTO katu hatushangai! Je una hakika gani anayetumia ID ya Pascal Mayalla ni yule yule wa zama?

Kuna kuzeeka na kuzeeshwa kama ilivyo kung'atuka na kung'atuliwa, kutumbua na kutumbuliwa. Kumbuka kiumbe anayeweza kubadilika na kubaki yule yule ni kinyonga peke yake
 
Na mbaya zaidi kaanza kuwa "prophet of doom" he always wishes doomsday to come in Tanzania for his devilish foresight about someone the "damned"

Na wote tuseme Amina ,
Mkuu The imp, kuna kitu umekisema hapa, Pascal Mayala kazeeka haoni mbele tarehe 25 mwezi 9, mwaka 2019 kunihisu mimi, halafu kilikuja kutokea kweli!. Nikisoma hapa ulisema nini kunihusu na nikipima na kilichokuja kutokea, kiukweli, naanza kujiogopa!.
Nakupitisha kwenye baadhi ya mabandiko yangu uangalie tarehe ya mabandiko hayo, nilisema nini lini na nini kimekuja kutokea kuhusu hicho nilicho kisema!.

The most powerful thing in this world is the power of will!.
Japo kuna msemo kuwa kauli huumba, kumbe kiukweli, kinachoumba sio kauli, bali the will ikiyoko ndani ya hiyo kauli.
If the will is strong enough, you can wish anything and it will happen or materialize!
P
 
Hii ni ID nyingine ya Paskali wa JF?
Mkuu nguvu , huyo Allyoki ni verified name, ndie mmiliki mwenza wa Masai Studio waliokuwa watayarishaji wa kipindi cha Kiti Moto, mimi nilikuwa just a presenter. Tena presenter wa kwanza wa Kiti Moto ni Betty Mkwasa.
Ila pia tangu kuanzishwa kwa TV Bongo, mimi ndio nilikuwa mtangazaji wa kwanza wa TV Talk Show Host kipindi cha "Mada Moto" on DTV, kipindi hiki kiliandaliwa na Abantu Studio ya Beatrice Mugishagwe akishirikiana na Mjerumani Wolfgang Baraniek, mwaka huo wa 1995 na ndio my first time kushika a 6 figure!. By then young with no family responsibilities, kiukweli... I just thank God, I'm alive!, maana kijana with no future plans kushika a 6 figure 1995!, it was very dangerous!. Nilioa chap chap, vikao ni Club Bilcanas, Honeymoon London!, then US!, nikashuka Bongo na Harley Davidson!.
P
 
Mkuu Mag3 , tangu nimejiunga JF, sijawahi kutumia fake I.D, nimejiunga as Pasco, (wajf) baadaye nikaongeza account ya pili ya Pascal Mayalla hivyo nika exist in duality, na baadae nika merge Pasco na Pascal Mayalla, sijawahi kuwa na fake ID yoyote!.
Kuna kuzeeka na kuzeeshwa kama ilivyo kung'atuka na kung'atuliwa, kutumbua na kutumbuliwa. Kumbuka kiumbe anayeweza kubadilika na kubaki yule yule ni kinyonga peke yake
Kiukweli mimi nimejizeekea tuu sijazeeshwa!.
P
 
sidhani kama kashagonga sitini...hapana nafikiri bado bado anasogea...afu kuna mzee mmoja alishasema kazi ya ofisini si kama kazi ya kuchanganya zege!! ha ha ha
Mkuu FUSO , you are absolutely correct, mimi ni wa late 60s, hivyo bado sijagonga 60 ila ndio naelekea!.
P
 
Kuna wakati nasoma kwa makini hoja zake ah nami hujiuliza vipi huyu but kuna wakati naona anatumia kitu katika fasihi kinaitwa "irony' yani mtu kusema kitu kumbe ni kama kinyume chake.
Mkuu mzamifu , nimefarijika sana na mchango wako huu kwasababu kiukweli kabisa wewe ni mzamifu na unazama kweli kweli!. A level nimesoma fasihi, kufuatia mwana JF mwenzetu humu kupotea katika mazingira ya kutatanisha baada ya kupost humu mada fulani iliyomhusu mtu fulani. Kwa vile no one knows what really happened if it was a friendly fires or ni wale 'jamaa' zetu!.

Every reasonable person would be very careful and takes every precautions nisije kuwa next!
Pia makala zake nyingine ni kama zinaonyesha ana uoga fulani kwa kuzifanya ziinamie upande anaouhofia.
True kabisa, kama umeumbwa kwa mwili wa nyama, lazima utaogopa,
Anyway historia ya uandishi wake hunifanya niendelee kumsoma lakini insnipa kazi kutafakari zaidi kulikoni!
That is good na bado naandika.
P
 
Mkuu Fabolous umenikumbusha mbali.
Daniel Yona is very smart.
P
 
Mbaya zaidi anazeeka na umasikini wake
Mkuu Kifurukutu , acha kufurukuta, it's not true kuwa nazeka na umasikini wangu, kiukweli kabisa mimi ni tajiri sana wa roho japo ni kweli ni masikini wa mali.

