Mgombea Mbunge kupitia Chama cha CHADEMA azindua kampeni ya Ubunge kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 mbele ya mkutano wake mkubwa wa kwanza jimboni Mbozi mkoani Songwe.
Mgombea Paschal Haonga akiwania kuchaguliwa kwa mara nyingine kupitia CHADEMA leo tarehe 27 Agosti 2020 amewaomba pia wamchague Tundu Lissu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kura nyingi hapo Oktoba 28 2020.
Uchaguzi Mkuu 2020 CHADEMA jimbo la Vwawa mgombea awasilisha rufani Dodoma
Fanuel Mkisi mgombea aliyeteuliwa na CHADEMA kusimama katika uchaguzi ngazi ya ubunge ktk eneo bunge la Vwawa mkoani Songwe azungumza
Fomu namba 12 ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Vwawa mkoani Songwe, kumuengua mgombea Fanuel Mkisi imefika katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa mjini Dodoma ili ndoto na haki za wananchi wa jimbo la Vwawa kumchagua mbunge wanayemtaka .
Hapo awali
Agosti 12 2020
Paschal Haonga na Fanuel Mkisi wateuliwa wa CHADEMA walipofika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mbozi anayesimama kama Msimamizi wa Uchaguzi wa majimbo mawili ya Vwawa na Mbozi kuchukua fomu