Pato la wastani kila Mtanzania wafikia TSh 3.05 milioni kwa mwaka

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), pato la wastani la kila mtu nchini limeendelea kuongezeka kutoka shilingi 2,653,790 mwaka 2020 hadi shilingi 3,055,606 mwaka 2023.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, jijini Dodoma, katika Mkutano Mkuu wa CCM, alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, kwa kipindi cha miaka minne (2020 - 2024).

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeendelea kutekeleza sera za kujenga uchumi imara, kupunguza umasikini na utegemezi, na kudhibiti mfumuko wa bei nchini. Kiwango halisi cha ukuaji wa Pato la Taifa kimeongezeka kutoka asilimia 4.8 mwaka 2020 hadi asilimia 5.1 mwaka 2023.

Aidha, Majaliwa ameeleza kuwa Pato halisi la Taifa linakadiriwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka 2024, na kuongezeka hadi asilimia 5.8 mwaka 2025. Kwa upande wa mfumuko wa bei, umeshuka na kufikia asilimia 3.0 Novemba 2024, ikilinganishwa na asilimia 3.1 Novemba 2020.
 
Ni sawa na Laki mbili na nusu kwa mwezi.
ChoiceVariable
 
Kuna umuhimu mkubwa wa serikali kusisitiza mpango wa uzazi ili kufanya control ya population na kuengeza pato la wastani.
 
Haya ni matatizo ya kugawa pato la nchi kwa idadi ya watu waliopo. Hiyo milioni tatu inayoongelewa hapa inaonesha tofauti kubwa ya wale wenye ukwasi wa kufikia shilingi bilioni kwa mwezi na wale wenye ukata /maskini wa kutupwa ambao hawajui leo watakula nini.
 
Back
Top Bottom