Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Mimi sio mtu wa kupangiwa unapaswa kufanya hiki kwa wakati gani kwasababu uliniajiri ili nifundishe sasa kwanini unipangie cha kufanya?
Kwasasa nafahamu sio kocha anaendaa kikosi cha kwanza hilo nafahamu wazi kwa kocha mahiri aliyeifanya kazi yake kwa muda mrefu ni ngumu kukubaliana na hiyo hali..
Niwe Mkweli mmiliki wa timu mara zote huniita kabla ya mchezo na baada ya mchezo nilikuwa nazungumza nae na mara nyingi alikuwa akihitaji kuona kikosi kinachoanza na nnamwambia hapana subiri mchezo ufike na baada ya hapo niliwambiwa napaswa kuwa makini..
Haikuchukuwa muda baada ya wiki nilifahamu michezo yote ndani ya timu kwanzia kwenye uongozi mpaka kulazimishwa kuwachezesha baadhi ya wachezaji na nikafahamu ni watu wa aina gani?
Mara nyingi walikuwa wanajaribu kuwafuata wasaidizi wangu na kufahamu nimempanga nani kwanzia madakitari wa Timu na wiki yangu ya kwanza tu kwenye kuiandaa timu nilimfukuza msaidizi wangu kwasababu nilijua anatumika na uongozi na baada ya hapo nikamchukuwa Denis Kitambi
Kuna watu wapo Singida zaidi ya miaka 6 hivyo mawazo yangu nilijua hii klabu inaenda kukua sana na niseme wazi tu kuwa Mmiliki wa timu hana watu sahihi wa kuiongoza timu yake
Aliyewahi kuwa kocha wa Singida Black Stars Patric Aussems amezungumza haya leo, Februari 19, 2025 kwenye kituo cha Crown FM.
Pia soma Kocha Aussems (Uchebe) aibua mazito: Wachezaji wa Singida hawakufurahishwa na kikosi kisicho cha ushindani dhidi ya Yanga