Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
- Thread starter
-
- #81
Kuna mfano mmoja nilitoa kuwa inasemekana kuwa watu wa Ulaya wanapenda sana process (how you do things). Kwa upande mwingine waMarekani wanapenda results (How you accomplish things).
Attitudes hizi kwetu hatuna. Tunapenda tu kuzungumza big things and big Ideas.
Kwa kweli watz tuna matatizo sana na sijui nini hasa nia yetu. Tumelalamika sana juu ya ufisadi na mafisadi, leo JK amefanya kweli, tumeanza kuponda mara wengine ajiuzuru, na hoja zingine nyingi za kumkatisha tamaa.
Tumuungeni mkono Rais ili afanikishe zoezi hili, akishindwa yeye tumeshindwa wa tz
Sober,
Nikipima na kusoma kilichofanyika na hata "nia" ya kufikisha Mramba, Yona, Patel na Lukaza, natatizwa na lilelinalojionesha kwangu kuwa hawa wamepelekwa mahakamani si kwa nia au madhumuni ya kweli kuwa wachukuliwe hatua, bali ni kutokana na mashinikizo na sababunyingine za kufanya kuonekane kuwa sasa Serikali inafanya kazi yake.
Tumeshajiuliza sana hapa kuhusu suala la EPA kuwa Deloitte and Touche walifanya audit, wakatoa ripoti moja mbaya sana kuhusu BOT. Ripoti hiyo, hata Utoah ambaye ni mdhibiti na mkaguzu mkuu wa Serikali aliafikiana nayo na kutoa tathmini kuwa BOT imefanya kwa makusudi au kwa uzembe wa kupindukia kuruhusu hujuma za EPA.
Dr. Slaa akatoa kauli bungeni na sis tukapiga kelele, lakini Serikali yetu kwanza ikatoa kauli kukanusha kuwepo hujuma kubwa kama hiyo. Ni mpaka pale mabalozi wa nchi tajiri walipoanza kupiga kelele wakiongozwa na Mark Green wa USA, yule jamaa wa Neatherlands, Norway na Ujerumani na mpaka nchi moja wafadhili walipotoa kitisho kusitisha misaada (unakumbuka Membe alvyojibu kwa kiburi kuwa sisi ni nchi huru tusiingiliwe?) ndipo taratibu Serikali na Bunge la CCM likakubali kuna tatizo nao wakaipa kazi ya uchunguzi kampuni ya Earnst and Young.
Kina E&Y wakaja na majibu yale yale ya Deloitte Touche na Utoah, wakawasilisha serikalini. Rais na Serikali, wakaundia tume chini ya IGP, DPP, AG na Takukuru ambao walikuwa wanalipwa laki moja kwa siku. Kamati hii teule, ikapewa muda, nayo ikashindwa kumaliza uchunguzi ikabidi iombe iongezewe muda.
Kamati ilipomaliza utafiti na uchunguzi wake, ikawasilisha ripoti ikulu na kusema inasubiri uamuzi wa Rais.
Wabunge wakahoji, ripoti iko wapi? Ikulu ikasukuma ripoti kwa Sitta na wabunge watoe maamuzi, Bunge likajivua jukumu hilo, hivyo faili likarudi Ikulu.
Sasa wakati wa danadana hizi, Mama Killango akatoa kauli hapendwi mtu, wakaja kina Serukamba, Kisumo na Kingung'e kutoa kauli kali na chafu na kudai kuwa hakuna la msingi kuhusu EPA. Zaidi, CCM ikabadilisha kibao na kuanza kuhodhi sakata lote la EPA kwa kudai kuwa eti, wao ndio walioliibua na si mtu mwingine.
Wakati E&Y wanafanya uchunguzi wao, Manumba ambaye ni DCI alitoa kauli kuwa wao Polisi hawawezi kuanza kufanya uchunguzi wowote mpaka E & Y wamalize uchunguzi wao.
Sasa najiuliza, ikiwa karibu miezi 18 tumekuwa tukiimba EPA, EPA, EPA na kwanza Serikali na Waziri wake Meghji wakakanusha hakuna wizi au hujuma, Manumba akasema anasubiri Ikulu impe maelekezo ya nini cha kufanya, unategemea kufikishwa kwa hawa jamaa Mahakamani kutanipa furaha zaidi ya kuhoji kwa kuangalia mashitaka waliyosomewa?
Zakumi anadai kuwa ni heri basi tuwafunge hata kwa hayo makosa madogo madogo, je hiyo ndiyo suluhisho na njia ya kuhakikisha kuwa hakuna tena uhujumu?