Kuna watu utajiri wa mali makes them happy, kuna tajiri fulani namfahamu, hawajawahi kuwa real happy, halafu kuna watu masikini wa mali kama mimi na matajiri wa roho, we are really happy and we enjoy life to the fullest!, we live for today as if hakuna kesho, tukipata pesa tunazitumbua kisawasawa, zikiisha tunatulia.
Pamoja na umasikini wangu huu, I have no any regrets kwa jinsi tulivyoponda raha enzi tunazo, tulikuwa tunakwea pipa kama daladala kwenye London, Paris, New York, Rome kwenda kuchilly tuu!.
Sasa tumezeeka, pesa tumeishiwa, usafiri wetu ni daladala na ndege tunazionea hewani only.
That is life and I am very happy now, nikiikumbuka enzi zile nina meno, sikumbuki kuna nyama gani sijatafuna!, ukikumbuka tuu ile raha ya kutafuna nyama, hata ukila mchicha, au kushindwa maji na usiku kupiga 'pasi ndefu' ile raha ya kutafuna nyama ambayo imebaki moyoni, kupitia kitu kiitwacho stigimata, unapata raha kweli kama unatafuna nyama, it makes me very happy always.

P
 
That is life and I am very happy now, nikiikumbuka enzi zile nina meno, kuna nyama gani sijatafuna!, ukikumbuka tuu ile raha imebaki machoni, it makes me very happy always.[emoji23]
 
Watu waliomjua Pascal Kupitia JF pekee poleni sana. Huyu jamaa hanijui lakini Mimi namjua sana.
Mkuu lee van cliff , thanks for this
Watanzania wengi twamjua sana, EAC wengi wanamjua sana ingawa yeye anawajua kwa kuwaona watu wachache sana lakini mamilioni ya watu tunamjua.
Thanks too for this
Kwa sababu gani?

Kwa sababu ni mtu mtangazaji marufu Sana hapa Tanzania
Mtangazaji maarufu wa zamani.
Kiukweli mwanzilishi wa jina la kipindi cha "Kiti Moto" sio mimi, mimi nilikuwa ni mwendeshaji tuu wa kipindi. Kipindi cha Kiti Moto kilikuwa ni kipindi kinachoandaliwa na Masai Studios, mwanzilishi ni Allyoki ambaye pia ni member wetu humu JF.

Wakati wa uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi, Mama mmoja wa Kihaya, Beatrice Mugishagwe na studio yake ya Abantu Vision ali team up na Mjerumani Wolfgang Baraniek wakaanzisha kipindi cha kwanza cha TV Talk Show Tanzania, kiitwacho "Mada Moto" na mimi ndio nikateuliwa kuwa mtangazaji wake, hivyo mimi Pasco Mayalla kuwa ndio the pioneers mtangazaji wa kwanza wa TV Talk Show Tanzania kupitia DTV.

Baada ya uchaguzi mkuu project ya Mada Moto ilikwisha ndipo Masai Studios wakainuka na kipindi cha Kiti Moto.

Kipindi kilianza kwa kuendeshwa na Betty Mkwasa, kisha akaja Ephraim Kibonde, Betty Mkwasa akanipigia cross nikatua Masai Studios na kuwa mwendeshaji wa kudumu wa kipindi hicho.
Asante, hili nimeisha lifafanua
Huyu Pascal wa JF sio yule, najua kazeeka yule alikuwa Bomba akiwepo kwenye press live akipewa nafasi ya kuuliza swali watazamaji wote utulivu ili kumsikiliza.
Kwa upande wa maswali mpaka sasa bado niko vile vile wala sijazeeka kivile!. Naamini hili swali ulilionaga Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli kwa hivyo sijazeka kivile!
Huyu wa JF kazeeka. Ameamua kukubalika kutukanwa mitandaoni kisa anatoa mada ngumu kuzielewa kwa vijana wa leo. Mada za mafumbo, za kuuma na kupuliza, za kutotaka lawama, anaishia kutukanwa na madogo.
It's true madogo wa sasa hawapendi kushirisha mental faculties zao, kuna issues nyingine ni ngumu kuzieleza hivyo kujikuta lazima uziongee kwa parables mfano issue kama hii kuhusu uchaguzi wa 2020 Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!
Yeye ukimlaumu atakuambia
"Read between the lines"
It's true kwa sasa nimejizeekea, naendelea kuandika makala za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo sasa ni ajili ya wote lakini zile hoja specific kwa watu maalum, lazima, ziendelee ambazo ili kuzielewa ni lazima uwe na uwezo to read in between the lines.

P
 
Give credit where it is due! Ubora na umaarufu wa "kiti moto" ni zao la Paschal Mayalla mwenyewe; kwa tunaomfahamu Paschal kitaaluma yeye ndiye alikuwa the brains behind the success of Kiti Moto; ile ilikuwa live interview sio studio production!
 
Ni watu wawili tofauti.wazamani alifatuta washabiki kwa nguvu zote. bila kujali cheo cha mwanasiasa ili aridhishe mashabiki.na huyu wa sasa anajikomba kwa wanasiasa ili aweze pata uteuzi.kwani wanahabari wengi waliokuwa hata siyo level yake tayari wamelamba teuzi yeye bado.hii kitu inamchanganya.
 
Baada ya kuona ID inaanza 'Kudoda' na 'Kufifia' sasa ni mwendo tu wa Kujianzishia Mada za 'Kipopoma' kwa ID zetu mbadala ( za akiba ) kisha Kujisifu ( Kujipakulia Minyama mingi ) ili Umaarufu usipotee JamiiForums japo ulishapotea baada ya kupata Kura 'Moko' tu katika Kura ya Maoni CCM ( 2020 ) Jimboni Kawe.
 
Mchambuzi wa siasa na uchumi. Mwaandishi wa uchunguzi wa habari. Mwanasheria. Kaka.
Bado yuko vizuri. Labda ni sisi tusiyemuelewa. Labda hatusomi nakala, mabandiko vizuri. Siyo kosa lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…