Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Mbona sijaona ulichoandika hapo kumtuhumu huyo pascal?
What if walidukua mawasiliano ya Kabendera?
Lakini pia kumbuka kashtakiwa kwa uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Wacha due process of law iamue.
Chanzo cha yyoteee hayo ni maandiko yake tunao jua tunajua usie jua kaa kimnya.
 
1.Sio atengwe aliyekuwa anaandika habari bila kufuata weledi na kuishia kutukana rais.
2. Unaposema hakumuita na kumuonya ina maana ye hakuwa anaingia humu jf na kusoma maandiko ya pasco au alikuwa anapuuza?
3. Kisha ndugu zake na mama yake wanapataje shida wakati alikuwa na backup ya watu wengi wakiwemo kina zitto, waende wakahudumie familia. Au anzisheni kapu la kuchangia familia yake.
4. Unapozichokoza mamlaka na kujiona shujaa jua tu utalipia gharama siku moja, ni suala la muda. Hata tundu lissu kalipia gharama. Na akiendelea atalipia tena. Kifupi dunia ina kanuni zake. Hiyo ni principle ya dunia nzima.
5. Lakini pia watz tumshukuru sana Pasco kwa kufichua habari za huyu kinyamkera ambaye ni ant government. Watu hawa wapo nchi nyingi tu. Lakini nadhani habari yake kwisha. Mtapiga makelele baada ya muda mtasahau na maisha yataendelea. Pengine atapelekewa tu tarifa za kifo cha mama yake kwa kukosa dawa. Kina zitto nao baada ya muda watakuwa bize na mambo yao na kumsahau kabisa.
 
Wewe unachuki binafsi na Pasco Mayala na unataka matatizo yako na Pasco yawe ya kila mtu. Hujaandika sababu ya msingi kwanini wanasigana kama ulivoandika, wanaugomvi? Kwanini amuharibie mwenzie? . Lakini pia hawa wawili kila mtu aliandika maoni yake kama wewe ulivokurupuka kuandika hii thread na the economist walivokurupuka kuchapisha habari bila kuifanyia utafiti.
 
Kitu ambacho Pascal anaonyesha Udhaifu wake ni katika kumtetea Jiwe hili halina ubishi siku hizi hatumuoni akimkosoa zaidi ya kumsifia lakini bado jamaa yuko vizuri katika sekta yake cha msingi ni kutumia Critical thinking pindi unaposoma Makala zake
 
Pamoja na madhaifu yote alionayo Pascal Mayalla.... Lakini kwa hili naona wazi jinsi mleta mada ulivyo na chuki ya wazi juu ya unae mtuhumu.
Kimsingi alicho kifanya Pascal Mayalla ni kupinga kwa hoja gazeti la mabeberu. Na lengo lake kubwa haikua kumuumiza Erick Kabendera, bali lengo lake kubwa lilikuwa ni kujenga hoja kwa mtazamo tofauti kwa uwezo wake wa uelewa.
 
Kama kweli zile makala za economist ziliandikwa naye, ni haki kula jeuri yake. Ukimdhalilisha Rais wa nchi yako ni uhaini. Ni haki kubanwa.
 
Ndugu zanguni tuweni na ukosoaji ulio na faida kwetu sote, kumuingiza Pascal Mayalla kwenye sakata la huyu kabendera ni kuonyesha namna gani ulivyo na chuki dhidi ya Pascal.

Jamiiforum ni ulimwengu wa habari, watu hujadili na kupingana kwa hoja, Kabendera ni mtu Kama ulivyo wewe.

Hakuna shitaka lolote dhidi ya kabendera linaloonyesha Kuna uhusiano na kile alichokisema Mayalla dhidi yake,

Acheni kuleta ukabila, kutaja WASUKUMA ni kushindwa kutambua kuwa mtu muelewa hawezi kujenga hoja kwa misingi ya ukabila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…