Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Kwa kipindi sasa nimekuwa sionekani. ila naamini maandiko yangu mengi hupanua ufikiri wa watu wengi. napenda kujifunza na kuelimisha wengine ili ninachojua kiwafikie wengine. Nasema hili kwasababu jamii bora na nchi bora ni ile ambayo watu wake wameelimika na wanaoweza kujiongoza wao binafsi kwa kutumia akili zao. ( self government )
hakuna elimu yeyote ambayo itamuokoa na kumuondoa mtu yeyote kutoka alipo zaidi ya ya kujitambua. Kuna kitu ndani na katika roho ya binadamu. Kitu hiko ni kikubwa zaidi ya binadamu kazi yetu ni kukifunua.
Binadamu wa miaka elfu hamsini iliyopita sio binadamu wa sasa. Binadamu kwa asili yake ni kama mnyama mwingine yule. lakini kitu kinachotutofautisha wao ni uwezo wa akili yetu kukua. Ni mawazo yetu ambayo hujenga na kubomoa, kila kitu unachoona ni zao la wazo. uovu au wema ni zao la mawazo yetu. Mawazo yetu huzaa matendo.
Kwahiyo ni muhimu kuangalia jinsi tunavyofikiri kwasababu mawazo yetu ndiyo ambayo hutujenga. Akili ya binadamu hukua kadiri unavyoitumia KWAHIYO ni muhimu kuwa na mawazo yanayojenga akili yako kila wakati. Nchi yetu itajengeka pale tu tutakapokuwa na mawazo bora na kuwa tayari kuyafanyia kazi mawazo hayo. Nchi za ulaya nyingi zimekuwa sababu ya mawazo, watu walifikiri.
Kwanza ni lazima tujitambue kama taifa kwakuwa pasipo kujitambua hatutaweza kulijenga taifa hili. Taifa kama taifa lazima liwe na kiini na kiini chake ni kujitambua kwake dhidi ya mataifa mengine. Hapa ndipo litakapokuwa pasipo kujitambua huku ni vigumu taifa hili kukua.Kwahiyo ni muhimu raia wajitambue na taifa kwa ujumla lijitambue kwamba wao ni watanzania na wana malengo kama nchi na sio kama mtu mmoja mmoja pekee.
Malengo ya mtu mmoja mmoja yakiwa sambamba na malengo ya Taifa na kila mtu akijua wajibu wake ni hatua moja kubwa sana kwa taifa letu kukua. Kwahiyo ni lazima tuji organize kama taifa. Ni lazima tutambue tuna njia tunapaswa kuifuata wote kama taifa. watoto wetu na kizazi chetu kitapata faida kama tutawatengenezea njia hiyo.
Hili ni muhimu kwasababu pasipo kujitolea kwa taifa hili hatutafika popote. misingi yataifa hili itajengwa na watu wanaojitolea kuona taifa hili likisimama na kuendelea.
Ni muhimu sana kuangalia elimu tunayotoa, malezi nyumbani kwetu na kwenye mitaa yetu na jinsi gani tunachukuliana sisi kwa sisi. Msingi wa taifa lolote lile imara ni mioyo na akili za watu. kwahiyo ni muhimu tukawekeza kwa watu. Vitu vinakuja baadae baada ya kujenga misingi imara katika mioyo ya watu juu ya utaifa, uzalendo na uwajibikaji.
Kukiwa na corruption ni dalili ya uwepo wa nchi iliyo collapse. Ambayo watu wake sio wamoja. Ambayo watu wake wabinafsi na wasio na malengo ya pamoja. Hatuwezi kuendelea na kusimama kama nchi kukiwa na corruption. Nimezungumzia sana kuhusu nidhamu katika maandiko yangu mengi siwezi rudia tena. Nimezungumza sana kuhusu ethics. Kama tunataka kunyanyua juu taifa hili ni lazima tuzingatie Ethics. Hakutakuwa na Order kama taifa halina ethics. Hakuna atakaye msikiliza mwenzake kama nchi haina nidhamu na utaratibu. Viongozi hawatasikilizwa kama hawatokuwa na nidhamu na maadili na kuonyesha mfano kwa wanaowatawala.
Tuna tatizo katika Taifa na mtu yeyote mwenye akili hawezi bisha. mifumo yetu mingi imekufa. tunahitaji kulihuisha upya taifa hili. ili watu wetu walitumikie upya taifa hili. Ni wakati sasa kujaribu angalau kwa kizazi hiki kutafuta njia ya kutoka kwa taifa hili. And for this Generation it will be our '' Greatest attempt''
Hatutaweza kama hatutatumia nguvu zetu zote kujaribu, kama hatutatumia akili zetu zote kujaribu na tutakapoendelea kujaribu; ninaamini ndani ya kiza kinene macho yetu yataanza kuona jua taratibu kama linavyochomoza kutoka angani na kuonekana dhahiri machoni kwetu. Na lile wazo la taifa letu kukua na kuwa kubwa litakuwa dhahiri. Without perseverence, without faith. Hatuwezi kufanikiwa kama taifa. Uzalendo ni muhimu sana. Ni muhimu kuwaweka watu wetu pamoja. Lakini hii yote inahitaji uongozi pasipo uongozi bora hatutaendelea.