Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Mbona sijaona ulichoandika hapo kumtuhumu huyo pascal?
What if walidukua mawasiliano ya Kabendera?
Lakini pia kumbuka kashtakiwa kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Wacha due process of law iamue.
Chanzo cha yyoteee hayo ni maandiko yake tunao jua tunajua usie jua kaa kimnya.
 
1.Sio atengwe aliyekuwa anaandika habari bila kufuata weledi na kuishia kutukana rais.
2. Unaposema hakumuita na kumuonya ina maana ye hakuwa anaingia humu jf na kusoma maandiko ya pasco au alikuwa anapuuza?
3. Kisha ndugu zake na mama yake wanapataje shida wakati alikuwa na backup ya watu wengi wakiwemo kina zitto, waende wakahudumie familia. Au anzisheni kapu la kuchangia familia yake.
4. Unapozichokoza mamlaka na kujiona shujaa jua tu utalipia gharama siku moja, ni suala la muda. Hata tundu lissu kalipia gharama. Na akiendelea atalipia tena. Kifupi dunia ina kanuni zake. Hiyo ni principle ya dunia nzima.
5. Lakini pia watz tumshukuru sana Pasco kwa kufichua habari za huyu kinyamkera ambaye ni ant government. Watu hawa wapo nchi nyingi tu. Lakini nadhani habari yake kwisha. Mtapiga makelele baada ya muda mtasahau na maisha yataendelea. Pengine atapelekewa tu tarifa za kifo cha mama yake kwa kukosa dawa. Kina zitto nao baada ya muda watakuwa bize na mambo yao na kumsahau kabisa.
 
Wewe unachuki binafsi na Pasco Mayala na unataka matatizo yako na Pasco yawe ya kila mtu. Hujaandika sababu ya msingi kwanini wanasigana kama ulivoandika, wanaugomvi? Kwanini amuharibie mwenzie? . Lakini pia hawa wawili kila mtu aliandika maoni yake kama wewe ulivokurupuka kuandika hii thread na the economist walivokurupuka kuchapisha habari bila kuifanyia utafiti.
 
Lipo bandiko lake humu kuhusu karma nadhani aliandika bila kulisoma.
038E136C-FAA8-422D-BB14-297B750A6BE6.jpeg
 
Kitu ambacho Pascal anaonyesha Udhaifu wake ni katika kumtetea Jiwe hili halina ubishi siku hizi hatumuoni akimkosoa zaidi ya kumsifia lakini bado jamaa yuko vizuri katika sekta yake cha msingi ni kutumia Critical thinking pindi unaposoma Makala zake
Hili linatoka moyoni mwangu, KAMA KUNA MTU MKABILA, MKABILA, ALIYETUKUKA NI Pascal Mayalla, A Tribalist and defined as : an advocate or practitioner of strong loyalty to one's own tribe or social group.
Pascal haoni doa lolote katika Jiwe, anamuona kama malaika Gabriel! Huyu naye akiwa Rais uwaja wa ndege utajengwa chooni kwake (if that could be possible anyway, he can dare do that!).
Mayalla namuheshimu sana enzi zake kabla ya Jiwe, sasa siye kabisa.
 
Pamoja na madhaifu yote alionayo Pascal Mayalla.... Lakini kwa hili naona wazi jinsi mleta mada ulivyo na chuki ya wazi juu ya unae mtuhumu.
Kimsingi alicho kifanya Pascal Mayalla ni kupinga kwa hoja gazeti la mabeberu. Na lengo lake kubwa haikua kumuumiza Erick Kabendera, bali lengo lake kubwa lilikuwa ni kujenga hoja kwa mtazamo tofauti kwa uwezo wake wa uelewa.
 
Nianze kwa kutoa rai kwa uongozi wa Jamii forum,naomba uzi huu usifutwe nmetanguliza ombi ilo kwani nina tambua ukalibu uliopo kati ya watumishi wa Jf na huyu Bwana mkubwa Pascally Mayalla.

Pia niombe wasomaji wangu mwelewe kuwa sina nia mbaya ninapo jarbu kuja na uchambuzi wa namna hii lengo langu ni kuoneshana kuwa nchi yetu iko hatarini hasa pale proffesionalbwa taaluma moja ambayo taifa linawategemea wanapo sigana katika jamii nani anae umia zaidi.

Nakumbuka siku za hivi karbuni gazeti la the Economist lilikuja na habar ambazo Mkuu Pascally aliziita kuwa ni habar za uwongo dhidi ya Rais wetu wa Tanzania.

