Tutafika
JF-Expert Member
- Nov 4, 2009
- 1,443
- 635
Msaada wanauchumi. Pamoja na rasilimali nyingi nchini, pato la wastani Rwanda ambayo ni landlocked na isiyokuwa na utajiri mkubwa wa madini linazidi pato la wastani la mtanzania kwa $200 kwa mwaka. Nini chanzo cha mafanikio ya kiuchumi ya Kigali?
Umedanganywa au unadanganya Makusudi. Pato la wastani la mtanzania (Per capita income) mwaka 2012 ilikua $ 1,700 na GDP ya $ 73.5 billion http://www.theodora.com/wfbcurrent/tanzania/tanzania_economy.html
Rwanda pato lao mwaka 2012 ilikua GDP ya $ 14.91 billion na pato la wastani la $1,400. http://www.theodora.com/wfbcurrent/rwanda/rwanda_economy.htmal
Kwa data hizi utaona kwamba hizi ni nchi 2 zilizo katika 'level' tofauti sana. Hakuna cha kulinganisha hapo.
Uganda $ 1,400
Kenya $ 1,800
Burundi $ 600
ANGALIZO:
1. Data hizi hazina ukweli halisi kwasababu hazihesabu kipato cha mtu ambae analima na kula mwenyewe bila kupeleka sokoni (ambao ndio wengi kwa mataifa yetu)
2. Data hizi hazina maana yoyote kwasababu yapo mataifa yana pato kubwa la wastani lakini YAMEFILISIKA na hayawezi kujiendesha. kati ya hayo ni Ugiriki ($24,900) na Cyprus ($27,500)