Paukwa... Pakawa!


nakuunga mkono mzee, kama kikwete akifanya kweli, watakao kalia msumari ni hao mawaziri etc, na kwa Mkapa naombea Bunge limvue kinga, na hata kama hato fungwa, wamfilisi mali zake na kumbakizia kidogo, zakumwezesha kumalizia siku zake, na ku-black list kwamba he was one of the worst president in Tanzania, ambaye hafai kuwekwa kwenye kumbuku za Viongozi, wastaafu.
 

Kutokana na mambo yanavyokwenda inabidi na rais pia ajiuzuru ili kupisha haki itendeke kwa kila anayeusika,kama alinyofanya mbeki baada ya kushutumiwa kua anaingilia mwenendo wa kesi ya zuma.lakini kwa kiasi kikubwa kikwete hizi kesi zote zinamgusa kwa namna moja au nyingine,hivyo ili haki iweze kupatikana ni lazima na yeye hajiuzuru ktk hili.
 
Nurujamii,
Nadhani sasa hapa hakuna logic bali ni chuki binasfi kwa Kikwete. Kwamba humtaki tu, basi!

Mkuu haya maneno mazito sana na sidhani kama kweli Rev, Kishoka amefika huko isipokuwa nadhani tatizo linalowasibu wengi hapa ni kesi zenyewe zilizowakilishwa dhidi ya viongozi waliotajwa zinaonekana kuwa ni DHAIFU sana kiasi kwamba zinaacha mwanya na penyo za ushindi kwa watuhumiwa. Jana tu nilikuwa naongea na mshikaji akanambia kwa nini anaona kuwa hili ni changa la macho!

Kama unakumbuka hapa JF sote tumepiga kelele kuwa hawa jamaa ni WAHUJUMU uchumi kwa hiyo tulitegemea kesi zenyewe ziwe ktk kundi hilo la mashtaka lakini inaonyesha wazi kuwa ni swala la Negligence or misconduct ktk ofisi zao...Jambo ambalo linapunguza nguvu ya mashtaka ya Hujuma walizofanya..

Kwa hiyo sio kwamba JF hakuna watu wanaoweza kumuunga mkono Kikwete isipokuwa kilichotakiwa haswa kufanyika sio tu kufikishwa watu hawa mahakamani isipokuwa kesi dhidi yao ziwe zile ambazo sote tunazijua..
Hadi sasa hivi namuunga sana mkono at least kaweza kuinua kidole!...Sasa hivi ndio baadhi ya Wadanganyika wanaanza kujua Mkapa alifanya nini..yet nashangaa bado wapo wanaosema alikuwa kiongozi bora!.. Yale yale ya Mugabe na wafuasi wake.
 


Rev alipoanza kuelezea hili, wengi pengine, hawakumuelewa.

Kuna mdau anasema, eti Rev anachuki binafsi na JK!!

Kuna wakati watanzania wanakuwa vipofu, ila si wote, kutupumbaza kwa kumuweka Yona na Mramba, kunaelezea mengi juu ya serikali ya JK na BMW.

KWANZA JK ALIMTEUA MRAMBA KUWA WAZIRI???? WHEN WAS ALEX STEWART HAPPENED??/

JK wakati anamteua mramba , EL, Chenge alijua fika kuwa thsese guys are not clean!!!!

unapozungumzia mikataba mibovu mingi JK alikuwa waziri nyakati hizo nae alihusika kwa namna moka ama nyingine, tena ashakuwa waziri wa nishati na madini.

Mkuu unaposema JK AJIUZULU UNAJIVUA KUTOKA KWENYE MACHO YA VIPOFU WENGI WANAOTAKA TUAMINI JK, IS CLEAN, WAKATI WAMESALETA HASARA YA ZAIDI YA HIYO BILIONI11.

