Passo inakula lita 1 kwa km 9

Passo inakula lita 1 kwa km 9

Fuqin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2018
Posts
306
Reaction score
625
Wakuu nina passo 1kr piston 3 mwaka wa 2 na nusu naitumia na safari zangu ni hapahapa town ila nimegundua kwamba inakula lita 1 kwa km 9. Nadhani kwa passo labda inakula km 15 kwa lita ila naona hii yangu sio kama passo nyengine ni fundi gani niende ili ipate kuwa vizuri
imetembea km 69854 mpaka sasa..
 
1. Mwaka wa 2 na Nusu uliinunua kwa nani? Ilikuja na kilometere ngapi?

2. Services gani umewahi kufanya kubwa hivi karibuni? Oil, Filter ya oil na air, plugs na coil?

3. Mizigo, tyre pressure na uendeshaji wako upoje? Na unaendesha sana town au?
 
wakuu nina passo 1kr piston 3 mwaka wa 2 na nusu naitumia... na safari zangu ni hapahapa town ila nimegundua kwamba inakula lita 1 kwa km 9 ... nadhani kwa passo labda inakula km 15 kwa lita ila naona hii yangu sio kama passo nyengine... ni fundi gani niende ili ipate kuwa vzuri
imetembea km 69854 mpaka sasa..
Hiyo sio passo tena naona imekuwa gari kubwa labda inaongezeka jinsi miaka inavyokwenda...huu tunaita ukuaji kisayansi😄😄.
So ibadili jina kutoka passo na iwe fusso
 
Mimi nimemiliki Paso Kadhaa na magari kadhaa ya Engine ndogo

Haya ndo Mawazo Yangu

1. Passo speed ndogno + AC inakula mafuta kama kawa tena kwa kuwa ni engine ndogo inakula zaidi na inakosa nguvu

2. Kufa kwa engine ndogo ni kuisha nguvu, engine < 1000 cc ukiona hata ufanye nini nguvu haiongezeki ujue ndio ishaanza kufa (hata siku moja hazikubali overhaul)

3. Ulaji wa mafuta pia ni accesories tunazoadd, yangu ilikuwa inakula 20km/l tire size 13R kwa safari na 14km/l mjini, nkaona ipo chini nkaweka tairi 14R , mafuta ikawa ulaji ni 14km/l kwa safari na 10km/l kwa mjini so accesories zinaongeza mzigo sanah kwa engine ndogo

4. Mengine nikikumbuka ntasema..
 
1. Mwaka wa 2 na Nusu uliinunua kwa nani? Ilikuja na kilometere ngapi?

2. Services gani umewahi kufanya kubwa hivi karibuni? Oil, Filter ya oil na air, plugs na coil?

3. Mizigo, tyre pressure na uendeshaji wako upoje? Na unaendesha sana town au?
mkuu unaposema service kubwa, unabadilisha nini na nini mkuu?
 
wakuu nina passo 1kr piston 3 mwaka wa 2 na nusu naitumia... na safari zangu ni hapahapa town ila nimegundua kwamba inakula lita 1 kwa km 9 ... nadhani kwa passo labda inakula km 15 kwa lita ila naona hii yangu sio kama passo nyengine... ni fundi gani niende ili ipate kuwa vzuri
imetembea km 69854 mpaka sasa..
Cheki koil na nozzle plug pia badilisha. Nna passo yangu kama yako nikiweka full tank naenda 500km kama ni highway. Huwa naenda nayo safari kubwakubwa mwanza dar maranyingi tu
 
Cheki koil na nozzle plug pia badilisha. Nna passo yangu kama yako nikiweka full tank naenda 500km kama ni highway. Huwa naenda nayo safari kubwakubwa mwanza dar maranyingi tu
Nimemuuliza fundi kuhusu nozzle kasema 1 inauzwa 20000 na si lazima kununua mpya anaweza kizibana zikawa fresh na hiyo coil kaniambia inauzwa 140000...
 
