Rev Kishoka and other 'skepticists' ningependa kujua ni nini hasa mlitaka Rais afanye kwa sasa? Ajipeleke yeye mwenyewe mahakamani au? Nafikiri hata kama hatuamini sincerity ya Rais kwa sasa tutoe basi alternative wakati tunapom-critique! Inachukiza mtu aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote mafisadi kupelekwa mahakamani, hadi kuamini kuwa kamwe hawatapelekwa mahakamani sasa anabadilika baada ya kuona wamepelekwa. Process inapoanza anadai hakubaliani na hilo kwa sababu anayeisimamia hiyo process naye ni muhusika katika ufisadi. Kwa hiyo afanyeje sasa! aache?
Sio kama nakataa kwamba kuna uwezekano wa kupigwa changa la macho, lakini kinachotakiwa sasa is to critique constructively. Pia kumbukeni sio lazima kubisha kila kitu ili uonekane unayajua mapambao sana au wewe ndio mwenye uchungu na nchi yetu kuliko wengine. Nimefikiria sana nini kinatakiwa Rais afanye ili apate support hapa JF lakini nimegundua hakuna. Labda ajipeleke mahakamani mwenyewe na kujiuzulu uraisi tu!
Nadhani sasa hapa hakuna logic bali ni chuki binasfi kwa Kikwete. Kwamba humtaki tu, basi!
Haya ni maoni yangu tu and I am open and flexible to change my position!
Nurujamii,
Tatizo si watu kupelekwa mahakamani, bali jinsi mazingira na mashitaka yenyewe yalivyo.
Nimeweka kwa umakini maamuzi ya Serikali mabovu(kwa mtazamo wangu na wengi hapa JF) ambayo ama yalitokana na uzembe au matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi wake na kuuliza, je hawa nao watafikishwa mahakamani?
Suala la Alex Sterwart ukisoma kiini cha kosa, utagundua ni kitu ambacho yeye Kikwete alikifanya akiwa waziri wa Madini, waziri wa fedha, kimefanywa na Mbilinyi, Kitine, Iddi Simba, Lowassa, Chenge, Msabaha, Meghji, Karamagi, na mawaziri wengine wengi.
Ama nikilenga kwenye mfano mmoja kama ule wa Karamagi kwenda kusaini mkataba mpya wa Buzwagi uliosababisha Zitto kusimamishwa kazi na hata Kikwete kuunda kamati, unakuta kuwa Waziri alitumia madaraka yake ambayo kapewa na Serikali na Katiba ambayo yanampa uwezo wa kufanya maamuzi kama aliyofanya Karamagi.
Tulipopiga kelele kuhusu kitendo cha Karamagi, tukaja baini kuwa kelele zetu ni bure kwa kuwa kwa mujibu wa Katiba na mamlaka ya Waziri wa madini(kama Ngeleja alivyosema hivi karibuni), Waziri ana uamuzi binafsi bila kumshirikisha mtu kuamua ni jinsi gani mkataba uwe, mwekezaji apewe misamaha ya kodi na ushuru hata kuongeza muda wa mkataba.
Walichofanya Mramba na Yona hakina tofauti na alichofanya Kikwete akiwa Waziri wa madini. Yeye Kikwete ndiye katika utawala wake, na ile jazba ya Serikali kuchochea Uwekezaji, alitoa kibali na kukabidhi umiliki wa ardhi yote yenye dhahabu kwa Sinclair. Leo hii mtu yeyote anayetaka kuchimba madini, lazima amuone Sinclair, alipe ada kisha apewe ruhusa ya kufanya survey na uchimbaji.
Serikali ya Tanzania inaambulia 3% ya ,malipo ambayo mwekezaji huyu kamlipa Sinclair. Je swali ni hili, ni nani alimpa mamlaka Kikwete ya kuingia makataba na Sinclair wa kutupa mapato duni kiasi hicho? Ikiwa TanRange au ndio Tanganyika Royalty kampuni ya Sinclair ina pata faida marudufu, je si ni halali kabisa kumfungulia mashitaka Kikwete na mawaziri wengine wote ambao walitumia madaraka yao kushinikiza uwekezaji na kukubali mikataba ambayo inaipunja Serikali na zaidi kutumia kichocheo cha msamaha wa kodi?
Ndio maana nauliza haya mazingaombwe ni mpaka lini? Yona na Mramba hawatafungwa, kama Kiula wataachiwa huru kesi ikimalizika, kwa kuwa itabainika kuwa maamuzi yao hayakuwa na dhamira ya kufanya kosa la jinai au kuhujumu.
La pili, jiulize, kama kosa lao kina Mramba, Yona na hata Jeetu Patel, Lukaza na Mwakosya wa BOT ni makosa ya kuhujumu uchumi kwa mijibu wa sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 1964 ambayo bado inatumika (reference kesi ya Mahalu), je ni mamlaka gani mahakama ndogo kama ya Kisutu iliyonayo kusikiliza kesi hizi? Kwa nini hazikupelekwa Mahakama Kuu ambako kwa mujibu wa Sheria ndipo kesi hizi zilipaswa zisikilizwe?
Ni kwanini kwa Ukihiyo wangu wa masuala ya Sheria na Katiba, naona mianya mingi ambayo inaonyesha udhaifu mkubwa wa kesi hizi na kukosekana kwa umakini kutoka kwa TAKUKURU, DPP na AG?
Kwa nini kesi hizi zinanikumbusha kesi za Vhalambia na hata ile ya Tanesco na IPTL kule London?
Hivyo basi, kwangu ni changa kali nami nimelivalia miwani ya mwogeleaji Michael Phelps!