Pata ushauri wa biashara - Business Consulting

Biashara2000

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2013
Posts
649
Reaction score
547
Habari zenu.

Nimekuwa nikipata maombi mbalimbali ya ushauri wa mambo ya biashara kutokana na posts zangu ambazo nimekuwa nikiweka humu JF. Na ambayo ilisababisha meseji nyingi zaidi ni ile post ya kuhusu mafunzo ya utengenezaji wa mkaa.

Maombi mengi yamekuwa ni simu ambazo zinahusu biashara na ujasiriamali kwa ujumla. Watu wengi huko nje wanapatwa na changamoto mbalimbali katika biashara zao. Nimeona kwa kuwa mimi naendesha biashara kwa sasa nione umuhimu wa ku share uzoeufu wangu wa kibiashara na watu watakaohitaji ili nao uwasaidie kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika biashara zao. Mimi sio tajiri ila ninauzoefu wa biashara kwa zaidi ya mwaka na nusu na nimepambana na changamoto nyingi sana wakati naanzisha na kuendesha biashara yangu na ushauri naotoa sio theory bali ni actual uzoefu wangu wa kufanya biashara. Mimi naendesha biashara ya kutengeneza na kuuza mkaa mjini Kibaha.

Ushauri ninaotoa ni katika sehemu zifuatazo:

1. Jinsi ya kuendesha biashara kwa mafanikio
2. Jinsi ya kupambana na changamoto za ujasiriamali na biashara
3. Ushauri utakaokusaidia kutoka kuwa mjasiriamali hadi mfanyabiashara
4. Jinsi ya kuongeza mauzo katika biashara yako
5. Mambo ya management kwa ujumla
6. Na kadhalika

Ushauri unaohusu mambo ya kisheria sitoi kwa kuwa mimi sio mwanasheria. Unaweza tafuta mwanasheria akusaidie katika hilo.

Ushauri huu nautoa kwa njia ya simu. Unanitumia ada ya ushauri ya shilingi 5,000 tu kwa M-PESA kwenye 0758 308193 halafu unanipigia tunaongea mpaka tatizo lako lipate ushauri wa kupata suluhisho. Watakaopenda kuchukua nafasi hii kuondoa matatizo katika biashara zao mnakaribishwa. Kama unapatwa na tatizo la kibiashara hata Bill Gates alisema inabidi uombe usaidiwe. Watoa ushauri wa ujasiriamali hapa mjini wanatoa ushauri based on theory tu. Mimi natoa based on experience. Wajasiriamali wengi nchini wanabaki tu kuwa wajasiriamali na si wafanyabiashara kwa kuwa wanachukua ushauri na mafunzo kutoka kwa walimu wa ujasiriamali wanaotoa tips kutoka kwenye internet na kuwamezesha. Matokeo yake wamama wa watu wanabaki kuwa pale pale katika maisha hawasongi mbele.

0758 308193

Karibuni.
 

Huoni kwamba hiyo bei yako ni ndogo kuliko wale wataalamu wa biashara walioko kule posta mpya ambao wana charge 100,000 kwa dk kadhaa tu za ushauri? Kwa 5,000 ni ndogo jaribu kupandisha
 
Acheni utapeli.

Kuna jamaa namfahamu, alianzisha baa kwa mtaji mkubwa wa mkopo.

Baa haikudumu kwa miezi sita. Akafilisika.

Ataishije mjini? Akaanzisha kampuni ya kutoa ushauri wa kibiashara!

Nikajiuliza, yeye baa ilimshinda, ni kipi atakachoshauri kwa wengine?
 

Mimi hunifahamu kwa hiyo usi judge.

Ondoa hiyo attitude ya uoga, sio nzuri kwa maisha yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…