nimemuuliza fundi kuhusu nozzle kasema 1 inauzwa 20000 na sii lazima kununua mpya anaweza kizibana zikawa fresh na hiyo coil kaniambia inauzwa 140000...
Mimi huwa sipendi ufundi anaokufanyia fundi wako nozzle za gari ndogo ukianza kuzirepair ndo hivo zinamwaga tu mafuta so its your choice ila mm nashauri nunua coil zote mpya, nozzle zote mpya ,plug zote mpya zile za sindano
Ila kama mfuko sio mzuri mwambie akutestie nozzle ambazo bado nzima uendelee kuzitumia, coil pia afanye hivo.
Adui mkubwa kwa gari za petrol hizi ndogo ni miss
 
Hapopana pasua kichwa kama asizidi 120km/h mbona kwenye specs zake hatuoni limitation ya speed zaidi ya kuandika highways km20/h na mjini 14/h?!
Ni uamuzi wako mkuu ila engine ya passo ni ndogo sana so ukiamia kitiririka usijekuta piston zinachomoka
 
Mimi huwa sipendi ufundi anaokufanyia fundi wako nozzle za gari ndogo ukianza kuzirepair ndo hivo zinamwaga tu mafuta so its your choice ila mm nashauri nunua coil zote mpya, nozzle zote mpya ,plug zote mpya zile za sindano
Ila kama mfuko sio mzuri mwambie akutestie nozzle ambazo bado nzima uendelee kuzitumia, coil pia afanye hivo.
Adui mkubwa kwa gari za petrol hizi ndogo ni miss
Mfuko sio mzuri bora zifanyiwe service baada ya mwezi kama bado nitanunua mpya
 
Mimi huwa sipendi ufundi anaokufanyia fundi wako nozzle za gari ndogo ukianza kuzirepair ndo hivo zinamwaga tu mafuta so its your choice ila mm nashauri nunua coil zote mpya, nozzle zote mpya ,plug zote mpya zile za sindano
Ila kama mfuko sio mzuri mwambie akutestie nozzle ambazo bado nzima uendelee kuzitumia, coil pia afanye hivo.
Adui mkubwa kwa gari za petrol hizi ndogo ni miss
Mambo vipi blaza kaka.
Nimekua nakufatilia sana maana namie nina Passo cc1290 piston 4.

Nahisi ulaji wake wa mafuta sio mzuri kama mwanzo.

Hivi hizo equipment ulizotaja kuweka zote mpya inaweza kunicost kufika bei gani nijiandae kisaikolojia?

Halafu umesema recommended engine Oil ni gani vile? ili niwe nayo akilini next service.
 
wakuu nina passo 1kr piston 3 mwaka wa 2 na nusu naitumia... na safari zangu ni hapahapa town ila nimegundua kwamba inakula lita 1 kwa km 9 ... nadhani kwa passo labda inakula km 15 kwa lita ila naona hii yangu sio kama passo nyengine... ni fundi gani niende ili ipate kuwa vzuri
imetembea km 69854 mpaka sasa..
Hutu tugari tudogo twenye engine ya Cc chini ya 1000 huwa ni changamoto sana.

Mimi nimetumia Passo ila niliexpirience the same thing as u. Nikaona nikafanyie service kwa kubadili plugs zote, air filter, oil, tairi, brake pads.

Ila nikafanikiwa kuongeza milage kidogo sana ya wastani kutoka 10km per 1litre hadi 12.5 km hadi 13 km per litre.

Nikaja kufanya utafiti zaidi nikagundua hivi vipaso havina nguvu. Na kwakutokuwa na nguvu ya engine muda wote engine inakuwa na mzigo hivyo consumption ya mafuta kiwastani inapanda.

Niligundugua hii nikachukua IST ya mshikaji wangu nilitumia wiki na ni Cc 1400 ila nitumia vizuri sana na ilinipa milage kubwa sana ya 15km hadi 16km per litre na hapo haijafanyiwa service.

Ile passo kuna muda nikibeba watu yaani mtu mbele na wawili nyuma. Ule muinuko wa tegeta kuja njia panda ya kawe ukiwa unaingia lugalo ilikuwa inanilazimu kuzima AC ili gari iwe na nguvu ya kupanda kwa urahisi maana unaisikia inaweweseka kabisa na kuelemewa mzigo. Engine haina nguvu kabisa.

Ila ile IST nilikuwa napita sehemu za muinuko na AC inawaka ila gari ina nguvu balaa.

Sasa ndipo nikajua kuwa sometimes hutu tugari tudogo hatuna fuel economy ile tunataka kwasababu hata nguvu ya kueconomize havina.
 
Back
Top Bottom