Pato la Wastani Rwanda $583, Tanzania $434

Msaada wanauchumi. Pamoja na rasilimali nyingi nchini, pato la wastani Rwanda ambayo ni landlocked na isiyokuwa na utajiri mkubwa wa madini linazidi pato la wastani la mtanzania kwa $200 kwa mwaka. Nini chanzo cha mafanikio ya kiuchumi ya Kigali?

Umedanganywa au unadanganya Makusudi. Pato la wastani la mtanzania (Per capita income) mwaka 2012 ilikua $ 1,700 na GDP ya $ 73.5 billion http://www.theodora.com/wfbcurrent/tanzania/tanzania_economy.html
Rwanda pato lao mwaka 2012 ilikua GDP ya $ 14.91 billion na pato la wastani la $1,400. http://www.theodora.com/wfbcurrent/rwanda/rwanda_economy.htmal

Kwa data hizi utaona kwamba hizi ni nchi 2 zilizo katika 'level' tofauti sana. Hakuna cha kulinganisha hapo.

Uganda $ 1,400
Kenya $ 1,800
Burundi $ 600

ANGALIZO:
1. Data hizi hazina ukweli halisi kwasababu hazihesabu kipato cha mtu ambae analima na kula mwenyewe bila kupeleka sokoni (ambao ndio wengi kwa mataifa yetu)
2. Data hizi hazina maana yoyote kwasababu yapo mataifa yana pato kubwa la wastani lakini YAMEFILISIKA na hayawezi kujiendesha. kati ya hayo ni Ugiriki ($24,900) na Cyprus ($27,500)
 
Kama tatizo/suala ni idadi tu ya watu basi China na India zingekuwa maskini zaidi

Unafikiri kama china ingekuwa na GDP iliyonayo na idadi yao ingekuwa watu 300M uchumi wake ungekuwa kama ulivyo? Kwa kuangalia GDP per capita China bado inakuwa categorized kama nchi inayoendelea!!
 

Hizi hapa UN certified data. Kwa taarifa yako gni/gdp Rwanda tayari imefika $644 2013/2012.
UNdata | country profile | Rwanda
 

usilete data za uongo hapa haupo kirabuni.....2010 kwanza it was estimated Rwanda ilizalisha 20Kg za dhahabu wakati tz ilizalisha 42 Tons ....takwimu za United States Geological Survey Mineral Resources Program (USGS) accessed before US Gov Shutdown.....Critical USGS Web Sites available during Government Shutdown na pia madini yanayopatikana rwanda ni Tantalum,tangsten,na tin....bei ya tantalum ni USD 120 kwa 100g wakati dhahabu kwa sasa ninapoandika ni USD 1274.30/oz Newyork Stock Exchange na 1 oz = 28.345g ......Tz inatosha tu kuwa na raslimali hata kama hazifanyi kazi maana ni kama mtoto mdogo ukiwapatia biscuit mmoja hatakula ataacha mwenzake amalize ili amdontishie....bila kujua future is uncertain....huu ugonjwa umeenea katika vichwa at an individual level kama wewe unatetea uzembe eti watu ni wa chache...kweli ni wa chache lakini wanachapa kazi...na upande wa giant linasubiri change za radar ndo shule ziboreshwe....
 

Hapana, unajaribu saaana kutetea umaskini wa Tanzania.
Hesabu hizi ziko sahihi kabisa.

Tatizo la Tanzania ni uongozi mbaya sana, na huu uonogozi mbaya ndio wana-CCM wengi wanajaribu kuutetea sana.
Tanzania ina mali nyingi sana, ilitakiwa iwe tajiri sana kuliko Afrika Kusini, na wala sio kulinganishwa na vi-nchi kama Rwanda au Kenya.
Utajiri wetu karibu wote 'unaliwa' na viongozi na familia zao, ndio maana unasikia mambo ya akaunti zilizoko Uswisi, unasikia kashfa kama za EPA, BoT, Richmond, n.k.
Amkeni wa-Tanzania, nchi yetu inafilisiwa na viongozi mnaowatetea saaana.
 