JK JIUZULU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


waberoya
 
Waberoya,
Mkuu sasa na wewe unatoka nje kwa sababu anayewashitaki hao watu sio Kikwete isipokuwa ni serikali ya Tanzania. Sasa tunapojaribu kusema kuwa mhusika wa mipango ya kesi hizi ni Kikwete moja kwa moja tunakuwa tunapotosha Umma..
Kikwete ameruhusu vyombo vya sheria vichukue hatua kuhusiana na watuhumiwa na sidhani kama ni kazi yake kufungua ama kupanga mashtaka gani yafunguliwe wala sidhani kama ni yeye aliyefanya uchunguzi, tujaribu kutafuta kiini cha vitu hivi badala ya kulaumu tuuu..Mfano kwa nini Kuhujumu Uchumi haikuwa sababu kubwa ya viongozi hawa kupandishwa Kisutu..
 


Mkuu Nurujamii
Mashaka ni lazima yawepo hata kama hukumu itasomwa kuwa wameadhibiwa kwa mujibu wa sheria. Swali ni kwanini mashaka yawepo...Watanzania hawakuwa watu wa mashaka kwa viongozi wao. Laghai ya viongozi kwa Watanzaia ndio chimbuko la mashaka haya. Uaminifu na uadilifu wa watanzania (walio wengi) kwa viongozi wao ndio wamelipwa fadhila ya kuibiwa na kunyang'anywa haki yao.
Kesi za kushindwa (kama anavyozibainisha MMJJ) zipo nyingi sana. Mbaya zaidi ni wasiwasi wa kuja kuwalipa fidia hawa watuhumiwa wa wizi pale watakaposhinda kesi hizi.
Lazima watanzania wajiandae kujua mwisho wa paukwa hii, mawazo mbadala ni lazima yawepo na yapewe nafasi. Maoni mengi yanatokana na uzoefu wa "funika kombe" na "changa la macho" mpaka itakavyobainika vininevyo
Hakuna mtu anachuki na mtu bila sababu. JK hachukiwi ila matendo yake ndio yanaleta chuki (kama unaziona ni chuki). Uongozi si kitu rahisi, tena kama wake yeye wa kuzunguka nchi nzima akibebeleza kura. "Kutupa raha" Watanzania ni moja ya ahadi zake "maisha bora kwa kila mtanzania"
 

Nurujamii,

Tatizo si watu kupelekwa mahakamani, bali jinsi mazingira na mashitaka yenyewe yalivyo.

Nimeweka kwa umakini maamuzi ya Serikali mabovu(kwa mtazamo wangu na wengi hapa JF) ambayo ama yalitokana na uzembe au matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi wake na kuuliza, je hawa nao watafikishwa mahakamani?

Suala la Alex Sterwart ukisoma kiini cha kosa, utagundua ni kitu ambacho yeye Kikwete alikifanya akiwa waziri wa Madini, waziri wa fedha, kimefanywa na Mbilinyi, Kitine, Iddi Simba, Lowassa, Chenge, Msabaha, Meghji, Karamagi, na mawaziri wengine wengi.

Ama nikilenga kwenye mfano mmoja kama ule wa Karamagi kwenda kusaini mkataba mpya wa Buzwagi uliosababisha Zitto kusimamishwa kazi na hata Kikwete kuunda kamati, unakuta kuwa Waziri alitumia madaraka yake ambayo kapewa na Serikali na Katiba ambayo yanampa uwezo wa kufanya maamuzi kama aliyofanya Karamagi.

Tulipopiga kelele kuhusu kitendo cha Karamagi, tukaja baini kuwa kelele zetu ni bure kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba na mamlaka ya Waziri wa madini(kama Ngeleja alivyosema hivi karibuni), Waziri ana uamuzi binafsi bila kumshirikisha mtu kuamua ni jinsi gani mkataba uwe, mwekezaji apewe misamaha ya kodi na ushuru hata kuongeza muda wa mkataba.

Walichofanya Mramba na Yona hakina tofauti na alichofanya Kikwete akiwa Waziri wa madini. Yeye Kikwete ndiye katika utawala wake, na ile jazba ya Serikali kuchochea Uwekezaji, alitoa kibali na kukabidhi umiliki wa ardhi yote yenye dhahabu kwa Sinclair. Leo hii mtu yeyote anayetaka kuchimba madini, lazima amuone Sinclair, alipe ada kisha apewe ruhusa ya kufanya survey na uchimbaji.

