Pascal Mayalla na Jacton Manyerere wakubaliana na Spika Ndugai kwa uamuzi wa kumrejesha Mwambe na wabunge 4 waliofukuzwa CHADEMA

Hata Mbowe akiteuliwa kuwa Katibu mkuu wa wizara, anawaachieni Chadema!
Mpaka sasa keshawathibitishia msimamo wake HADHARANI.
Mmeisha hangaika sana kumrubuni, kumtisha mpaka hata kwa kumharibia biashara zake lakini bado yuko imara.
Wa aina hii wanazidi kuwa ADIMU hapa TZ na hata Africa.
Mungu atazidi kumbariki na kumuongezea UIMARA ili aushinde moto huu wa majaribu.
 
Biashara gani aliyoharibiwa?!
 
Nilikuwa mfuasi nkubwa Sana wa Pasukali enzi zake za ubora wa mawazo yake. Tangu alipoambiwa na tafsiri ta mayala kisukuma Kuwa ni njaa, basi nayo nguvu ya kufikiri imrgeukia njaa. Hana mvuto tena namnet mabandiko yake. Nayaruka kula nionapo maana kuyasoma kunaniharibia siku.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwashee unapaswa kwenda na wakati......usikariri maisha!
 
Pascal Mayalla,

..wakati mwingine ni bora uwe unajibu " ..no comment.." kuliko kujibu kwa mafumbo-mafumbo ambayo huishia kuipotosha jamii.

..uandishi na majibu ya mafumbo, pamoja na kwamba unakuepusha wewe na mkono wa sheria, unawapoteza na kuwapotosha vijana wengi ambao wako naive na hawawezi kuutambua ujumbe ulioko "between the lines."
 
Lakini pascal mayalla alijaribu kufafanua maana ya exclusive power walizonazo viongozi wa mihimili,wewe mtoa mada hukusikia uchambuzi vizuri ni vizuri ukalejelea upya kile kipindi ili ujiridhishe
 
Lakini pascal mayalla alijaribu kufafanua maana ya exclusive power walizonazo viongozi wa mihimili,wewe mtoa mada hukusikia uchambuzi vizuri ni vizuri ukalejelea upya kile kipindi ili ujiridhishe

..kuna katiba na sheria, halafu kuna "exclusive powers."?

..sasa hapo ndiyo kuna uchochoro wa kuvunja sheria, na kuwa na double standards.

..kwa mfano, "exlusive powers" za Spika zilitumika kumfukuza ubunge Nassari bila kumpa nafasi ya kujitetea.

.."exclusive powers" hizo tena zinataka kumrudisha bungeni Cecil Mwambe ambaye kwa hiari yake alikihama chama chake.

..Spika anadai anataka barua ya kikao cha CDM kumvua uanachama Cecil Mwambe!! Barua ya namna hiyo ya nini wakati Mwambe alitangaza mwenyewe ktk vyombo vya habari? Na muda umepita bila Mwambe kukanusha habari hizo, na pia ameacha kuhudhuria vikao vya bunge.
 
Mwambe amesema wazi kuwa yeye ni mwanachama wa CCM na kuwa anatarajia kuingia tena Bunge kupitia chama hicho. Hivyo amerudi Bungeni kama mwanachama wa CCM anayewakilisha jimbo lake kupitia Chadema. Go figure.

Amandla....
 

Yatupasa kujua kuwa hiyo ni Bluetooth spika na inakuwa remoted toka mbali. Hiyo spika inatoa sauti ya anaye miliki microphone.
Sasa kama boss wake anataka iwe hivyo, yenyewe itasema nini tofauti na boss?
Kama jambo linaibeba ccm, basi serikali yake itaweka nguvu zote hata kama hilo jambo lina madhara kwa uma.
 
mtu kutangaza tu haitoshi kumvua uanachama bali ilitakiwa kamati ikae imuhoji kwa utovu wa nidhamu,kwa kuzingatia katiba,kanuni na taratibu za chama
 
mtu kutangaza tu haitoshi kumvua uanachama bali ilitakiwa kamati ikae imuhoji kwa utovu wa nidhamu,kwa kuzingatia katiba,kanuni na taratibu za chama

..alitangaza kuhama cdm, na kujiunga na ccm.

..halafu akaacha kuhudhuria vikao vya bunge.

..maana yake ni kwamba anafahamu kwamba ubunge wake ulikoma kwa maamuzi yake ya kujiunga na ccm.

..kwa maoni yangu cdm hawana haja ya kusumbuka naye, kwani si mwanachama wao.

.. spika atakuwa anavunja sheria akimruhusu arudi bungeni.

..hebu ona hapo chini. Sasa mtu aliyekabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CCM Spika anamrudisha bungeni kwa misingi ipi?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…