Pato na Rafael Waitwa - Ronaldinho Kulikoni?

Pato na Rafael Waitwa - Ronaldinho Kulikoni?

Companero

Platinum Member
Joined
Jul 12, 2008
Posts
5,606
Reaction score
1,711
pato_ronaldinho_milan1.jpg

Hatimaye kocha mpya wa Brazil, Mano Meneze, amemuita mshambuliaji chipukizi Alexandre Pato. Mpachika mabao huyo kinda aliachwa bila sababu ya msingi na kocha wa zamani, Carlos Dunga, katika kikosi kilichotolewa mapema katika Kombe la Dunia na kupelekea kufukuzwa kazi kwa kocha huyo mbishi. Lakini swali ambalo bado linawaumiza sana kichwa mashabiki wa samba, akiwamo Gang Chomba, ni, je, ipo siku kocha huyo mpya atamrudisha kiungo mahiri Ronaldinho Gaucho ambaye naye aliachwa hapo awali kwa sababa tata na tete. Swali hili linazidi kuwa gumu hasa baada ya kocha huyo kunukuliwa akidaia kuwa suala la umri ni kigezo muhimu kwa kuwa kuna vijana chipukizi ambao muda wao umefika hivyo wanastahili kupishwa na maveterani. Vijana hao ni pamoja na beki matata Rafael ambaye tayari anakubalika duniani. Je, huu ndio mwisho rasmi wa kumuona kiungo mtabasamushaji akiwa amevalia jezi za manjano na samawati?
 
the stone that a builder refuse,will always be the head corner stone!,ngoja tuangalie labda huu usemi unaweza kufanya kazi.
 
picha za lini hizo - mbona alishalikata tumbo hilo na kulirudisha kwenye siksi paki!
 
Back
Top Bottom