Serikali ya Tanzania inaambulia 3% ya ,malipo ambayo mwekezaji huyu kamlipa Sinclair. Je swali ni hili, ni nani alimpa mamlaka Kikwete ya kuingia makataba na Sinclair wa kutupa mapato duni kiasi hicho? Ikiwa TanRange au ndio Tanganyika Royalty kampuni ya Sinclair ina pata faida marudufu, je si ni halali kabisa kumfungulia mashitaka Kikwete na mawaziri wengine wote ambao walitumia madaraka yao kushinikiza uwekezaji na kukubali mikataba ambayo inaipunja Serikali na zaidi kutumia kichocheo cha msamaha wa kodi?

Ndio maana nauliza haya mazingaombwe ni mpaka lini? Yona na Mramba hawatafungwa, kama Kiula wataachiwa huru kesi ikimalizika, kwa kuwa itabainika kuwa maamuzi yao hayakuwa na dhamira ya kufanya kosa la jinai au kuhujumu.

La pili, jiulize, kama kosa lao kina Mramba, Yona na hata Jeetu Patel, Lukaza na Mwakosya wa BOT ni makosa ya kuhujumu uchumi kwa mijibu wa sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 1964 ambayo bado inatumika (reference kesi ya Mahalu), je ni mamlaka gani mahakama ndogo kama ya Kisutu iliyonayo kusikiliza kesi hizi? Kwa nini hazikupelekwa Mahakama Kuu ambako kwa mujibu wa Sheria ndipo kesi hizi zilipaswa zisikilizwe?

Ni kwanini kwa Ukihiyo wangu wa masuala ya Sheria na Katiba, naona mianya mingi ambayo inaonyesha udhaifu mkubwa wa kesi hizi na kukosekana kwa umakini kutoka kwa TAKUKURU, DPP na AG?

Kwa nini kesi hizi zinanikumbusha kesi za Vhalambia na hata ile ya Tanesco na IPTL kule London?

Hivyo basi, kwangu ni changa kali nami nimelivalia miwani ya mwogeleaji Michael Phelps!
 

Jamani eee, pamoja na Ukihiyo wangu, lakini najua kusoma na kufikiri!

Ukisoma hiyo nukuu ambayo TAKUKURU wameiweka katika kumfungulia kesi Mramba, utagundua kuwa Mramba hakufanya alichokifanya kwa siri, bali alikitangaza hadi kwenye Gazeti la Serikali.

Sasa najiuliza tena, kama Mramba alifanya hivi kwa miaka mitano mfululizo, Raisi wake, Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa TRA, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Baraza la Mawaziri, Wabunge na wale wote wenye mamlaka kumhoji na kumsitisha kufanya alichokifanya, walikuwa na mtazamo gani waliposoma matangazo haya ya misamaha kwenye Gazeti la Serikali? Kwa nini walikaa kimya hata wao TAKUKURU?

Kwa nini tulimruhusu Mramba kwa miaka mitano aendelee kutoa msamaha kinyume na sheria za mamlaka ya kodi ya mapato? Kwa nini TRA hawakulalamikia hili hata kulipeleka Ikulu au kufungua mashitaka pale uvunjaji huu wa sheria na matumizi mabaya ya uongozi ulipotokea?

Je Waziri, Baraza la Mawaziri, Tanzania Investment Center, Mkuu wa TRA na hata Rais, wana nguvu na mamlaka gani kisheria wanapotoa misamaha ya kodi? Je maamuzi yao ya kuvutia wawekezaji hayapingani na sheria na mamlaka za TRA?

Je waziri wa fedha na hata waziri wa viwanda na biashara si wana turufu ya kutoa maamuzi ya misamaha kupingana na sheria au bado Mchungaji anachanganya mambo?
 
We can't be sure for now, mpaka tuone kama sungura atabaki kwenye kofia baada ya mazingaombwe as MMKJ puts it.

