Pascal Mayalla na Jacton Manyerere wakubaliana na Spika Ndugai kwa uamuzi wa kumrejesha Mwambe na wabunge 4 waliofukuzwa CHADEMA

Pascal Mayalla na Jacton Manyerere wakubaliana na Spika Ndugai kwa uamuzi wa kumrejesha Mwambe na wabunge 4 waliofukuzwa CHADEMA

Wakuu Dotto Bulendu, Pascal Mayalla na Jackton Manyerere wako mubashara Star tv wakijadili uhalali wa Spika Ndugai kumrejesha bungeni Cecil Mwambe na kuwabakiza bungeni Selasini, Silinde, Komu na Lwakatare.

Pascal anasisitiza kuwa Spika ana nguvu za " ziada" katika kufikia maamuzi fulani kama ilivyo kwa Rais na Jaji mkuu na kwa kutumia nguvu hizo maamuzi ya Spika Ndugai ni halali kabisa.
Jackton Manyerere anakubaliana na Pascal katika hili.

Mjadala unaendelea, karibu.

Maendeleo hayana vyama!
Natumai Pascal aliambatanisha na kifungu cha sheria zinazompa ndugai mamlaka hayo.
 
Wanasemaga paskali siku hizi anaongea kinyume kinyume, ili kulinda kitumbua chake, pale penye kusema wewe mbaya anaweka mzuri, yaani mfanoi baada kukuambia utaenda motoni anasema kwa wizi huo uliofanya unaenda peponi kabisa, wakati kila mtu anajua mwizi sehemu yake ni wapi, kifupi jamaa anafanya ucomedy.

nani anataka mambo ya kutekana mchana kweupe, siku ukutwe imejinyonga huko mwabwe pande wakati miti imejaa tele kila sehemu mpaka uifate Ile kule ya mwabepande, sijui ukijinyonga nayo unaenda peponi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana Lumumba wanasema Magu ni nabii na Covid imeshaisha kwa Tz/Africa.

Nguvu kubwa sana inatumika ku suppress issue ya Corona badala ya kupambana na Corona.

Angalia pale juu trending zote ni Corona. Ila angalia vi nyuzi uchwara kwenye majukwaa mchanganyiko na siasa kujaribu kuhamimisha magoli. Mara CHADEMA, mara mtatiro nk.

Hatudanganyiki:

IMG_20200516_085252_391.jpg
 
Wakuu Dotto Bulendu, Pascal Mayalla na Jackton Manyerere wako mubashara Star tv wakijadili uhalali wa Spika Ndugai kumrejesha bungeni Cecil Mwambe na kuwabakiza bungeni Selasini, Silinde, Komu na Lwakatare.

Pascal anasisitiza kuwa Spika ana nguvu za " ziada" katika kufikia maamuzi fulani kama ilivyo kwa Rais na Jaji mkuu na kwa kutumia nguvu hizo maamuzi ya Spika Ndugai ni halali kabisa.
Jackton Manyerere anakubaliana na Pascal katika hili.

Mjadala unaendelea, karibu.

Maendeleo hayana vyama!
Hiyo nguvu ya ziada waliyonayo ipo kwenye katiba? Ipo kwenye kanuni za bunge?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal anasisitiza kuwa Spika ana nguvu za " ziada" katika kufikia maamuzi fulani kama ilivyo kwa Rais na Jaji mkuu na kwa kutumia nguvu hizo maamuzi ya Spika Ndugai ni halali kabisa.
Jackton Manyerere anakubaliana na Pascal katika hili.
Hapa Pascal amepotosha. Alianza vizuri kueleza kuwa Raisi hata akishauriwa, hafungwi na ushauri wowote, maamuzi ni yake. Hili halina ubishi kwani sheria pia husema hivyo. Ameboronga alivyo sema kuwa kwa spika ni hivyo hivyo katika muktadha wa uondolewaji wa wabunge. Hapa kuna sheria na kanuni ambazo zinamfunga kila mtu-chama, bunge na serikali. Spika hana "discretion" hapa -kama chama kimefuata sheria katika kumfukuza mbunge uanachama, mbunge huyo anakuwa ana chama na anafukuzwa mara moja vinginevyo anaweza kwenda mahakamani (kama Zitto na wengine walivyofanya). Spika atakataa kuwafukuza ubunge tu akijiridhisha kuwa chama kimekwenda kinyume na sheria. Hili la kusema mbunge anawatumikia wananchi sitamuondoa ni ujinga au upumbavu, kwani kwa Tanzania mbunge hutumikia wananchi kupitia chama chake (na sheria yetu husema hivyo). Hata Raisi kama chama chake kitamfukuza basi anamwaga unga. Ukimruhusu Spika kutumia utashi wake na si sheria ndio haya tunayo yaona. Hati Mwambe hajaandika barua kwa Spika-Mwambe ana kadi ya CCM na amehama chama hadharani, lakini kwa kuikomoa CDM basi spika anaamua (na Pascal na Manyerere wanaona poa tu). Wabunge wa CUF waliondolewa bungeni kwa speed ya umeme hakukuwa na tahadhari yeyote. Speed ile ilikuwa kukwepa yanayoweza kutokea kama watakwenda mahakamani. Kwa ufupi Spika Ndugai anatumia ubabe wa ubovu wa sheria na kanuni za bunge kufanya haya maamuzi.
 
Nguvu kubwa sana inatumika ku suppress issue ya Corona badala ya kupambana na Corona.

Angalia pale juu trending zote ni Corona. Ila angalia vi nyuzi uchwara kwenye majukwaa mchanganyiko na siasa kujaribu kuhamimisha magoli. Mara CHADEMA, mara mtatiro nk.

Hatudanganyiki:

View attachment 1451521
Aisee hapo kwny trending news zote ni za mambo ya Corona mkuu.
 
Aisee hapo kwny trending news zote ni za mambo ya Corona mkuu.

Ukiona hivyo ufahamu nyingi ya mada zingine zote kwenye majukwaa yote ni za kubumbabumba kujaribu kubadilisha upepo bila ya mafanikio.

Dalili ya kuwa misukule inashindwa.
 
Tangu walipomuingiza mayalla kwenye hicho kipindi cha jicho letu ndani ya habari nshakizarau hicho kipindi sikufuatiliagi hata,eti mayala anajiita mwanasheria nguli jamanii dah....huku ndiko kusoma bila kuelimika,hata mtoto wa civics wa form one anajua kilichofanywa na redio sio sahihi
 
Back
Top Bottom