Uchaguzi 2020 Paschal Mayalla hufai hata kuongoza kitongoji

Uchaguzi 2020 Paschal Mayalla hufai hata kuongoza kitongoji

Hichilema,
!
Bro Usimlaumu Bure Mzee Wa Watu. Uwezo Wake Wa Kufikiria Ndio Umeishia Hapo Ulitaka Afanyaje? Besides, Unajua Chama Anachotokea Huwa Kinauwezo Wa Kumbadilisha Mtu Kutoka Polepole Wa Katiba Mpya Mpaka Huyu Mwenezi Wa Sisiem. Kwa Hiyo Kwa Maoni Ynagu Kama Kasema Hivyo Mpongeze Kajitahidi Sana. Maana Usijeshangaa Siku Nyingine Akasema Internet Na Mitandao Izimwe Yote Turudi Kwenye Sanduku La Posta
 
Nimekuwa nikifuatilia mienendo ya siasa za nchi kwa miaka mingi sasa. Nchi hii imebariki watu wenye vipawa mbalimbali.
Tasnia ya siasa imekuwa inaheshimika kwa miaka kadhaa sasa. Kipindi hiki kimeshuhudia kushuka kwa hadhi ya tasnia hii kutokana na wimbi kubwa la wanasiasa uchwara wenye kupigania zaidi matumbo yao kuliko wananchi masikini wa nchi hii.
Mmoja wa watangaza nia ndugu Mayalla ni miongoni mwao. Kiukweli nilikuwa nakuheshimu sana ila nilikuona mtu apendaye kucomplicate vitu vidogo vidogo. Nimefuatilia michango yako hasa huko Star Tv ukiishauri TCRA kufunga twitter nikajiuliza hivi hiyo ndo akili ya mtia nia atakaye kuwaletea maendeleo watu?
Wananchi wana kero nyingi ambazo TCRA wanapaswa kuzitatua kama gharama za vifurushi vya internet , tatizo la kukosekana mtandao maeneo ya vijijini n.k
Kushauri twitter ifungwe siyo suluhu la matatizo yetu. Acha unafiki na uchumia tumbo. Hufai kuwa kiongozi tafuta kazi nyingine.

Mkuu, baba wa taifa (rip) kwa watu wa namna hii aliwahi kusema, "mtu anasema anachukia rushwa, lakini ukimwangalia usoni unajiuliza. Huyu?! Kweli anachukia rushwa huyu?" Mwisho wa kumnukuu.

Kwa hii njaa kali iliyopo huku kitaa kwa sasa na athari za covid, si bure. Mwamba naye mwisho kaamua kusuka, yanini bwana? Atakuwa ameamua kuachana na kunyoa baada kugundua hawezi kutoboa. Atakuwa amejiridhisha kuwa hii njaa itammaliza akiangalia!

Mkuu, wa hivyo huku kitaa hayuko peke yake, yuko na wenzake. Wapo wengi tu, wengi wa kumwaga. Bila kusahau kuwa hata huku mitandaoni nako pia wapo!

Maajabu ya Mussa yako hivi, kufa kufaana 'ngwengwe' nayo si bado inatambaa kimugongo mugongo mkuu? Subiri kidogo, utasikia chief tayari kala, wenyewe wanaita kala 'bingo.' Yaani karamba uteuzi.

Mkuu karibu kitaa. Wenyewe wanaita akili mkichwa!

Hiiiii bagosha!
 
Kazi ipo kweli kweli jukwaa mchanyato, kaka Mayalla labda uje mwenyewe, mimi sijaelewa unabezwa, unapondwa, unaelimishwa, au mtu kaja na hoja kinzani kujibu hoja yako.!?
 
Back
Top Bottom