Pascal Mayalla na Jacton Manyerere wakubaliana na Spika Ndugai kwa uamuzi wa kumrejesha Mwambe na wabunge 4 waliofukuzwa CHADEMA

Pascal Mayalla na Jacton Manyerere wakubaliana na Spika Ndugai kwa uamuzi wa kumrejesha Mwambe na wabunge 4 waliofukuzwa CHADEMA

Hapa Pascal amepotosha. Alianza vizuri kueleza kuwa Raisi hata akishauriwa, hafungwi na ushauri wowote, maamuzi ni yake. Hili halina ubishi kwani sheria pia husema hivyo. Ameboronga alivyo sema kuwa kwa spika ni hivyo hivyo katika muktadha wa uondolewaji wa wabunge. Hapa kuna sheria na kanuni ambazo zinamfunga kila mtu-chama, bunge na serikali. Spika hana "discretion" hapa -kama chama kimefuata sheria katika kumfukuza mbunge uanachama, mbunge huyo anakuwa ana chama na anafukuzwa mara moja vinginevyo anaweza kwenda mahakamani (kama Zitto na wengine walivyofanya). Spika atakataa kuwafukuza ubunge tu akijiridhisha kuwa chama kimekwenda kinyume na sheria. Hili la kusema mbunge anawatumikia wananchi sitamuondoa ni ujinga au upumbavu, kwani kwa Tanzania mbunge hutumikia wananchi kupitia chama chake (na sheria yetu husema hivyo). Hata Raisi kama chama chake kitamfukuza basi anamwaga unga. Ukimruhusu Spika kutumia utashi wake na si sheria ndio haya tunayo yaona. Hati Mwambe hajaandika barua kwa Spika-Mwambe ana kadi ya CCM na amehama chama hadharani, lakini kwa kuikomoa CDM basi spika anaamua (na Pascal na Manyerere wanaona poa tu). Wabunge wa CUF waliondolewa bungeni kwa speed ya umeme hakukuwa na tahadhari yeyote. Speed ile ilikuwa kukwepa yanayoweza kutokea kama watakwenda mahakamani. Kwa ufupi Spika Ndugai anatumia ubabe wa ubovu wa sheria na kanuni za bunge kufanya haya maamuzi.

Umenena vema kabisa. Natamani Pasval na mwenzake.wasome.hii post.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni Manyerere aliyejenga pale chini ya kwa Mwl Nyerere Butiama? Manyerere anataka ubunge wa Butiama hivyo lazima aseme hayo ili asije kukosa kupitishwa na jiwe mpitishaji kwenye kura za maoni.

Pasco yeye faili yake ipo kwa jiwe na anajua hilo anaogopa sana kesi ya utakatishaji pesa. Pasco endelea kua hivyo hivyo uvuguvugu unatafutwa sana na kesi ya utakatishaji pesa na kutengeneza ile software kama Tito Magoti na ...

Manyerere yeye akiendelea hivi mwakani mtamwona Bungeni kwa tiketi ya mupe muruke.
 
Wakuu Dotto Bulendu, Pascal Mayalla na Jackton Manyerere wako mubashara Star tv wakijadili uhalali wa Spika Ndugai kumrejesha bungeni Cecil Mwambe na kuwabakiza bungeni Selasini, Silinde, Komu na Lwakatare.

Pascal anasisitiza kuwa Spika ana nguvu za " ziada" katika kufikia maamuzi fulani kama ilivyo kwa Rais na Jaji mkuu na kwa kutumia nguvu hizo maamuzi ya Spika Ndugai ni halali kabisa.

Jackton Manyerere anakubaliana na Pascal katika hili.

Pascal anasema kuna madai mitandaoni kuwa kwa sababu Spika na naibu wake ni wana CCM wamekuwa na kuwaida ya kuwapendelea wabunge wa chama chao ndio sababu Lisu na Nassari walifukuzwa lakini Muhongo na Mkono bado wanadunda japo hawapo bungeni.

Manyerere ambaye anatoka jimboni kwa Mkono amesema mbunge wake ni mgonjwa kwa takribani miaka mitano sasa na amewataka watu waache kumsema sema vibaya kwani siyo utamaduni wa kitanzania kuwateta wagonjwa.

Wanamjadala kwa pamoja wanasema ni vema sasa Tanzania ikawa na wagombea binafsi kwa sababu hii hama hama haina tija ni sawa tu na Uhujumu uchumi.

Mjadala umemalizika, nawashukuruni sana Dotto Bulendu na Pascal Mayalla kwa mjadala huu.

Maendeleo hayana vyama!
Pasco mayala yuko kwenye project ya tokomeza UA Chadema, sijui kama inamlipa
 
Wakisema Ndugai hayupo sahihi ka TV ka watu katafungiwa! Kwa mazingira wanayozungumzia waacheni wazoze watakavyo! Ila kila mtu anajua Ndugai katowa boko la karne!

Sent using Jamii Forums mobile app
Katiba inasemaje kwa mtu asiye na dhamana ya chama cha siasa kuwa mbunge? Kweli matamko na matakwa ya mtu yawe juu ya katiba? Kweli Mayalla na Manyerere mnatetea uvunjifu wa katiba unaofanyika mchana kweupe? Basi mna matatizo!
 
uko umuhimu mkubwa mawazir icwe lazima wawe wabunge yaan rais achague yoyote anaoona anafaa na mbunge awe na uwezo wa kuhama chama au kuanzisha cha kwake huku akibaki na ubunge wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni Manyerere aliyejenga pale chini ya kwa Mwl Nyerere Butiama? Manyerere anataka ubunge wa Butiama hivyo lazima aseme hayo ili asije kukosa kupitishwa na jiwe mpitishaji kwenye kura za maoni.

Pasco yeye faili yake ipo kwa jiwe na anajua hilo anaogopa sana kesi ya utakatishaji pesa. Pasco endelea kua hivyo hivyo uvuguvugu unatafutwa sana na kesi ya utakatishaji pesa na kutengeneza ile software kama Tito Magoti na ...

Manyerere yeye akiendelea hivi mwakani mtamwona Bungeni kwa tiketi ya mupe muruke.
Pascal aonewe huruma kwa kutopata uteuzi licha ya kuunga mkono juhudi kwa nguvu zote. Karibuni amekosa kwa karibu sana kuteuliwa kujaza nafasi ya Sheria na Katiba ingawa sifa zote anazo ikiwa ni pamoja na Homeboy, kuunga juhudi na kuwa na njaa Kali. Tunaofahamu jitihada zake za muda mrefu za kutaka kuteuliwa, ile nafasi ya Mtwara iliyoachwa na Homeboy mwingine tulikuwa na uhakika atapata lakini alizidiwa kete. Hata hivyo amefikia hatua ya matumaini makubwa ya uteuzi nafasi ikitokea karibuni maana TV alikokuwa leo na kila Jumamosi ni ya Mwenyekiti. Tz bila wa kukubeba hufiki mbali!
 
Back
Top Bottom