Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,606
- 1,711
Hatimaye kocha mpya wa Brazil, Mano Meneze, amemuita mshambuliaji chipukizi Alexandre Pato. Mpachika mabao huyo kinda aliachwa bila sababu ya msingi na kocha wa zamani, Carlos Dunga, katika kikosi kilichotolewa mapema katika Kombe la Dunia na kupelekea kufukuzwa kazi kwa kocha huyo mbishi. Lakini swali ambalo bado linawaumiza sana kichwa mashabiki wa samba, akiwamo Gang Chomba, ni, je, ipo siku kocha huyo mpya atamrudisha kiungo mahiri Ronaldinho Gaucho ambaye naye aliachwa hapo awali kwa sababa tata na tete. Swali hili linazidi kuwa gumu hasa baada ya kocha huyo kunukuliwa akidaia kuwa suala la umri ni kigezo muhimu kwa kuwa kuna vijana chipukizi ambao muda wao umefika hivyo wanastahili kupishwa na maveterani. Vijana hao ni pamoja na beki matata Rafael ambaye tayari anakubalika duniani. Je, huu ndio mwisho rasmi wa kumuona kiungo mtabasamushaji akiwa amevalia jezi za manjano na samawati?