Sasa hivi, minong'oni ni kuwa ili CCM ishinde kwa kishindo, inabidi suala la EPA na ufisadi yapatiwe japo namna ya kufanana na ufumbuzi. Zaidi ni ukweli kuwa wahisani wamesema hawatoi pesa zao kusaidia bajeti yetu mpaka kieleweke.
Sasa kwa nini mnamkasirikia au kufadhaishwa na Mchungaji anaposema kuwa hili ni changa na hakuna nia ya kweli kutafuta ufumbuzi?
Ama nikupeni mfano mwingine. Lowassa, Karamagi, Chenge na Msabaha. Hawa walifanya uzembe na wanatuhumiwa kuwa wamekula mlungula. Lakini baada ya wao kujitoa kwenye madaraka, hata ndaniya CCM yenyewe hawajachukuliwa hatua, hawajapewa karipio badala yake wanafanywa ni wafalme, wamepewa maandamano kuwapokea, bado wananyenyekewa ndani ya chama na v=hivyo kuonyesha umma kuwa wao wana nguvu na Serikali haina nguvu.
Ni mpaka pale matatizo yetu yatakapotatuliwa kwa nia ya kweli na usahihi wa kutatua, ndipo nitapata faraja. kinyume na hapo, ni changa mbalo nimelivalia miwani.
- Mzizi wa fitina kukatwa next week kati ya Jumanne na Jumatano, confirmed!
Kikwete and all the comapany wanaweza kuwa wazuri tu...! But kama haku-analyse the whole issue critically linaweza likawapelekea kusipo. that is why we ask them or anybody...kama kuna critical analysis iliyofanywa..ilwekwe hadharani sio vibaya tukishare. Na sio kufikirikwamba we are negative to what is happening.
Tusione aibu kutaka kujua mfumo unaotumika tangu kuanza kwa awamu ya nnne.
Umabadilika? and why?
Ni uleule?..kama ni hivyo tulikosea kuutizama?
Kama ni uleule na ulitegemewa kuyaleta haya yanayotokea sasa sawa...Lakini tudhibitishiwe!
Inawezakana kabisa ...We had a wrong perception na serekali ya awamu ya nne. Nakama ni hivyo sindio tunataka uchambuzi.
Personaly i really love what is happening! but also I should not be terrified to question it criticaly.
- Again ninaomba ksuema kuwa tuko kwenye the right track, na huu ni wakati wa kumpa rais ushirikiano wetu, na hasa ningetegemea kuwaona upinzani waki -take charge, maana huu ndio hasa wakati wao, pale tunapoambiwa hakuna ushahidi wao ndio wanaopaswa kujitokeza na ushahidi mzito, maana sisi wananchi walipa kodi tunawalipa ruzuku kila mwezi, sasa tunawalipa ruzuku for what kama sio watusaidie wka mambo kama haya?
- Kuendelea kumlaumu rais after all this kwa kweli sioni kama ni productive, kwa sababu rais anatakiwa afanye nini zaidi ya haya aliyokwisha fanya tayari? Amefungua mlango sasa sisi wananchi tu-take a charge na pia tu-take advantage, Mramba na Yona wako rumande sio kwa sababu ya kushindwa dhamana, isipokuwa ni kuthibitisha kwamba wahusika wa ushitaki wako serious, binafsi ninataka kutoa pongezi nzito sana kwa rais na wahusika wote wa hii operation, na ningependa kuwapa moyo kwamba baadhi yetu wananchi tuko nyuma yao na tuko tayari kuwapa msaaada ikibidi, lakini nasema hvi rais amefanya ya kwake, sasa ni zamu yetu wananchi kumalizia na hasa ninategemea Upinzani kutuongoza hapa, maana ndio hasa sababu ya kuwapa ruzuku.
Ahsante Rev!
Mkulu Kishoka,
Heshima mbele bro, kwa kweli kinachoendelea so far ni mapema mno kusema wazi kwamba exactly ni nini hasa, between sheria na siasa, lakini:-
1. Wananchi wa Tanzania, tumeonewa vya kutosha na tumenyanyaswa na viongozi hasa wezi kwa muda mrefu sana, wakati wa Sokoine na uhujumu uchumi tumeona dagaa wakiswekwa lupango, huku papa wakiendelea kunawiri na kutucheka, tunasikia Sokoine alitaka kufanya kweli lakini Mwalimu alikataa kabisa, sasa this time is for real tunaona papa wakiswekwa lupango.
