Patrick Aussems ameibadilisha sana Simba SC

Shida ya sisi wabongo ni kwamba wote ni makocha. We ulitaka kanda afanane na Okwi kiuchezaji au?
Hao wabrazil mi naona wameanza vizr tu ukiangalia ni kwamba wametoka Kwenye mazingira na tamaduni tofauti.
Afu kutolewa kwa simba sio sababu ya usajili, ila ni matokeo ya mpira tu.
Tuache kujadili yaliyopita tujadili yanayokuja.
Tunaacha kuwapa Moyo wachezaji kwa kile wanachokifanya ila tunakua sehemu ya kuwabeza. Hata Okwi na kotei walikua bora kwa sababu ya timu kua na umoja nje ya uwanja na ndani ya uwanja.
@ Simba nguvu moja.
 
Mimi kwa upande wangu naona Shiboub na Tairone wapo vizuri ila kwa Deo Kanda na Fragas pale Simba kala za uso. Na huyo Wilker bado hatujui uwezo wake maana kacheza chini ya dakika kumi tu tangu ligi ianze.
Fraga(kiungo mkabaji haswaa) unamuona afai kwasabau hana mbwembwe za kupiga kanzu,tobo ila ni mchezaji mwenye kutekeleza majukumu yake uwanjani. Ila ni mchezaji mzuri tu.

Je nikikuuliza Fraga alichokosea nini kwenye mechi alizopangwa mkuu.
 
Kwa mtazamo wangu, “Gerson Fraga Vieira” ni mchezaji sahihi kwa Simba.

Anatimiza majukumu yake yale ya ‘Msingi’ na sio kucheza na Jukwaa kama Jonas.

Tofauti yake kubwa ni Kotei, Fraga anapiga pasi nyingi mbele wakati Kotei ni mzuri zaidi kwenye ‘Kukaba’ ila pasi nyingi alikuwa anapiga nyuma na kupelekea timu muda mwingi kubaki nyuma.

Mara nyingi katikati ya uwanja ndio ‘Transition’ ya mpira hufanyika,hivyo humuhitaji kiungo kupeleka mipira mbele kwa uharaka zaidi. Hili jukumu Kotei lilikuwa linampa shida sana japokuwa ni mzuri sana sana kwenye kukaba.

Nina imani na usajili uliofanyika,wachezaji wameonyesha kitu, kikubwa ni kuwapa nafasi zaidi na kuwavumilia.

Nani alijua kama Zana Coulibally angesajiliwa na As Vita na kupata nafasi? Wachezaji wengi wa kigeni sisi mashabiki ndio tunawafelisha na kuwakatisha tamaa.

Mashabiki wa Kitanzania tunaamini anaejua mpira ni yule mwenye ‘Madoido’ mengi ya kucheza na jukwaa.
 
Simba sio timu nzuri, bali ligi kuu imejaa timu mbovu , ndio maana walivyocheza na vibonde UD SONGO akina Kagere, Chama, Shibob hawakuonekana kabisa, ligi ya tanzania inatakiwa iwe na timu tano tu
Hahaa nadhani hili ni jibu sahihi kabsa

5imba wanajipima uwezo na Vilaza halaf wakikutana na team ya kawaida kama UD SONGO wanapigwaa

endeleeni kusubiri msimu ujao
 
Mkuu hapo kwa Shiboub habari nyingine hyo,,

Kwa Wabrazil tumepgwa nakubali kabisa,

Ukweli ni kwamba huo usajili kocha hajausika kabisa,,
 
Simba sio timu nzuri, bali ligi kuu imejaa timu mbovu , ndio maana walivyocheza na vibonde UD SONGO akina Kagere, Chama, Shibob hawakuonekana kabisa, ligi ya tanzania inatakiwa iwe na timu tano tu
Mkuu hadi leo yanga kacheza game moja tu VPL,,

Ratiba si rafiki
 
Umeanza vizuri kumbe takataka.
 
Shiboub
 
Yanga wakupe nafasi pale,,


Nimegundua ww unaujua mpira [emoji3]
 
Kwa Fragas na Deo Kanda sijui wenzangu mnatumia vigezo gani. Wachezaji wapya wanaposajiliwa tunategemea wawazidi wale waliowakuta na waliondoka. Tukianza na Fragas je anakitu gani cha kumzidi sana Mkude pamoja na mapungufu yake? J
Mkuu, huyo Mkude si yupo Simba? Sasa ulitaka Simba wamsajili Mkude badala ya Fraga, wakati tayari Mkude yupo Simba!
 
Hapo umekwepa swali.Kama kocha ni huyuhuyu na simba ya msimu uliopita ilikuwa bora kuliko hii basi msingefungwa zaidi ya magoli 10.Kocha naye anaudhaifu kwa sababu simba sio nzuri kwenye beki ikikutana na safu imara ya ushambuliaji.Kocha muda wote anafunguka,haeshimu wapinzani mwisho wa siku mechi 3 magoli 15+
Kile kilitufanya tukaingia Robo fainali ya Champions League!
 
Wenzio mliokuwa nao walifungwa magoli 10+?
Ni sawa na mwanachuo aliemaliza degree ya kwanza kwa kupata sup 7 na carry 2 GPA 1.8.
Ni kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa wa Afrika. Hauwezi kufungwa hizo usipofikia hatua hiyo
 
Kanda nadhani tumeuziwa saa kumi 12, alikuwa mzuri Sana kwa wale ambao tunamfahamu, alikuwa mzuri ila kwa Sasa amebaki na maufundi tu but Hana sumu golini, shiboub ni mtu na nusu, fraga na yule beki mbrazil ni wazuri, wanafanya majukumu yao vizuri, siyo wabaya wakizoea ligi na soka la kiafrika watakuwa poa, kahata pia ni mzuri akicheza katkat I mean namba kumi, ila winger sidhani Kama inamfaa Sana, kutolewa kwetu nadhani tumeanza kucheza qualifications bila hata kucheza mechi za ligi compared na last season tulikuja kucheza champions league katkat ya league, wachezaji walisha zoeana na pia match fitness walikuwa nayo msimu huu, zaidi ya mechi ya Simba day
 
Kanda yupo kwa mkopo wa mwaka 1 kutoka TP Mazembe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…