Paukwa... Pakawa!

Paukwa... Pakawa!

Rev. Kishoka,
Dr. Hussein Mwinyi ana nyumba zake kadhaa na moja iko pale Mlalakua kapangisha watu wa VETA na anakusanya si chini ya $4000.00 kwa mwezi!Jiulize mshahara wake kwa mwezi ni kiasi gani na tunaambiwa ana nyumba nne kapangisha wazungu na ma-TX?

Kibaya zaidi ni kwamba halipi kodi ya mapato hayo na huwezi kuulizia utapoteza maisha!.. Hii ndio Tanzania aliyoijenga Mkapa, kusifiwa kuhusu utaratibu wa kukusanya kodi..
Viongozi wote wana majumba na imekuwa biashara kubwa sana sasa hivi tena wengine wanapangisha nyumba za Msajili wakipokea kifungua kinywa dollar 30,000 (upewe ufunguo)...
 
Mkandara naomba kufanya masahihisho, hiyo $4000.00 ni kwa nyumba moja! sasa nyumba nne ni $16000! Mshahara wake karibu wa mwaka mzima!
 
Siasa (politics) na biashara(business) ni vitu hatari katika taaluma (profession) ya utumishi wa umma (public service) - ukivichanganya unaleta mianya ya kuifanya rushwa (corruption) na ubadhirifu (embezzlement) viwe nyemelezi. Ukisoma maadili ya utumishi wa umma Tanzania na Sheria za Utumishi wa Umma utaona zina mianya mingi ya kuchanganya siasa na biashara kwenye taaluma/kazi ya utumishi. Hivi vyote shurti vitenganishwe ili watumishi wa umma watumikie wananchi kwa uadilifu na usawa bila kujali utashi wa kisiasa na ushawishi wa kibiashara. Huu mwongozo unahitajika katika nchi ya Kijamaa kama unavyohitajika katika nchi ya Kibepari. Lila na Fila havitangamani.

Hii ndio Historia ya Mwongozo:

1. Wakoloni waliuleta katika miaka ya mwisho ya 1950 tulipokaribia kupata uhuru
2. Viongozi wa Tanganyika huru wakauzika kwenye miaka ya mwanzoni ya 1960
3. Wananchi wakaurejesha kwenye miaka ya mwisho ya 1960 kuwadhibiti wabenzi
4. Vigogo wakautupilia mbali kwenye miaka ya mwanzo ya 1990 ili wafanye ufisadi
5. Wazalendo wanaurudisha kwenye miaka ya mwisho ya 2000 kuinusuru Tanzania
 
Zakumi,
..
Exactly!.. Azimio la Arusha lilikuwa na mabaya yake ambayo ndiyo yalitakiwa kurekebishwa na Azimio la Zanzibar lakini badala yake kilichobadilishwa ni Ethics za Uongozi.. Kumbuka kwamba tuliacha Siasa za Ujamaa July 1984 siku mwalimu alipotangaza kushindwa kwa Ujamaa hivyo kuacha milango wazi ya Biashara..
Toka siku hiyo policy ya open market ilikutumika na mabaya tuliyoyajua sisi ndio ulikuwa mwisho wake...Mwaka 1992 - miaka minane baadaye (kama sikosei) ndipo Mwinyi alipotangaza Azimio la Zanzibar hiyo - RUKSA..na hakuna jambo lolote lililokuwa geni ktk Uchumi isipokuwa nafasi ya viongozi wetu kujihusisha na biashara. Kwa hiyo Azimio la Zanzibar lilikuja kuvunja miiko ya Uongozi. Uongozi wa Mwinyi unatia Kichefuchefu kiuchumi toka hilo Azimio lilipotangazwa, machafu yote utayakuta baada ya Azimio hilo..
Hivyo mkuu, unapolipigia debe Azimio la Zanzibar ni sawa na kupingana na maneno ya mwalimu uliyoyaandika hapo juu..Hakuna kati yetu anayesema Azimio la Arusdha lilikuwa bomba kichizi isipokuwa pale tunapogusia swala la Uongozi bora na ndilo tatizo kubwa la Tanzania. Mara nyingi tumeshindwa kutafuta kiini cha matatizo yetu badala yake tuna laumu watu na sio policy iliyoshinikiza.
Ukitazama ukumbi wa siasa utaona karibu mada zote zinahusiana na Uongozi bora na kwa bahati mbaya tumeshindwa kuelewa kwamba yote haya yametokana na kuvunjika kwa hiyo miiko ya Uongozi. Ni hilo Azimio la Zanzibar lilompa uwezo Mkapa, Mramba, Yona, Karume, na wengine wote kufanya waliyoyafanya kwa sababu ilikuwa ruksa kufanya biashara ama kwa lugha inayoendana na Uongozi nitasema KUJITAJIRISHA...

Hakuna ethics za Uongozi ambazo zinaambatana na sheria zinazowapa uhuru Viongozi kufanya biashara. Ni sawa na Padre unayemruhusu kufunga ndoa lakini anakatazwa kutongoza mwanamke au mwanafunzi wake... unafikiri huyo mke atampata vipi?..