- Sokoine alikuwa tayari ana list ya viongozi wa juu mawaziri wakiwemo aliotaka wakamatwe, kwa kuhujumu uchumi na pia alimuhakikishia Mwalimu kwamba ana ushahidi wa kutosha, kati ya viongozi hao walikwemo Barongo, na Kahama, katika kutayarisha ushahidi wake Sokoine alishikirikiana sana na Kaisi, na Kolimba. Lakini Mwalimu alipokataa wasishikwe, Kaisi ambaye sasa alikuwa RC Bukoba was so upset kwamba akaamua kwa hasira kumuweka ndani Barongo alipofika Bukoba, na hata Kahama pia lakini Mwalimu akamlazimisha kumuacha haraka sana the minute alipojaribu kule Bukoba uwanja wa ndege, wakati sir George anashuka kutoka Dar. Kina balozi Magombe wamefanya mambo ya aibu sana huko majuu, kina Maryogo na wengine wengi sana, lakini ninampa heshima rais kwa kuimaliza hii tabia ya kulindana kwa viongozi, rais ameweka mfano sasa ni wajibu wetu wananchi ku-take it form there!
Ahsante Rev!
Nimefurahi kusikia wanaowashtaki Mramba na Yona si Kikwete ila serikali, na wanafanya kazi pale Kikwete anapotoa go ahead!
So hatuna serikali, ila mpaka iambiwe na Kikwete!!!!!
hapa kutakuwa na uonevu, kuwa wezi fulani waende na wengine wasiende
Kwa hiyo mwizi yeyote awe raiskwa sababu hatuna imani na atakayekuja!
Yaani katika watanzania milioni 40, we can not trust someone to lead us???
ina maana una confirm jamii ya watanzania ni fisadi wote, so siyo kosa kabisa Kikwete kuwa rais hata kama naye aliingia mikataba mibovu na kuua watu!!
Inabidi tuwe clean, siyo kusema huyu afadhali msafi kuliko huyu?? kichekesho hiki.
Mchakato mzima wa kumpata rais Tanzania ni kichekesho kwenye vyama vyetu, wanampata ka presha za muda huo na sio nini alifanya siku za nyuma.
UKIFIKA WAKATI UKAONA KIKWETE ANAFAA KWA URAIS NA UKAONA HAKUNA WA KUM-REPLACE BASI FORGET CCM WILL RULE FOREVER!!!!!!
Mkuu Field Marshall,
Mwalimu alikokusea nini, ama aliwakosea nini ancestors wako? Katika postings zako naona unapopata mwanya lazima uchomekee lawama kwa Mwalimu! Let the old man rest in Eternal Peace, Amen. Kalifanyia makubwa Taifa hili, makubwa ambayo wala hayawezi kulinganishwa na si rahisi kufutwa.
Naelewa unajua mengi ama umesimuliwa mengi kutokana na sources zako, lakini I think it is uncalled for kutumia informations ulizonazo kuchafua majina ya wazee waliolitumikia taifa hili ambao wala hatuoni mijimali waliyojilimbikizia kwa kutoshitakiwa na Mwalimu!
Let's be realistic, Barongo, Sir George na Mzee Maryogo ndio 'papa' walioachiwa kuendelea kunawiri na kuwachekeni?! Mzee Barongo, kama sikosei, ni marehemu na kafa maskini baada ya kulitumikia taifa hili kwa uwezo wake wote pamoja na elimu duni aliyokuwanayo. Tumeishasahau jinsi alivyokuwa akihamasisha Kilimo Bora? Sioni sababu ya msingi ya kuwataja na kuwachafua wazee hawa ambao walijitolea kulitumikia taifa letu kabla na baada ya Uhuru na hawakutumia nafasi zao kujilimbikizia mijimali. Wapo waliotamani, lakini tamaa zao hazikuweza kutimia kutokana na udhibiti na jicho kali la Mwalimu.
Nimetoa tabasamu kubwa kusoma jina la Kaisi! Nsa ni mwanajeshi, huenda alitumia taaluma yake bila utaratibu!
