SoC03 Pasipo Afya hakuna Siasa

Stories of Change - 2023 Competition

Rosca Muandishi

New Member
Joined
Jul 3, 2023
Posts
1
Reaction score
1
Afya ni hali ya kujisikia vizuri ki mwili , ki akili ki roho na ki utu, bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote.

Ili mtu aendelee na shughuri zake za kila siku ni lazima awe na afya njema , hii ndio inaleta kichwa Pasipo afya hakuna siasa.

Afya ya mtu inapokuwa dhahifu inabidi apate matibabu ili kurudisha afya yake kiwa imara, moja tunajua uhusiano wa afya na tiba .

Andiko hili linazungumza kuhusu afya na tiba au matibabu, andiko hili linapendekeza mabadiliko kwenye gharama za matibabu na kufikia kuwa na matibabu bule, najua kwa urahisi kila mmoja ataona ni kitu ambacho hakiwezekani , lakini andiko hili limetoa ufafanuzi na mwanzo wa njia ya kufikia hapo kwa haraka.hata mtu awe gaidi mkubwa duniani lakini lazima atathamini afya hakuna sababu yoyote ya kujitetea ili nchi isithamini afya, watu wengi wameshapoteza maisha kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu, wengi wanaishi na kuendelea kiusambaza ugonjwa kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu, hatari zake ndio hizo na mwishowe ni kupoteza nguvu kazi na kuendelea kukuza umasikini kwa familia mpaka kwa taifa.

Gharama za matibabu ni kubwa zinapaswa kuondolewa kabisa , ukichukulia upande wako utaona ni gharama ndogo ni za kawaida hakuna mtu anashindwa ku mudu , lakini nakwambia ugonjwa ndio dharula kubwa na watu wengi wanashindwa kumudu gharama ya matibabu , nadhani kabla ya kuweka huduma yoyote kipau mbele hii ndio inatakiwa iwe ya kwanza kufanyika kiwa matibabu ni bule.

Matibabu iwe ni bule, hii itakuwa njia ya kuokoa maisha ya wengi , pia itakuwa njia ya kuzuia kusambaa kwa magonjwa , njia ya kuboresha afya , njia ya kuimarisha nguvu kazi kukuza mapato ki familia mpaka ki taifa, hii itafanya wananchi wajione kuwa wanathamani wanathaminiwa na taifa lao na watatoa ushirikiano mzuri kwa taifa kwenye mambo mbalimbali ikiwemo siasa, mfano mtu hawezi toa ushirikiano kwenye mambo ya siasa wakati ana mtu kwenye familia hajapata matibabu , au aliwahi kumpoteza mtu wa karibu kwa kushndwa kumudu gharama za matibabu , hii itapelekea aone viongozi wote hawana msaada na wananch atatuhumu hata watu wasiohusika .

Ugumu, changamoto na vikwazo matibabu bule , kuna mambo yanayochangia tuone hakuna uwezekano wa matibabu bule sababu hizo zipo nyingi ila baadhi ni kama , Kuhisi hatutojitosheleza ki fedha, ubia wa mashirika ya bima na sekta ya afya (biashara).

Wachakataji wa bajeti kwenye afya au watu wenye nafasi za juu kwenye afya wote ni watu wanaozimudu gharama za matibabu hivyo hawaoni uzito wa gharama hizo, mzaha kwenye vituo vya afya , sekta binafsi kwenye afya , hizi ni baadhi ya sababu zinazofanya tuhisi kishindwa.

Leo nikwambie kuwa hakuna kinachoshindikana chini ya jua kama nia itawekwa , mfano kama Musa aliigawa bahari, mchungaji au mfugaji wa wanyama aliweza kuwa mfalme, Tumeweza kuweka elimu bule japo mwanzo ilionekana ni kitu ambacho hakiwezekani.

Tumeweza kuondoa ukabila , Tumeweza kutunza amani kwa muda mrefu mpaka sasa, kuna nchi zilizofanya matibabu ni bule, Tulivuka kipindi cha Covid 19 kwa kitegemea jina la Mungu , nadhani kama haya yote yameweza kutokea kwenye dunia hii sidhani kama nia ya dhati ikiwekwa kwenye hili litashindikana wapo wataalamu wakukaa mezani na ku draft (kupangilia) hili na kukawa na uwiano na likafanikiwa, ni malize kwa kusema.

Itamfaidia nini mtu akapewa mali za dunia nzima na akaupoteza nafsi yake/ uhai wake .tusiogope kupoteza pesa za nchi kwa kuwekeza kwenye matibabu bule, kwani hata tusipofanya hivyo bado tutaziacha hizo pesa duniani bila kuwa na kazi yoyote, binadamu ndie alietengeneza pesa lakini tunazuia pesa kumtengeneza binadamu haiji, ......nukuu ya kukaliliwa ENDAPO TUKIFANIKIWA KUFANYA HILI ITAKUWA NCHI PENDWA YA MUNGU NA ITAKIWA YA TOFAUTI DUNIANI ITAKUWA NA KITU CHA TOFAUTI KIROHO ., , Mungu asaidia hili lionekane alainishe mioyo ya watu lipitisshwe na liwezekane, AMEN
 
Upvote 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…