Pata ushauri, michango na mawazo ya ufugaji wa bata wa kienyeji kibiashara

Asante sana mkuu kwa maelezo mazuri,, vip kuhusu aina ya mbegu kama alivyochangia mheshimiwa mmoja hapo juu kwamba , rangi nyeupe ni nzuri kulingana na soko, kwa upande wako unasemeaj kuhusu hilo,

Pia katika ufugaji huu ninaoenda kuuanza , unaweza kukadiria idadi ya chini ya kuanza nayo isipungue kiasi gani ili lengo la kufuga kibiashara liweze kutimia

Nashukuru sana kwa ushauri…!!
 
mkuu kama ni hao bukini hebu pitia hapa ujisomee jinsi ya kuwafugaKILIMO BORA: UFUGAJI BORA WA BATA BUKINI
 
Hapana mkuu,, mimi nahitaji hawa wa kienyeji
ok kama ni hawa wa kawaida huwa awana shida ni wewe tu utaangalia unakiasi gani na utaangalia uanze na wangapi maana uwiano wao dume moja linapanda majike manne hadi sita cha kwanza inatakiwa uwandae mazingira ya watakapo ishi huwa inapendeza kama utawatengenezea fensi kwenye sehemu yao ya kupumzika jioni ndio wanaingia bandani,jiandae pia kuwalisha vizuri na maji wapate ya kutosha
ANGALIZO:hao bata ukiwatunza kiusafi wanakuwa wasafi kweli mfano huu
ukiwatunza kiuchafu wanakuwa wachafu kweli hadi wanakuwa hawapendezi mfano huu
 
Sijajua kipi kimekufanya uache kuku navyoona Bata ni wazuri hawana nagonjwa mengi na gharama kubwa ni pumba na maji tu Lkn sijaona Soko kama la kuku, unaweza kimbilia Bata na ukawapata Lkn Fanya utafiti kabla kwa wanaofuga ili ujue soko lilivyo binafsi Naona kuku wowote wale wana soko kubwa na la hakika
 
Ahsante kwa maneno mazuri ila inakuwa vyema kutiana moyo, sio kutishiana.
Siyo kama anatisha, anasema uhalisia, ni vizuri kuambiwa ukweli ukajua hali halisi na namna ya kupambana kuliko kutiwa moyo kufanya jambo usilolijua ugumu wake. Bora kujua ukweli kuliko kudanganywa ukafanya, ukija kushindwa utakata tamaa kabisa!
 
Kwa bata huko nimeonja mafanikio, muda si mrefu nitawakaribisha wadau walioko Mwanza tukale bata sehemu nitakayowatangazia.
Mkuu kama hutojali naomba unipatie mawasiliano yako nikutafte ,, coz mimi pia nimeanza ufugaji huu wa bata but sijapata details za kutosha kuhusu huu ufugaji, so kam hutjali naomba unisaidie kupata mawasiliano yako kwa ushauri zAidi,, niko Mwanza pia
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…