Awamu ya Kwanza kulikuwa na uozo gani mkubwa sana uliotendeka wa kuweza kulinganishwa na haya tuliyoyashuhudia ndani ya awamu zilizopita na tunayoyashuhudia hivi sasa, tunayojadili? Mind you, UTU aliokuwanao Mwalimu ulimfanya awe makini sana alipopelekewa tuhuma dhidi ya kiongozi ama mtu yeyote yule. Hakupenda kumuonea mtu. Kabla hajatoa uamuzi wa jambo lolote zito, alikuwa mwepesi kufanya utafiti wake binafsi kwa kuwatumia watu mbalimbali na kwa kupata mawazo ya watu makini walioaminika, wakiwemo viongozi wenziwe, nje ya mfumo. Kutokana na taarifa alizopata, aliweza pia kuwajua wafitini wa wakati huo. Kama alimwambia Kaisi awaachie aliowakamata, alikuwa na uhakika hao hawakuwa wahujumu uchumi wa wakati huo.
Mwalimu alimheshimu sana Sokoine na kuithamini sana kazi nzuri aliyokuwa akiifanya kuhusu uhujumu uchumi. Tusisahau kwamba hapa tunazungumzia Rais na Waziri Mkuu wake. Kabla ya Sokoine (Waziri Mkuu) kuchukua hatua yoyote ya aina hiyo lazima alishauriana na kukubaliana na (Rais) Mwalimu. Kwa maana hiyo, suala la kuwashughulikia wahujumu uchumi halikuwa la Waziri Mkuu pekee. Nashindwa kupata picha ya Sokoine kunung'unika pembeni kwamba alitaka Barongo na Sir George wakamatwe lakini Mwalimu amekataa bila sababu! Sokoine hakuwa mnafiki!
And, Mzee Maryogo of all the people! FEMS, huyu mzee atakufa maskini kwa sababu ya uadilifu wake. Pia atakufa maskini kwa sababu yeye ni 'maskini jeuri', neno kujipendekeza halimo kwenye vocabulary ya mzee Maryogo! Alipokuwa Utalii, aliweza kuokoa mamilioni ya fedha za Serikali kwa kumpelekea Mwalimu taarifa za kufichua njama za uhujumu. Ah! na marehemu Magombe naye alikuwa 'papa' wa uhujumu?!
Tuwasifie ma-Rais wetu na viongozi wa awamu zilizopita, awamu ya sasa na awamu zijazo kwa hatua wanazochukua kwa manufaa ya taifa letu. Mazingira ya miaka 40 iliyopita hayawezi kamwe kufanana na ya juzi, jana, leo, ama kesho. Tutakuwa hatumtendei haki Mwalimu aliyejitahidi kwa akili zake zote, kwa nguvu zake zote na kwa uwezo wake wote kutuwekea misingi bora ya uadilifu, tukaibomoa wenyewe.
FEMS, no hard feelings, ni kujaribu kukupunguza munkari dhidi ya Mwalimu na marehemu wengine!
Mkuu Field Marshall,
Mwalimu alikokusea nini, ama aliwakosea nini ancestors wako? Katika postings zako naona unapopata mwanya lazima uchomekee lawama kwa Mwalimu! Let the old man rest in Eternal Peace, Amen. Kalifanyia makubwa Taifa hili, makubwa ambayo wala hayawezi kulinganishwa na si rahisi kufutwa.
Naelewa unajua mengi ama umesimuliwa mengi kutokana na sources zako, lakini I think it is uncalled for kutumia informations ulizonazo kuchafua majina ya wazee waliolitumikia taifa hili ambao wala hatuoni mijimali waliyojilimbikizia kwa kutoshitakiwa na Mwalimu!
Let's be realistic, Barongo, Sir George na Mzee Maryogo ndio 'papa' walioachiwa kuendelea kunawiri na kuwachekeni?! Mzee Barongo, kama sikosei, ni marehemu na kafa maskini baada ya kulitumikia taifa hili kwa uwezo wake wote pamoja na elimu duni aliyokuwanayo. Tumeishasahau jinsi alivyokuwa akihamasisha Kilimo Bora? Sioni sababu ya msingi ya kuwataja na kuwachafua wazee hawa ambao walijitolea kulitumikia taifa letu kabla na baada ya Uhuru na hawakutumia nafasi zao kujilimbikizia mijimali. Wapo waliotamani, lakini tamaa zao hazikuweza kutimia kutokana na udhibiti na jicho kali la Mwalimu.
Nimetoa tabasamu kubwa kusoma jina la Kaisi! Nsa ni mwanajeshi, huenda alitumia taaluma yake bila utaratibu!
