PreGE2025 Patrick Kipangula: Waandishi wa Habari wasiosajiliwa na Bodi ya ithibati kukutana na Rungu la TRA

PreGE2025 Patrick Kipangula: Waandishi wa Habari wasiosajiliwa na Bodi ya ithibati kukutana na Rungu la TRA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Serikali kupitia Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imetoa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia May22,2025 hadi June 21, 2025 kwa Waandishi wa Habari wote wanaofanya kazi za kihabari nchini, kujisajili kupitia Mfumo wa TAI-Habari, ili kuomba kuthibitishwa na kupewa vitambulisho (Press Card) ambapo imesema muda huo ukipita Waandishi watakaofanya kazi bila ithibati watachukuliwa hatua ikiwemo kulipa faini au kufungwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula amesema kutokana na uwepo wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu, Waandishi wote wa Habari watakaotekeleza majukumu ya kihabari yanayohusiana moja kwa moja na mchakato wa uchaguzi huo wanapaswa kuwa wamethibitishwa na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari na kwamba Wamiliki wa Vyombo vya Habari watakaoendelea kuwaruhusu Waandishi wasio na ithibati kufanya kazi watakutana na rungu za Mamlaka zinazowasimamia ikiwemo TCRA.

“Bodi inawahimiza Waandishi wa Habari kutumia ipasavyo muda uliotolewa kwa ajili ya kujisajili na kupata vitambulisho, ili waweze kufanya kazi za kihabari kwa mujibu wa sheria, usajili huo pia utatoa fursa ya kuundwa kwa Baraza Huru la Habari, kama inavyoelekezwa katika Kifungu cha 24 cha Sheria ya Huduma za Habari, Sura 229, Waandishi wote wanapaswa kujisajili kupitia kiunganishi cha TAI-Habari
Kabla ya kuingia katika kiunganishi hicho mwombaji anapaswa kuwa na mahitaji yafuatayo; namba ya simu na barua pepe vinavyofanya kazi, namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) pamoja na ada ya Ithibati shilingi Elfu Hamsini (50,000 kwenye simu kwa urahisi wa kulipa)0

Kwa mujibu wa Kanuni ya 17 (1) (a) ya Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari, Tangazo la Serikali Na. 18 la tarehe 03 Februari, 2017 wanaopaswa kujisajili na kupewa Ithibati ni pamoja na Waandishi wa habari, Wahariri, Waandishi wa kujitegemea (Freelancers na Correspondents), Watangazaji wa Radio na Televisheni, Wapiga picha, Waandaaji wa vipindi vya habari (News Producers) na Waandishi wa habari wa kigeni”
​
 
Back
Top Bottom