Pata elimu kidogo kuhusu makato CRDB

Acha uongo we jamaa...

kuangalia salio/mini-statement kupitia CRDB App hakunaga makato siku zote.
 
Mie baada ya kuona nakatwa nikawa nimeacha kuona salio. Nadhani mara ya mwisho kucheki salio ilikuwa mwaka jana sikumbuki vizuri ilikuwa mwezi upi. Mie ni mteja wao huu mwaka wa 11.
Cheki ulivoanza kubadili gia angani.
Kama hujui kitu uliza kwanza.

CRDB App haijawahi kuwa na makato upande wa kuangalia salio. Hata kucheki mini-statement ya mwezi mzima ni bure!
 
Kwanini unakua liongo hivi?
 
Acha uongo we jamaa...

kuangalia salio/mini-statement kupitia CRDB App hakunaga makato siku zote.
Mkuu sipo hapa kubisha wala kujifanya mjuaji. Siyo utamaduni wangu huu. Naomba tu tuendelee kufahamishana vizuri.

Hiyo jana wadau waliposema kuangalia salio ni bure ilibidi nifanye hivyo. Niliangalia salio kama mara 5 hivi kupata confirmation. Wakati naangalia salio kwenye hiyo account nilikuwa na balance ya Tsh 3449.12. Wakati huo sikukatwa na salio likabaki lilivyo. Baada ya saa kama 5 hivi baadae nikacheki tena na nikakuta salio langu ni zero.

Wakati huu ulipotoa jibu lako hili, nikaangalia tena nikakuta nina negative balance ya (Tsh -438.89). Nikawa nimejaribu kuomba statement ya mwezi mzima na naambiwa kuwa nina insufficient balance na hivyo siwezi kupata statement.

Sipo hapa kupika maneno wala kuleta ubishi usio na tija maana siyo utamaduni wangu.

1. Mkuu, with all due respect, nakuomba uelezee ni nini tafsiri ya maelezo hayo niliyotoa.
2. Je, hizo taarifa za kuwa ukiangalia salio kupitia App ni bure ulizipata wapi, ni ofsin kwao ama huwa unaangalia tu nakuondoka. Kisha hufanyi ku-trace tena account yako?

My take: Nadhani wewe na wadau wengine mnaosema hizo huduma ni bure (kuangalia salio na kuomba statement, achana na zile automatic statements za kila mwezi) huenda mtakuwa na akiba ya kutosha kwenye account zenu hivyo kikikatwa hicho kiasi kidogo mnadhani hakuna impact yoyote.

Kama siyo sahihi nachodhani, basi huenda kuna namna account yangu haipo sawa, na natakiwa kufuatilia, maana nakosa hizo huduma ili ziwe bure kama walivyo watu wengine.

Ahsante.

NB: Siwezi ku-screen shot hapa account yangu, ningeambatanisha na ushahidi.
 
waongo wanadai ukifungua account ya nmb bonuce account free sio kweli upande wa ATM Card wanataka makatoo
 
Tena kama Hawa NMB ndiyo wezi sana, wanakwambia kadi ya Chap chap Haina makato Kumbe ni wizi mtupu ukitumia ndani ya miezi mitatu tuu wanaanza kulima kama kawaida.
 
Internet banking kuwa bure it means uwe na application ya benki husika in your phone. Then hakikisha una bundle, fungua hyo app e.g NMB mkononi app, alaf angalia salio lako
Hqpana internet banking ile ya kwee app,
Unatumia http websites kuingia kwenye akaunt yako, kwa hiyo unaweza kuipata kwenye simu au computer or anything that can access interet
 
Uzi kabambe
 
kitu ambacho sijaelewa, kwa balance ya kama 20m wamekata karibia 165,000 kama monthly charges. si bora kuweka nyumbani tu, au nimeibiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…