Tuliumizwa sana na enzi za 'zidumu fikra za nanihii' nashukuru sana kuwa sasa WaTZ tunachanganua mambo. Safi sana.
Msisitizo wangu nauongeza katika kutenganisha 'usajili jina', 'hosting' na website designing. Na nimependa kila mtu ameona kwa namna yake, nasi tuliona kwa namna yetu. Ni wakati sasa kuchanganya maoni ya pande yote na kuweka mantiki. Hii ndio maana haswa ya kuthamini wanaokuzunguka.
Kwa kuwa bei ya kutengeneza tovuti ndio ishu, na haswa kwamba wengi hushindwa Tukaona tufanye bure. Hosting na domain registration hatujaweza kufanya bure, japo wataalamu hapa wanaamini zikiwa tovuti kama mia zote zinalipa hosting, kuna fursa kubwa sana kurudusha hosting chini kwa 50%. Tunapishana namna tunavyoona, huu ni upeo wetu wa kuona. Huwezi kushusha bei ukiwa na watu wanne, tunahitaji wengi ili tununue unlimited package kisha turudishe bei. Napenda michango yenu na nazidi kusubiri maoni zaidi, yaani km kuna mtu anajua tunapoweza kufanya nafuu zaidi asisite kuniambia. Pia anayewaka bei kali asiishie hapo, atupe mbadala. Na mwisho, kituko kwa wengi labda, ni kwamba km wewe ni website designer na upo tayari KUJITOLEA KUTENGENEZEA WATU WEBSITE BURE, karibu sana ktk project yetu. Pamoja tunaweza.