Gazeti ilo liliwai kuja na habar kuwa "Rais wa Tanzania hapendi kukosolewe"

Gazeti ilo baada ya kuchapishwa Pascally Mayalla alikuja na bandiko la kupinga habar ile huku akionesha jinsi ambavyo sio kweli Rais wetu anapenda kukosolewa.

Alikwenda mbali zaid akamnukuu Rais wetu kuwa aliwai kuwambia wanahabar kuwa yeye anapenda kukosolewe ila akosolewe kwa Staha,na kwa hoja.

Pascally Mayalla kwenye andiko lake anatolea mfano kuwa yeye pascally Mayalla ni moja ya wanahabar ambao waliwai kumkosoa Rais na Rais alikubali kukosolewa kwa kumjibu huku akimtania.

HOJA.

kwanza lazma watu mjue kuwa andiko la Pascally kupinga habar ya the economist ndio iliyoamsha watu na kuanza kufatilia ni nani na yuko wapi anae ripoti habari hizo katika gazeti la the Economist?

Hapa naomba nieleweke,hata watumishi idara nyeti walianza kufatilia gazeti ilo baada ya kusoma bandiko la Pascally Mayalla hapa Jf, na ndipo wakaja kugundua kuwa kumbe mwandishi wa habar zile na nyeti kupitia gazeti lire ni ndgu yetu Fredrick Kabendera.

Kwa nini walifatilia,kiukweli kilichoandikwa na mwandishin huyo wa habari kilikuwa na ukweli wa 100%ingawa huyu Ndgu Pascally Mayalla alikipinga kwa lengo la KUJIPENDEKEZA KWA MSUKUMA MWEMZAKE.

je pascally Mayalla alijua tangu awali kuwa fredrick kabendera ndie anae andika habar nyeti na kuziripoti the economist na alishindwa kumuita kama mdogo wake na kumpa onyo?

Kimsingi kifungo cha Fredrick kabendera nadhani ni furaha kwa pascally Mayalla,kwani alimjua tangu awali na alishindwa kabsa kumuita na kumuonya ingawa wote wanatoka kanda ya ziwa.

Je Pascally alijua fredrick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?

Nadhani yote aliyajua ndio maana tangu fredrick awekwe korokoloni hajawai jitokeza popote kulaani kukamatwa kwa kijana huyu zaidi inasemekana ndo kwanza anatafta makala zote zilizoandikwa uko nyuma na kuzisoma na kuzifafanua kwa vijana wa idara nyeti ili kijana azidi kubanwa.

Andiko la Pascally Mayalla dhidi ya kumtetea ndugu yake liko hapa jf linauzi linaumiza kwani humo ndani anawataja wakosoaji wakubwa wa nchi hii ambao leo hii wamegeuziwa rangi ya unga wa ndere wao wanaita unga mweupe sasa huku wakila kuku kwa mirija.

Nasisitiza waandishi wa habar mtengeni Pascally Mayalla na waandishi wote wenye vinasaba vya ukabilana wanao shindwa kusimamia taaluma badala yake wanaishia kujipendekeza kwa kuofia uhai wao.

Natoa rai kwa Serikali ya Jamhuri kumwachia huru Fredrick Kabendera,tuspomdai kwa kisswahili tutawataka kwa kilugha, na hapo ndipo tutakapozzuia kiongozi yyte kuingia mkoa wa KAGERA mpaka "omwana weitu mumutishure.""
Kama kweli zile makala za economist ziliandikwa naye, ni haki kula jeuri yake. Ukimdhalilisha Rais wa nchi yako ni uhaini. Ni haki kubanwa.
 
Ndugu zanguni tuweni na ukosoaji ulio na faida kwetu sote, kumuingiza Pascal Mayalla kwenye sakata la huyu kabendera ni kuonyesha namna gani ulivyo na chuki dhidi ya Pascal.

Jamiiforum ni ulimwengu wa habari, watu hujadili na kupingana kwa hoja, Kabendera ni mtu Kama ulivyo wewe.

Hakuna shitaka lolote dhidi ya kabendera linaloonyesha Kuna uhusiano na kile alichokisema Mayalla dhidi yake,

Acheni kuleta ukabila, kutaja WASUKUMA ni kushindwa kutambua kuwa mtu muelewa hawezi kujenga hoja kwa misingi ya ukabila.
 
Back
Top Bottom