Kwenye uzi huu
Uchaguzi 2020 - RC wa Mwanza, John Mongela avunja Mwiko wa Kampeni Kwa Kuongea Ukweli Bayana!, "Tukimpa Mitano Tena, JPM Kuigeuza Tanzania Nchi ya Maziwa na Asali"
jana nilikuwa member wa kwanza kuchangia na kwakweli nilikerwa na uzi wa ndugu yetu Pasco. Nilikerwa kwakuwa ni yule muumini wa "Hayajatokea kwangu na familia yangu hivyo hayanihusu"
Niwie radhi maana nilikuporomoshea mzigo mpaka mods wakaamua kuufuta, aidha niombe radhi kwa wote niliowakwaza!
Nina swali moja tuu kwa Pasco, nimeamua kuacha mengine lukuki najua anayajua.
Je, Pasco hujui kuwa Ben Saanane tulikuwa naye humu tukijadiliana? Nani wa kupaswa kuulizwa alipo Ben? Nani tuliyemkabidhi ulinzi na usalama wa watanzania wote? Kwanini hajali kuhusu Ben? Je, Kazi zake zina baraka kutoka kwa nani hadi hiyo Ulaya ije Tanzania?
NB: Hilo ni swali moja tu! Yapo mengi nimeyaacha na unayajua.
Ipo methali moja inasema "Mchuma janga hula na wakwao"
Usije ukajiaminisha kuwa wewe siyo "Wakwao" ukifikiria hivyo basi unafanya kosa kubwa kabisa!
Kumpa Magufuli miaka mingine mitano ni kuchuma janga! Tukubaliane kwa lugha ya kawaida kabisa kuwa Rais wetu amepungukiwa kiasi kikubwa mno cha ubinadamu! Huo ni ukweli! Tusiupinge kwa kuangalia ubinafsi wetu kwa muda huu! Tuangalie jamii nzima kwa miaka mitano ijayo!
Ndugu yangu
Pascal Mayalla, nakusihi jikalie kimya tu kama walivyoamua kina
barafu na
Mzee Mwanakijiji. Hawa wameamua kuona aibu baada ya kutokujua uhalisia hapo kabla. Kumnadi Magufuli ni kukosa hofu ya Mungu! Usiruhusu hilo likatokea kwako!