Awamu ya Kwanza kulikuwa na uozo gani mkubwa sana uliotendeka wa kuweza kulinganishwa na haya tuliyoyashuhudia ndani ya awamu zilizopita na tunayoyashuhudia hivi sasa, tunayojadili? Mind you, UTU aliokuwanao Mwalimu ulimfanya awe makini sana alipopelekewa tuhuma dhidi ya kiongozi ama mtu yeyote yule. Hakupenda kumuonea mtu. Kabla hajatoa uamuzi wa jambo lolote zito, alikuwa mwepesi kufanya utafiti wake binafsi kwa kuwatumia watu mbalimbali na kwa kupata mawazo ya watu makini walioaminika, wakiwemo viongozi wenziwe, nje ya mfumo. Kutokana na taarifa alizopata, aliweza pia kuwajua wafitini wa wakati huo. Kama alimwambia Kaisi awaachie aliowakamata, alikuwa na uhakika hao hawakuwa ‘wahujumu' uchumi wa wakati huo.
Mwalimu alimheshimu sana Sokoine na kuithamini sana kazi nzuri aliyokuwa akiifanya kuhusu uhujumu uchumi. Tusisahau kwamba hapa tunazungumzia Rais na Waziri Mkuu wake. Kabla ya Sokoine (Waziri Mkuu) kuchukua hatua yoyote ya aina hiyo lazima alishauriana na kukubaliana na (Rais) Mwalimu. Kwa maana hiyo, suala la kuwashughulikia wahujumu uchumi halikuwa la Waziri Mkuu pekee. Nashindwa kupata picha ya Sokoine kunung'unika pembeni kwamba alitaka Barongo na Sir George wakamatwe lakini Mwalimu amekataa bila sababu! Sokoine hakuwa mnafiki!
And, Mzee Maryogo of all the people! FEMS, huyu mzee atakufa maskini kwa sababu ya uadilifu wake. Pia atakufa maskini kwa sababu yeye ni 'maskini jeuri', neno ‘kujipendekeza' halimo kwenye vocabulary ya mzee Maryogo! Alipokuwa Utalii, aliweza kuokoa mamilioni ya fedha za Serikali kwa kumpelekea Mwalimu taarifa za kufichua njama za uhujumu. Ah! na marehemu Magombe naye alikuwa 'papa' wa uhujumu?!
Tuwasifie ma-Rais wetu na viongozi wa awamu zilizopita, awamu ya sasa na awamu zijazo kwa hatua wanazochukua kwa manufaa ya taifa letu. Mazingira ya miaka 40 iliyopita hayawezi kamwe kufanana na ya juzi, jana, leo, ama kesho. Tutakuwa hatumtendei haki Mwalimu aliyejitahidi kwa akili zake zote, kwa nguvu zake zote na kwa uwezo wake wote kutuwekea misingi bora ya uadilifu, tukaibomoa wenyewe.
FEMS, no hard feelings, ni kujaribu kukupunguza munkari dhidi ya Mwalimu na marehemu wengine!
Heri said:Tangu baada ya Yona na Mramba kushtakiwa kwa kosa la "Abuse of Power na kusababisha loss of 11 billion shilingi kwa Taifa" , nadhani itakuwa ni muda muafaka kujadlili Abuse of Power ni nini. Ni nani ni wahusika ? Kama wataalam wa wizara walimshauri Waziri wao nao hawahusiki? Je Mawaziri wana uwezo wa kuingia Mkataba wowote bila ridhaa ya Rais au Baraza la Mwaziri? Je
Kitendo cha Hakimu Henzeron ni mfano wa Abuse of Power?
UKAGUZI WA MAJENGO BENKI KUU NI USANII MWINGINE
Sasa hapo jameni kuna ukweli kuhusu stori ya mwandishi wa Nipashe ya jumapili. Hizi ni kampuni za kimataifa za kukagua mahesabu ya ujenzi kweli? Makao makuu ya MEKON yako uchochoroni kijitonyama nyumba ya kupanga hii kampuni na bwana Mkony wanababe wa kukagua Benki kuu kweli. Kipato chao kidogo kabisa, wanawezaje kuwa independent wakati total income yao ni kiduchu na wanataka kukagua benki kuu yenye mabilioni, je code of ethics za Engineers zinakubali hali kama hiyo?
Watakuwa prone for intimidation kani consulting fee toka Benki kuu kwa kazi hiyo ni kubwa mno.
Benki kuu/Gavana kaamua kuchagua kijikampuni kilicho very local, wenyekukimiliki wako hoi kwa poverty wakikimbiza vijitenda vya ujenzi hapa na pale. Kwa makusudi Gavana anataka aweze kuwacontrol. Kwani wamejifunza baada ya kuajiri makampuni ya kimataifa yanakuwa ngangari na kuwashikia bango.