Patrick Mafisango Dead: Former Rwanda Soccer Captain Dies In Car Crash.

Dah!!! Uvumilivu umenishinda ngoja nikalie weeeeeeeeeee mpaka hacra iniishe dah..... R l p mafisango kipenz chetu
 
Ndio maana nikaweka kiulizo kana kwamba unapowataja Maestro hao niliowaorodhesha je nimuweke na yeye?

Then umenishauri nimuweke Sir Paul Scholes well ntamuweka.
Je na Sir mwenzie Elton John?

Muweke na rafiki yako sir.Davd Camerun
 
hapa nyimbo zilizo tamalaki ni nyimbo za dini ya kikristo tu."zawadi gani hii ya kumtolea bwana ila roho yangu tuu..pokea sifa hizi bwana tena uzibariki bwana..."
 
naona wanakaribia kumaliza kuaga bila shaka watakatiza watu kabla hawajaisha sababu wamemuambia mchungaji Titto siame aanze kujiandaa kwa ajili ya sara za mwisho kabla ya kufunga jeneza. nafikiri haitachukua mda mrefu kutoka sasa jeneza kufungwa.
 
baadhi ya waimbaji na wapiga vyombo wa akudo impact wapo maeneo haya. kumbuka mafisango alikuwa mshabiki mkubwa wa akudo na usiku aliopata ajali alikuwa club maisha na waimbaji wa akudo.
 
yani mi nalia tu, hata siamini, nackilizia kwa mbali nyimbo za hapo msibani. Kwaheri Patrick
 
baada ya kuaga hapa mwili wa marehemu mafisango utapelekwa uwanja wa taifa wa mwalimu Nyerere kuhifadhiwa tayari kwa safari hapo kesho kuelekea congo kinshasa.
 
Aya bwana kila lakheri mungu awatangulie mwanzo mpaka mwisho kumpunzisha kijana wetu ameeen
 
vilevile mkuu wa mkoa wa dar es salaam ndg. meck sadick yupo maeneo haya. wacongo wakifika wanapewa nafasi ya kuaga mapema kuliko wenyeji. mfano hawa akudo wamekuja sasa hivi but wamesha aga na kukaa pembeni wakati wengine wakiungua jua. hiyo ni kazi ya polisi.
 
yaani nimeipenda sana style yako ya ku update hili tukio mkuu wangu dubu ...hasa hiyo sehemu ya watu kupigwa virungu umeifafanua safi sana
 
kwa ufupi mwili wa mafisango unaonekana kubondeka kwenye paji la uso yaani pamebonyea. na mdomoni pametapakaa damu. inaonekana alipata majeraha ya kichwa.
 
kwa ufupi mwili wa mafisango unaonekana kubondeka kwenye paji la uso yaani pamebonyea. na mdomoni pametapakaa damu. inaonekana alipata majeraha ya kichwa.
Chondechonde mkuu,usiweke picha ya mwili wa marehemu hapa,maana ni makosa makubwa kwa M/mungu na kwa maiti yenyewe kuidhalilisha.
 
Aden Rage anasema "Nawashukuru wanasimba, waziri wa africa mashariki samwel sitta, mkuu wetu wa usalama wa dar es salaam meck sadick, jeshi la polisi na watu wote hasa wahudhuliaji wa hii shughuli kwa kuwa wavumilivu na wasikivu. Nidhamu iliyo onyeshwa ni ya hali ya juu kiasi kwamba hakuna aliyepigwa kirungu wala kusukumwa kwani walikuwa wasikivu asanteni sana.
 
Chondechonde mkuu,usiweke picha ya mwili wa marehemu hapa,maana ni makosa makubwa kwa M/mungu na kwa maiti yenyewe kuidhalilisha.

Mkuu jf ndo sehemu ya kuongea kila kitu. nitaweka tahadhali mwenye roho nyepesi asiangalie.
 
kwa ufupi mwili wa mafisango unaonekana kubondeka kwenye paji la uso yaani pamebonyea. na mdomoni pametapakaa damu. inaonekana alipata majeraha ya kichwa.
Chondechonde mkuu,usiweke picha ya mwili wa marehemu hapa,maana ni makosa makubwa kwa M/mungu na kwa maiti yenyewe kuidhalilisha.
 
Nawapa pole wapenzi wa soka Tanzania na Africa masharika kwa ujumla kwa kuondokewa na kiungo mshambulia Patric Mafisango, kwa pamoja tumeguswa sana na msiba huu. R.I.P Mafisango
 
born 1980 dead 17 may 2012. Oli mpwa wake na marehemu vilevile alikuwemo kwenye ajali.
Sasa hivi wamesha piga stop watu kuaga na mch.Titto ndo anatoa ruksa ya kufunikwa kwa jeneza. ndugu wa marehemu ndo wanaenda kufunika jeneza kama ishara ya kumzika marehemu.
 
Mkuu jf ndo sehemu ya kuongea kila kitu. nitaweka tahadhali mwenye roho nyepesi asiangalie.
Tatizo siyo roho nyepesi wala roho ngumu,tatizo hapa ni kwamba ni makosa makubwa kwa M/mungu!
 
mchungaji titto kasoma kitabu cha WARUMI 9:14. MCH.CHILWA ndo anafunga kwa maombi ya kuahilisha shughuli hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…