wakuu nina passo 1kr piston 3 mwaka wa 2 na nusu naitumia... na safari zangu ni hapahapa town ila nimegundua kwamba inakula lita 1 kwa km 9 ... nadhani kwa passo labda inakula km 15 kwa lita ila naona hii yangu sio kama passo nyengine... ni fundi gani niende ili ipate kuwa vzuri
imetembea km 69854 mpaka sasa..
Hutu tugari tudogo twenye engine ya Cc chini ya 1000 huwa ni changamoto sana.
Mimi nimetumia Passo ila niliexpirience the same thing as u. Nikaona nikafanyie service kwa kubadili plugs zote, air filter, oil, tairi, brake pads.
Ila nikafanikiwa kuongeza milage kidogo sana ya wastani kutoka 10km per 1litre hadi 12.5 km hadi 13 km per litre.
Nikaja kufanya utafiti zaidi nikagundua hivi vipaso havina nguvu. Na kwakutokuwa na nguvu ya engine muda wote engine inakuwa na mzigo hivyo consumption ya mafuta kiwastani inapanda.
Niligundugua hii nikachukua IST ya mshikaji wangu nilitumia wiki na ni Cc 1400 ila nitumia vizuri sana na ilinipa milage kubwa sana ya 15km hadi 16km per litre na hapo haijafanyiwa service.
Ile passo kuna muda nikibeba watu yaani mtu mbele na wawili nyuma. Ule muinuko wa tegeta kuja njia panda ya kawe ukiwa unaingia lugalo ilikuwa inanilazimu kuzima AC ili gari iwe na nguvu ya kupanda kwa urahisi maana unaisikia inaweweseka kabisa na kuelemewa mzigo. Engine haina nguvu kabisa.
Ila ile IST nilikuwa napita sehemu za muinuko na AC inawaka ila gari ina nguvu balaa.
Sasa ndipo nikajua kuwa sometimes hutu tugari tudogo hatuna fuel economy ile tunataka kwasababu hata nguvu ya kueconomize havina.