However, it is really doubtful whether JK is doing this for a genuine love for his country or for the sake of getting back part of his lost popularity
 


Mkandara:

Kuna kitu kimoja, nchi itumie sheria au ifanye hukumu kuridhisha wananchi. Unapohamua kutumia sheria ni lazima hoja ijengwe ya kisheria. Yona anaweza kuwa na nyumba nzuri Arusha wakati mshahara wake hauwezeshi yeye kuwa na nyumba hiyo. Kama unatumia sheria ni lazima u-prove kuwa nyumba hiyo haikupatikana kihalali na sio kutumia maoni ya wananchi.

Wachangiaji wengi hapa wanataka hukumu itolewe kwa kufuata maoni ya wananchi kama vile mitaani tunavyomshusha mwizi wa kuku.

Mfano mzuri ni Al Caponi. Al Caponi alitumia u-Mafia kuua watu lakini hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kumfunga. Lakini mwendesha mashitaka aliweza kumfunga kwa kutumia kipengele cha tax. Tax aliyolipa ilikuwa ndogo kuliko Mali aliyomiliki. Hivyo alipatikana na kosa la kukwepa kulipa tax na aliramba mvua ya miaka 11.

Kwa mtaji huu UDHAHIFU wa kesi sio kitu muhimu sana iwapo watu watakwenda ndani na haki kutendeka.

Lakini kama UDHAHIFU wa kesi ni kumfanya mshtakiwa ashinde, that's another story.
 

Pundit,

By the way I hear the Wahisani are refusing to put their signature to the 40% URT 2008/09 budget until Kieleweke!

Now I am confused, is it a daily double, campaign 2010 and lets have wafadhili release mshiko or all bets are off to hell with Mtandao or Umoja ndani ya CCM?
 

Kwako Mkadara:

Nimefurahi na kushukuru sana kwa maoni haya.

Imenichukua muda mrefu kutafakari toka huko nilikokuwa na hata kurejeea jamvini kushiriki mchakato.

Nilikuwa na maswali yamsingi yananitatiza ambayo naona kama umeyajibu tena very clearly...ingawa unasema ni hisia zako tu!!

Nilijiuluiliza:

1. Kikwete yuko consistence na anachokinfanya.?
2. Ana clear definitinon ya anatoka wapi na anakwenda wapi?
3. Ana Principal na mwelekeo unaoelezeka kwa A-Z na sio kuwa anakurupuka?
4. Inamaana he was learning the MOVE all the time before He CONFRONT...Mhhh ...does it mean He is that Clever??
5. Inamaana He is so good to have that clarity and patince....REALLLLLLY?

MKANDARA:

Post yako inanifanya niamini kuwa Umejibu maswali yangu yote. . . Inanifanya nione kuwa anachokifanya sasa sio mchezo wa kitoto! Ameanza na atamalizia kwa heshima ya taifa na faida ya kila mtanzania na sio maslahi yake ya utukufu wa uchaguzi ujao au vitu kama hivyo.

Mkandara unataka niamini hivyo...?
 

Waberoya:

Inabidi utumie the following doctrine; "You go to war with the Army you have but not with the Army you might want or wish to have at a later time."

Unaposema JK jiuzulu, je hiyo process ya kuwapata watakatifu wa kuongoa mafisadi itafanyika wapi?

Na nani ame-guarantee kuwa atakayechukua baada ya JK kujiuzulu atakuwa bora zaidi?

Politics ni ku-seize the moment.
 

Mimi natofautiana na wewe kiasi,ktk nchi inayofuata utawala wa sheria ambapo tanzania haimo,raisi wa nchi hana mamlaka ya kuwafikisha au kutoa kibali ili mtu afikishwe mahakamani,bali ni vyombo vya dola vyenye dhamana ya kushughulia maswala yote ya ukiukwaji wa sheria na taratibu za nchi.