Natambua jf si kilabuni, ila teknolojia inanifanya nikufikie toka hapa nilipo kwa mama siwatu nikipunguza uchovu wa jana. Nikuagizie supu ya kongoro!
Rwanda ni nchi ya kidikteta, hauwezi pata takwimu sahihi za uzalishaji. Kwenye nchi kama hii si ajabu kuona jeshi wana kitengo cha uchimbaji. Wachumi wetu na mtazamo mwepesi wa kimtandao! baadae utasema kenya wanazalisha tanzanite kwakua bepali weupe wanaipata huko. Supu yako tayari akuwekee na ngozi?
Wahanga wa vita wakubwa wadhaifu, wazee, watoto, na kina mama, wakipona wanaongezeka kwetu kama wakimbizi. Kundi tegemezi linapungua, rasilimali inagawanywa upya kibabe. Kiuchumi ni ushindi kwa waliobaki. Kama vita ilipangwa m.f. Rwanda. Salaam
 
ina maana familia ndogo ambayo kila mmoja anapata kipato cha 583 ni maskini kuliko familia kubwa ambayo kila mmoja wake anapata 434? Kajipange upya.

Kuna vitu vingi mmevifanya kuwa constant, mmesahau aina ya mgawanyo wa kipato. inawezekana kabisa sehemu kubwa ya kipato Cha Tanzania kipo mikonoi mwa Bharessa, Mengi, Lowassa, Rostam na wengine wachache wa hivyo.....huku wakiacha Watanzania mamilioni wakiwa hoi vivyo hivyo kwa Rwanda. To Me GDP ya nchi yangu siwi proud nayo sana, zaidi ya kupambana niwe sehemu wa wanaokata keki kubwa ya hiyo GDP
 
jumla ya pato gawanya kwa idadi ya watu........
 
Inamaanisha wao wamefanikiwa kutumia vizuri idadi yao ya watu ambao wengi wao ni wazalishaji.

Sisi tuna watu wengi wategemezi. Unakuta kuna vijana wapo kwa ndugu zao wanakula kulala bure lakini bado tunawafumbia macho!
 
Hizi hapa UN certified data. Kwa taarifa yako gni/gdp Rwanda tayari imefika $644 2013/2012.
UNdata | country profile | Rwanda

Link ina data za mwaka 2011 na zinakubaliana na nilichosema mwanzoni. Tatizo huna ufahamu wa haya mambo ya uchumi na fedha, ukiona GDP unaibuka tu bila kujua imetumika 'method' gani kukokotoa! Ukweli usiopingika ni kwamba uchumi wa nchi nzima ya Rwanda haufikii uchumi wa mkoa wa Arusha!
 
Unafikiri kama china ingekuwa na GDP iliyonayo na idadi yao ingekuwa watu 300M uchumi wake ungekuwa kama ulivyo? Kwa kuangalia GDP per capita China bado inakuwa categorized kama nchi inayoendelea!!

sure china ni nchi inayoendelea siyo developed country!!!!!
 
Kama tatizo/suala ni idadi tu ya watu basi China na India zingekuwa maskini zaidi


Pato la china unalifahamu mkuu? China na htaua waliyopiga lakini maisha ya wachina bado kabisa ndio maana wako kariakoo wanauza karanga.
 

Nazungumzia GDP per capita ie GDP/Total population. Kwa lugha nyepesi wastani wa thamani ya huduma na bidhaa anazozalisha kila raia kwa mwaka mzima.
 
Propaganda zingine toka RPF! hawa wahamiaji haramu (zaidi ya 10,000) walikuwa wafanya nini Tanzania kama huko Rwanda mambo yao mazuri kuliko TZ?
 
Propaganda zingine toka RPF! hawa wahamiaji haramu (zaidi ya 10,000) walikuwa wafanya nini Tanzania kama huko Rwanda mambo yao mazuri kuliko TZ?

umenena vyema.
Kuwa na pato kubwa sio kigozo tosha kuwa mnamaendeleo au wananchi wanamaisha mazuri.
 
Nazungumzia GDP per capita ie GDP/Total population. Kwa lugha nyepesi wastani wa thamani ya huduma na bidhaa anazozalisha kila raia kwa mwaka mzima.

Kila Raia (citizen) au kila Mkaazi (resident)? GDP per capita ndio nimeongelea tangu mwanzo na link zote nilizokupa na pia hiyo yako (Japo ya zamani sana) zinaonesha Tanzania iko juu kuliko Rwanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…