Pata simu za kisasa(smartphone) mpya kabisa kwa BEI POA kutoka UK

Pata simu za kisasa(smartphone) mpya kabisa kwa BEI POA kutoka UK

Kuhusu kufungwa kwa simu sio kwamba ni ya wiz. Bali inakuwa locked kutumika kwa mtandao mmoja
 
Samahani kama nitakuwa nimekosea ila simu kama mpaka zimefungwa zitakuwa za wizi, utanunuaje simu ipo locked. Mm na nunua sana simu toka nje ila kabla sijanunua na angalia kama ipo locked.

Mkuu usiongee usichokijua Utachekwa! Kuna simu kuwa locked na Blocked , Locked ni simu za mtandao fulani, tuseme tigo wanakupa simu na dakika lkn hzo zinakuwa zinatumika na line ya mtandao huo tu na unakuwa unalipa kwa bili kila mwezi, mfano tigo wanakupa simu zao unakuwa unatumia kwa line ya mtandao wa tigo tu ukitaka kutumia line ya mtandao mwingine kama voda ndio inabidi uzifungue, BLOCKED ni zile simu ambazo mtu amepoteza akairiport ktk mtandao husika aliokuwa anautumia wanazifunga au simu za wizi na simu zikiwa blocked zinaweza zisitumike ktk nchi husika ambazo zimekuwa blocked nyingine hazitumiki dunia nzima zikiwa blocked na pia ikiwa blocked inaweza tumika nchi nyingine lkn ukirudi nchi ambayo iko blocked aifanyi kazi...Sasa hizo ninazouza zilikiwa Locked sio Blocked na hata ukirudi nayo ktk nchi husika bado ianfanya kazi....
 
Hii ni tamaa, kwani umekatazwa kufungua thread yako? Au labda haujui kutangaza biashara unaingilia ya watu. Na hizo bei zilivyo ndogo lazima kuna kitu hapo. Inabidi ujieleze zaidi kwa thread yako weye.

Sentensi yako ya mwisho...(weye) inaonekana ww ndio walewale ndugu zetu chakochako changu chako basi na ww kafungue jamii forums yako kwenu Yakheee si hamtutaki....Biashara ushindani hatiiii.....
 
Mamakibunju Simu zwko ulifungulia wap. Maana ninayo bb q5 imefungwa

Pia kisutu karibu na chef pride kuna mhindi anafungua simu aina zote, nenda maeneo yale waulizr wauzaji simu au kwenye maduka ya simu watakuelekeza maana hapa nikuelekeza nitakupoteza...
 
Huyu jamaa ni mwizi anakuja kuuza simu za wizi humu tumekustukia labda ukauze ubungo stendi ya mkoa humu tumestuka
 
Ok. Umeeleweka. Ya kwangu iko locked to specifi sm card


Wanafungua hizo hapo karibu na chefprie na kariakoo pia uliza mafundi cm wengine! Anyway ni aina gani ya cm na inatumia cm gani? Yaani imefungwa ktk mtandao gani?
 
Mamakibunju sijapenda tabia yako kuingilia tangazo langu na kuweka lako kwenye coments. Mpaka sasa tunachanganyana na kuaribiana biashara. Kama una account unashindwa nn kuanzisha post ya kwako!?
 
Blessings. Mwiz akiiba simu ya laki tano atakuuzia kwa laki moja au hata elfu themanini. Humu ndani hamna simu ya namna hiyo. Kama kweli umekuwa interested unaweza kununua au kuchangia positively sio kushutumu kuita biashara za watu ni za wizi
 
Me Ninayo blackberry Z10 kwa 450,000 , Samsunga Galaxy S3 Mini 380,00, Lumia 610 300,000 , Galaxy S4 mini 550,000 na Iphone 5 500,000(iphone ilikuwa na water damage lkn imetengenezwa na apple shop uk inafanya kazi kama mpya)....SIMU ZOTE ZILIKUWA LOCKED NA UK NETWORKN LKN ZIMEFUNGULIWA INGAWA LOGO YA NETWORK BADO IPO
mbona unavamia tangazo la mjasiriamali mwenzako?~!
 
Mamakibunju sijapenda tabia yako kuingilia tangazo langu na kuweka lako kwenye coments. Mpaka sasa tunachanganyana na kuaribiana biashara. Kama una account unashindwa nn kuanzisha post ya kwako!?


Umelipia kiasi gani kwa hilo Tangazo lako, Ni Report kwa MD anipige Ban
Roho mbaya kama wahindi wa iMTU
 
Umelipia kiasi gani kwa hilo Tangazo lako, Ni Report kwa MD anipige Ban
Roho mbaya kama wahindi wa iMTU

Mama, tatizo siyo kalipa kiasi gani,ni ustaarabu tu, mtu kafungua thread anajaribu kutafuta chochote kitu si ustaarabu unakuja kupandia juu na wewe unauza bidhaa zilezile! Pendaneni jamani, mbona kufungua thread ni rahisi na ni bure!
 
Wabongo bhana. Unaleta ubabe wakati unajua umekosea. Hata kama cjalipia, hata wew usingelipia. Katika hali ya kawaida ulipaswa kuomba samahan sio kuwa mbabe@ mamakibunju
 
Mama, tatizo siyo kalipa kiasi gani,ni ustaarabu tu, mtu kafungua thread anajaribu kutafuta chochote kitu si ustaarabu unakuja kupandia juu na wewe unauza bidhaa zilezile! Pendaneni jamani, mbona kufungua thread ni rahisi na ni bure!

Ebu angalia thread ngapi me nimeshaweka za kuuza vitu na watu wameweka matangazo yao na wanauza vitu vyao na bei ndogo kuliko niliyoweka mimi! Nyie ndio mnaoshinda kwa waganga kuroga .....Sifungui Thread yangu na ukifungua nyingine naweka tangazo pia...#DealwithiT
 
We mgeni Jamii Forum! Check thread zangu zilizopita wangapi wameweka matangazo yao? Kama auna cha kuchangia Chapa Lapa...

Tatizo siyo ugeni au uwenyeji, tatizo ni ustaarabu!
Picture1.png
 
Back
Top Bottom