Ethics za Uongozi ni lazima ziambatane na sheria zinazokataza hata kukaribia kufanya maovu, Wala Takribun - waarabu wanasema..Hata katika mashirika ya kawaida huwezi kumwona CEO wa shirika moja la Simu akiruhusiwa kufungua kampuni yake ndogo ya simu na ukategemea hataifanya kazi ya shirika hilo vizuri..Acha hilo huku Ulaya kuna mashirika hata ndugu yako huruhusiwi kuwajiri ukisha kuwa na wadhifa fulani...
Ukimwacha Lowassa anunue hisa ya kumiliki Celtel unategemea atafanya nini zaidi ya kuhakikisha anaua Ushindani, anaweka masharti rahisi na pengine kodi ndogo ktk shirika hilo..
Hata ukitazama matatizo ya nyumba na viwanda.. Kinachotuumiza wengi sio ununuzi wa viwanda hivyo ama fedha njugu walizolipa isipokuwa ni ile ruksa ya hao viongozi kujipanga na kuzichukua.. hakuna mtu ambaye atajipangia bei kubwa ama masharti magumu lakini kama hawa viongozi wangekuwa hawaruhusiwi ungeona tofauti ya bei na tender za Ukweli zikitumika..UWAZI ungekuwepo kwani hakuna mtu angetaka kuonekana kauza kitu kwa hasara...Mkapa kaichukua Kiwira kwa sababu alikuwa rais hakuna sababu nyingine..Ni hivyo hivyo kwa viongozi wote wamegawana mali zetu chini ya uhuru waliopewa na sasa hivi tumeganda hatujui la kufanya.. Kisheria walilipa thamani ya viwanda hivyo hata kama ilichorwa, lakini walilipa hawakuiba wala kunyang'anya, hivyo sio wao waliovunja sheria isipokuwa sheria zenyewe ndizo zilikuwa mbovu.. tazama maswala ya madini hata Waziri mkuu wa Canada alishangaa kusikia tumefungiwa kanyaboya na Barricks kiasi kile, na kashidnwa kutusaidia kwa sababu tuliingia mkataba kisheria.. Mkapa kaondoka na asilimia zake 10 ambazo huweiz kuziona zinaingia direct ktk sahani lake...

Mkandara:

You are so rigid. Jamii ni lazima ifanye experiments. Je kwenye mkutano wa Azimio la Zanzibar, wajumbe walikuwa migodi ya makaa ya mawe, majumba ya kupangisha au walifikiri kuwa one day mfumo wa vyama vingi utakuwepo Tanzania.

Walifanya hayo yote kulingana na mazingira ya wakati huo (period). Na mmoja wa architecture wa Azimio la Zanzibar Horace Kolimba unajua yaliompata.

Kwa maoni yangu mimi Azimio la Arusha is so pre-historic. Haki ya kushika madaraka ya uongozi ni haki ya kiraia kwa kila mwananchi wa Tanzania. Awe masikini, mfanyabiashara, prof wa university au mkulima.

Azimio la Arusha lilifanya nchi iwe na career politicians ambao hawajui kingine zaidi ya siasa.

Kwa mfano mimi ni meneja wa MacDonald Rest. Najua supply chain, najua msimu wa kupata mapato. Najua ni kipindi gani nipunguze wafanyakazi. Najua ni wakati gani nivae magwanda na kupiga mzigo kama waiter.

Uzoevu wangu wa kazi ni adimu kwa mameneja wengi wa biashara hotel na migahawa Tanzania. Je nikiwa na biashara ya hotel Tanzania, utanikataza nisijiingize kwenye uongozi wa kisiasa kwa sababu mimi ni mfanya biashara?

Na unaponikataza mimi si utakuwa umekiuka haki zangu za kiraia. Na unapokataa watu wenye mafanikio, alternative unayobakiwa haitakukuakishia kukupa mafanikio.

Mkapa kaingia Ikulu masikini katoka akiwa tajiri mwenye mgodi uliopo Tanzania. Kungekuwepo na Azimio la Arusha angeingia Ikulu masikini na kutoka madarakani akiwa tajiri mwenye akaunti iliyo Uswiss au kutumia pesa alizoiba kwenye ulevi. Kipi bora hapo?
 
Mkandara naomba kufanya masahihisho, hiyo $4000.00 ni kwa nyumba moja! sasa nyumba nne ni $16000! Mshahara wake karibu wa mwaka mzima!

Sasa kwanini mafanikio yake yamnyime nafasi ya yeye kuwa kiongozi. Katika mjadala huu mnashindwa kuonyesha ni jinsi gani kiongozi masikini anaweza kuwa na ethics za uongozi na Kiongozi mwenye kufanya biashara akashindwa kuwa na ethics.

Nyerere hakuwa masikini, alikuwa mtoto wa chifu. Alikuwa na mifugo kwa, Mkulima na Mwandishi wa vitabu. Lakini alikuwa na ethics za uongozi.
 