Lakini bongo eti mpaka mtu fulani aseme ndio wengine wafuate,raisi pamoja na serikali yake kazi yao ni kuwasimamia watendaji ikiwa na kuondoa uzembe wote uliopo kwa watendaji ambao awatekelezi majukumu yao waliyokabidhiwa na wananchi.

Kumbuka ule msemo wa nchi haitakalika au itayumba ni pamoja na wakuu wa serikali kwa na uhusiano wa haya mashitaka.
 

Mkandara.

Nafikiri huu ndio msingi wa hoja yenyewe!!
 

Kwa mtaji huu ni mwendasha mashitaka na vyombo vingine vya usalama na sheria ndivyo vyenye kuhusika na sio Rais.

Hivyo Jaji Samata akitoa hukumu kuwa Mramba na Yona waachiwa mara moja. Kwa mila zetu, lawama zitakuwa kwa Rais na sio kwa Jaji.
 

Zakumi,

Wakati wa kikao cha bajeti cha Bunge, Bernard Membe alisema kuwa kuhusiana na suala la EPA, wananchi wajiandae watafurahishwa na Serikali kuhusiana na mambo ya EPA. Sasa tunafurahishwa tunapiga kura za Ndiyo, miezi 22 kabla ya uchaguzi!
 

A perfect 10 point score to question the validity of this move!
 

Rev.

Ni hoja hii na nyingi kama hizi zinanifanya ni pelee kutoa vifijo na nderemo kwa kinachotokea nchini.

Ninashidwa kabisa kupata clear definition of what is going on to the extent ya kutoa warm congratulation to the..Kwa kinachotokea.

Ni kweli kuna kanuni concrete na objective principles guiding all this? Au ni vurugu vurugu tu?

Sina tatizo kwa kinachoonekana kuwa ni maendeleo mazuri etc...Tatizo ni kwa kile kilicho nyuma ya kinachoonekana.

Ni kweli kabisa kuwa Ukiwa ndani ya gari linalokwenda kasi Utaona kama miti na mazigira yote kule nje navyo vinakwenda kasi .... in the opposite direction. Sawa ..all is moving ..lakini Ni muonekano tu! In reality hakuna kinacho Move.

Najua hoja hii inaendela na nitaelimishwa zaidi.
 
Zakumi,

Wakati wa kikao cha bajeti cha Bunge, Bernard Membe alisema kuwa kuhusiana na suala la EPA, wananchi wajiandae watafurahishwa na Serikali kuhusiana na mambo ya EPA. Sasa tunafurahishwa tunapiga kura za Ndiyo, miezi 22 kabla ya uchaguzi!

Rev Kishoka:

Na ndio hapo demokrasi inapofanya kazi. Iwapo kiongozi atafanya vizuri na sio kuwafunika watu macho katika kipindi cha miezi 22 kabla ya uchaguzi atakuwa amelisaidia sana taifa.

Kwa mfano Bail out ya $700 Billion na Stimulus inayokuja itagemea kufanya kazi miaka miwili baada ya kutolewa (miezi 24 ambayo ni karibu sana na miezi 22).

Miezi 22 ni mingi sana katika shughuli za kisiasa. Chukua mfano. Sokoine alikuwa waziri mkuu kuanzia 24 February 1983 mpaka 12 April 1984. Katika kipindi hicho cha mwaka mmoja alitia watu ndani.

Hivyo serikali yetu ina tools zote za kufanya mabadiliko katika kipindi cha miezi 22.


Kuna mtu anasema kuwa Europeans wanapenda process. Na waMarekani wanapenda results.

Hivyo inabidi tuchague kuwa kama waEurope au WaMarekani. Tukiwa kama waEurope itabidi tuangalie kipindi kizima. Na kama tutakua kama wamarekani basi results hata kama hizo results zinapatikana miezi sita kabla ya uchaguzi.

Mfano mzuri ni michezo. Wamarekani hawapendi soccer kwa sababu ni mchezo wa process. Na michezo ya ni lazima mshindi apatikane hata kama ni dakika ya mwisho.

Kwa upande wangu nataka watu waende ndani tu. Hata kama wataende siku moja kabla ya uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…