KWELI Passport ya Tanzania haikubaliki kutumika kama Kitambulisho cha taifa (National ID)

KWELI Passport ya Tanzania haikubaliki kutumika kama Kitambulisho cha taifa (National ID)

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kuna mijadala mingi inayosema kuwa Passport yetu ya Tanzania haikubaliki kama proof of ID je ni kweli?

E26997EE-FB64-4652-AE81-B7C7766DFD75.jpeg
 
Tunachokijua
Katika kutafuta ukweli wa jambo hili, JamiiForums imefanya mawasiliano na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Mrakibu wa Uhamiaji, Paul John Mselle ambaye amesema;

Passport siyo Kitambulisho, ni hati ya safari anayopewa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa madhumuni ya kusafiri nje ya nchi. Pia, ni utambulisho wake akiwa nje ya nchi kuwa ni raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vitambulisho vipo vya aina nyingi na tofauti, kuna kitambulisho cha Utaifa, kitambulisho cha Mpiga Kura n.k, huwezi kufananisha passport na kitambulisho kwa sababu vitambulisho vipo vya aina tofauti tofauti.

Aidha, passport kwa madhumuni yake haitolewi kama Kitambulisho, lakini katika matumizi yake inaweza kutumika kama Kitambulisho.

Passport ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria ya passport hutolewa kwa dhumuni la safari, haitolewi kwa matumizi kama ya kitambulisho kwa Mtanzania. Akiwa hapa nchini, Mtanzania anaomba passport kwa ajili ya safari.

Kama atataka Kitambulisho akiwa hapa nchini basi akachukue kitambulisho cha NIDA au cha kazi, hizi ndivyo vitamtambulisha.

Mselle amemaliza kwa kusema dhana ya Kitambulisho ni pana sana, pia dhana ya passport ni pana sana, lakini zinaweza kutumika kwa kubadilishana pale inapobidi.
Kitambulisho cha nida hata wasio raia wanapewa ili mradi tu awe na residence permit ya class yeyote ile,
Naungana na msemaji wa uhamiaji kwamba hii ni dhana pana sana
So twende taratiiibu chuki zinabomoa tu
Kwani mtoto mchanga hana utaifa? Utaifa ni wa yeyote aliyezaliwa na wananchi wa taifa fulani. Kuna miitu mizima kama migabacholi inayovyo vitambulisho vya kitaifa wakati si watanzania.
 
Mbona magabacholi na wasomali hata wakenya wanazo? Sisi ni watu wa hovyo tusiojithamini na kuthaminiana mbali na utaifa wetu. Tungekuwa tunajitambua, hawa magabacholi wasingetokea kuwa matajiri wakati wakitubagua na kutudharau kama kuku.
Duuuh!!, umetoka nje ya mada mkuu
 
Wewe usiwe rofa.Namba ninayo ila kitambulisho sina kila nikienda kuchukua naambiwa niwe na sms kutoka kwao au niwe nimepigiwa?

Issue hapa muhusika wa juu awajibishwe aletwe mwingine huyo atakuwa makini na kazi yake.



Kabla nguvu nyingi ni kugonga glass tu na kujipongeza
Tutawalaumu sana NIDA, lakini ukifikria kwa undani na sakata liliowakuta kuhusu vitambulisho hivi, kwa upande mwingie utawahurumia tu. NIDA anategemea 100% ruzuku ya serikali, hana vyanzo vyake vya mapato. Seriali akimpa pesa NIDA ili achape vitambulisho vya raia wote sidhani kama NIDA atazungukazunguka. hapa wa Kumshona kiroho mbaya ni Serikali wala sio NIDA
 
Sasa kama Passport sio kitambulisho mbona kwenye madaftari ya kujisajili kwenye hoteli unapokuwa ugenini hapa hapa Tanzania huwa wanauliza namba ya passport?
 
Back
Top Bottom