Patcho Mwamba Akanusha Kufumaniwa

Patcho Mwamba Akanusha Kufumaniwa

Richard Mlangi

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2012
Posts
380
Reaction score
193
Habari tulizozipata kupitia mtandao wa GPL zinasema,-MWIGIZAJI na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba hivi punde ameibuka katika ofisi za mtandao huu na kukanusha vikali-taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.

Akiongea na mtandao huo, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost yeye mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.

"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe
juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho akiwa katika ofisi za mtandao huu zilizopo Mwenge-Bamaga, Dar.

26.12.2014----Tags:- Patcho Mwamba-

http://www.bongomovies.com/news/update-patcho-mwamba-akanusha-kufumaniwa-na-kupigwa-adai-ni-pombe/557
 
Mods ningeomba uzi huu ubaki hapa ili kumtendea haki victim
 
Ha ha ha,ebu atuonyeshe kule behind kwake Kama Kuna usalama! Tujuavyo kadundwa na kazibuliwa na wababe...
 
kama anajua pombe inamvimbisha manundu mbona alikunywa? harafu sio kila kitu ukimbilie kujipiga picha na kutupia mtandaoni tuwe tunachagua picha
 
Huyu mkongo anapenda sana wanawake wa bure atakua kaingia tu kwenye anga za mke wa mtu., watu wakamfanyia yao.. Hio kujipiga picha na kusingizia pombe ni kuua soo tu.. Hapo 713 lazima ihusike... Pole sana papaa mopao ndo bongo daslaama hio.
 
majuzi alipanda jukwaani pale maasai club na kukanusha kufumaniwa...
 
​ukipigwa 0713 unaonekana alama eeeehhhh!! mwambie na bado kichapo kingine chaja...

Sio alama tu!!muhuri unagongewa!!ukipigwa ngumi ya jicho lazima alama nyeusi ivilie hasa kama jicho lilivimba kama vile!!
 
Uvimbe ule siyo wa allergy bali wa kupigwa. Mmwamba usituone wote humu jamvini kuwa wajinga
 
Uvimbe ule siyo wa allergy bali wa kupigwa. Mmwamba usituone wote humu jamvini kuwa wajinga

Kuna maswali ungejiuliza ili usionekane mjinga.

Kama kweli alifumaniwa angethubutu kukanusha ?

Na waliomfumania wangeacha akanushe ?

Halafu waliomfumania wampige picha moja tu ya passport size ?

Lini, ...wapi, ...na nani ...??? ...nk

Its not good to wish others bad things.
 
Kuna maswali ungejiuliza ili usionekane mjinga.

Kama kweli alifumaniwa angethubutu kukanusha ?

Na waliomfumania wangeacha akanushe ?

Halafu waliomfumania wampige picha moja tu ya passport size ?

Lini, ...wapi, ...na nani ...??? ...nk

Its not good to wish others bad things.

Kwa hiyo utaalamu wako unakutuma kuwa hiyo ni allergy? Hapana. Huyo kapigwa, inawezekana siyo katika fumanizi
 
Nimemwona Patcho Marry brown wala hana alama yeyote ya kichapo!!ile ilikua allergy!

Kinachowaponza watu wengi siku hizi ni kuexpose maisha yao kwenye social media na Shigongo hiyo kwake ni fursa.

Kuna jamaa zangu nikisomaga tu status zao Facebook huwa najuwa kabisa kimeshanuka kwenye Familia zao, ila wao hawajiulizi kwa nini wengine huwa tunauchuna tu kama hatupo kumbe huko Facebook naingia kila siku. Sina muda wa kupost ujinga au emotions na stress za kimaisha.
 
10897773_1112930352054715_1716959572468291439_n.jpg

Mwigizaji na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba ameibuka na kukanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo. Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost mwenyewe baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.

"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe juzi nilikunywa bia mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho.
 
Kinachowaponza watu wengi siku hizi ni kuexpose maisha yao kwenye social media na Shigongo hiyo kwake ni fursa.

Kuna jamaa zangu nikisomaga tu status zao Facebook huwa najuwa kabisa kimeshanuka kwenye Familia zao, ila wao hawajiulizi kwa nini wengine huwa tunauchuna tu kama hatupo kumbe huko Facebook naingia kila siku. Sina muda wa kupost ujinga au emotions na stress za kimaisha.

Teh teh
Awadh Samuel Kiwelu
eric kiwelu
 
Last edited by a moderator:
Shamvu la kopo limeisha tafunwa atulie tu libanebane wakale tena miaka yooote analewa hovyo apati hayo allegy ati leo ndo apate
 
Back
Top Bottom