Patasi ya Diamond Platinumz yatoboa tobo Marekani

Maboso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
5,164
Reaction score
5,762
Tukiwa tunasubiria kwa hamu kubwa ile collabo bora ya kimataifa kati ya Diamond Platinumz na Neyo, mtoto wa Alicia Keys akiwa ndani ya gari la baba yake ameshindwa kuvumilia na kujikuta akisankoroka vilivyo. Baba yake bila kusita ikabidi arushe kwenye mtandao maarufu kabisa wa instagram ili kuionyesha dunia namna gani Nana ilivyompa homa mwanae.

Hizi dalili njema kwamba mziki wetu umeshatoboa tobo USA kiasi kwamba producer maarufu kama huyu mume wa Alicia Keys anasikiliza muziki wetu tena ndani ya gari yake mwenyewe. Rai yangu kwa wasanii wa Tanzania ni kuwa acheni chuki na wivu wa kijinga kwa Diamond, bali angalieni kafanyaje hadi kaweza kufanikiwa kiasi hicho ili nanyi muweze kufikia kiwango hicho na pengine kuzidi. Tunapofanikiwa si sifa kwenu binafsi bali ni sifa kwa taifa nzima.

Hongera sana Diamond na uongozi mzima wa Wasafi kwa kazi nzuri mnayoifanya.

Post ya mume wake na Alicia Keys huko instagram



Post ya Diamond Platinumz kuhusu collabo yake na Neyo

Attachment ya tatu ni video ya mtoto wa Alicia Keys akisankoroka.

.......................................................................
UPDATES>>

Baada mashabiki wa Diamond Platinumz kuvamia post ya Swiz Beats ikimuonesha binti yake anavyosankoroka na Nana fever, jamaa kapost clip nyingine ikionesha binti yake akimfundisha namna ya kucheza wimbo wa Nataka kulewa wa Diamond Platinumz. Bonyeza hapa kupakua clip hiyo.


View attachment therealswizzz.aviView attachment therealswizzz-natakakulewa.avi
 

Attachments

  • nataka_kulewa_therealswiz_vibes.jpg
    33.7 KB · Views: 5,763
  • diamond_ft_neyo.jpg
    64.8 KB · Views: 1,426
  • therealswiz_vibes.jpg
    42.5 KB · Views: 5,751
Mi kwa mapenzi maskini
nikamvisha na pete kwa kumuoa
kukata vilimi limi vya wazushi
wanafiki wanaomponda
kumbe mwenzangu na mimi
ni bure tu unajisumbua
si tuko kama ishirini
mabuzi ving'asti wengine anawahonga
oh mapenzi, [mapenzi] yalinifanya kama mtoto nilie vibaya
mie siwezi, walionikuta waniache nisemee jina
oh mapenzi, [mapenzi] yalinifanya kama mtoto nilie vibaya
na nina mengi, ah yamenijaa moyoni

oyooooooooo mtag swiz basiii aje achukue mistari hii kidogo, chibu anawaimbisha kiswahili HIO NDIO MAANA YA ICON, na hapo mastaa wengi wanacheza huku wamejifungia chumbani na madem zao hahahahaha, sema tu ubishi hawataki kupost




TEAM DIAMOND PLATNUMZ FOREVER

PROUDLY WCB

TOROKA UJEEEE cute b
 
Ni nadra sana mnyamwezi swizz bitz kumkubali mtu.. Kwa hili salute nyingi kwako diamond, upo mbali sana we mtu.
 
Ha ha ha... Kidingi wew ni mnafik ujue kwa nini? Umeniita kinafiki... eti matokeo ya yanga ni ngapi ngapi...

NIMESEMA HIVII BANDO LANGU NA YA KWAMBA UNAFKI SITAKI. Hivi hamuelewi mtu akisema amejitoa kwenye hayo mambo ya kimbea? Kila mtu na maamuzi yake.. SASA KWA TAARIFA YENU SIJASOMA WALA SIWEZI SOMA UPUUZI ULIONIITA NIUONE.

#CHAGUA
#LOWASA..
#TEAM #MABADILIKO.
 
Good news Hizi habari zimfikie Davido! Yule jamaa alivyo na wivu
 
Nafurahia sana moyoni mtz mwenzangu anapopiga hatua kama hii. Diamond forever. I just voted for you 100 times. U make me proud of my country
 
Almost mwaka mmoja uliopita nilikuwa na kauli mbiu humu kwamba kumchukia Diamond ni kujitafutia ugonjwa wa moyo bure! Watu hawakunisikia lakini lililo wazi ni kwamba, tangu nitoe kauli hiyo hadi sasa, wanachopata ni maumivu tu huku furaha yao pekee ni kusubiria scandal yoyote ya Diamond hata kama ni ya kijinga ndipo wajifekishe kufurahi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…