Kuna mijadala mingi inayosema kuwa Passport yetu ya Tanzania haikubaliki kama proof of ID je ni kweli?
- Tunachokijua
- Katika kutafuta ukweli wa jambo hili, JamiiForums imefanya mawasiliano na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle ambaye amesema;
Passport siyo Kitambulisho, ni hati ya safari anayopewa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya kusafiri nje ya nchi. Pia, ni utambulisho wake akiwa nje ya nchi kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vitambulisho vipo vya aina nyingi na tofauti, kuna kitambulisho cha Utaifa, kitambulisho cha Mpiga Kura n.k, huwezi kufananisha passport na kitambulisho kwa sababu vitambulisho vipo vya aina tofauti tofauti.
Aidha, passport kwa madhumuni yake haitolewi kama Kitambulisho, lakini katika matumizi yake inaweza kutumika kama Kitambulisho.
Passport ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria ya passport hutolewa kwa dhumuni la safari, haitolewi kwa matumizi kama ya kitambulisho kwa Mtanzania. Akiwa hapa nchini, Mtanzania anaomba passport kwa ajili ya safari.
Kama atataka Kitambulisho akiwa hapa nchini basi akachukue kitambulisho cha NIDA au cha kazi, hizi ndivyo vitamtambulisha.
Mselle amemaliza kwa kusema dhana ya Kitambulisho ni pana sana, pia dhana ya passport ni pana sana, lakini zinaweza kutumika kwa kubadilishana pale inapobidi.