Siasa (politics) na biashara(business) ni vitu hatari katika taaluma (profession) ya utumishi wa umma (public service) - ukivichanganya unaleta mianya ya kuifanya rushwa (corruption) na ubadhirifu (embezzlement) viwe nyemelezi. Ukisoma maadili ya utumishi wa umma Tanzania na Sheria za Utumishi wa Umma utaona zina mianya mingi ya kuchanganya siasa na biashara kwenye taaluma/kazi ya utumishi. Hivi vyote shurti vitenganishwe ili watumishi wa umma watumikie wananchi kwa uadilifu na usawa bila kujali utashi wa kisiasa na ushawishi wa kibiashara. Huu mwongozo unahitajika katika nchi ya Kijamaa kama unavyohitajika katika nchi ya Kibepari. Lila na Fila havitangamani.

Hii ndio Historia ya Mwongozo:

1. Wakoloni waliuleta katika miaka ya mwisho ya 1950 tulipokaribia kupata uhuru
2. Viongozi wa Tanganyika huru wakauzika kwenye miaka ya mwanzoni ya 1960
3. Wananchi wakaurejesha kwenye miaka ya mwisho ya 1960 kuwadhibiti wabenzi
4. Vigogo wakautupilia mbali kwenye miaka ya mwanzo ya 1990 ili wafanye ufisadi
5. Wazalendo wanaurudisha kwenye miaka ya mwisho ya 2000 kuinusuru Tanzania

Kijana ujachoka tu na mapinduzi.
 
Zakumi,

Umetunyooshea kidole kwa kuchanganya mambo, lakini naona nawe umessahau kitu kimoja ambacho nimekikumbuka bada ya kusoma maoni ya Kisumo kwenye gazeti la Rai.

CCM ni chama cha kijamaa na kimejijenga kwa kanuni za ujamaa. CCM bado inapiga baragumu la ujamaa na kujitegemea kwa wananchi na wanachama. Iweje viongozi wawe mabepari?

Mfano huo wa Dr. Mwinyi, inabidi ujiulize, yeye Dr. Mwinyi ni katika muda gani tangu aanze kazi ameweza kupata mshahara na malipo mengi ya kutosha kwa umri wake mdogo na kuweza kuwa na mali nyingi namna hiyo?

Si kuwa ni fisadi au kahujumu, lakini pindi inapokuwa kwamba kujipatia kwake mkopo, mali, nyumba na viwanja vimetokana na kuwa yeye ni nani kwa wasifu wa jina na mamlaka, huoni hapo kuna kasoro?

Let say wamempa mkopo in good faith ajianzishie mradi, sawa na ule mkopo wa ANBEN wa $500000, je ni lini Zakumi na Mchungaji wanaweza kupewa mikopo au kupata viwanja "in good faith" ili kuwe na usawa?

Sikatai mtu kuwa tajiri au kujihusisha na siasa, lakini kkwa nchi kama Tanzania ambayo bado wananchi wake wengi ni wanyonge wa fikra na mali, executive priviledge kwa wanasiasa hugeuka kuwa abuse na greed!
 
Nikirudi kwenye mada yenyewe ya upaukwa na upakawa, tunawaita Yona na Mramba Pwagu na Pwaguzi, lakini tuliwapa mamlaka kikatiba na kisheria kufanya maamuzi ambayo leo tunalalamika.

Adam Malima akimjibu Spika Sitta kuhusu mikataba, kasema kuwa mikataba ni siri ili mwekezaji alindwe.

Swali linakuja je Mtanzania ni nani anamlinda?

Karamagi alipokwenda Churchill hotel na kuangusha gumba kwenye Buzwagi II, alikuwa anatumia executive powers and priviledges kuingia mkataba. Sisi tumelipokea kama ni abuse of power na corruption kwa kuwa kwanza alikiuka tamko la wazi la Rais kusitisha mikataba ya madini na pili alifanya ni siri.

Lakini yeye Karamagi, kama vile Lowassa wanatumia kinga ya executive priviledge and powers. Sasa hii appearance ya abuse of power au corruption kama vile mwendesha mashtaka wa TAKUKURU na DPP wanavyotaka tuone kuhusiana na Yona na Mramba, itakuwa ni vigumu sana kwa Serikli kupata ushindi kwenye kesi hiyo.

Mbaya zaidi narudia kuwa Mramba alichofanya kiliandikwa na kuchapwa kwenye gazeti la Serikali kwa zaidi ya miaka mitano, swali ni kwa nini kama ilionekana kuna abuse of power mara ya kwanza tatizo hilo halikupatiwa ufumbuzi na utatuzi?

Tutasema kuwa alikuwa anaogopewa kama Waziri? kwa msingi upi? je Katiba inasema kuwa kiongozi analindwa na kufanyiwa upendeleo hata kuogopwa kwa kuwa kiongozi? au katiba inasema ni haki na ni lazima kulinda kila mtu kutoka na unyanyaswaji na uonevu?

Ndiyo maana Mchungaji anahoji mchakato mzima wa hawa jamaa kupelekwa mahakamani kwa kosa la "abuse of power' au maarufu kama matumizi mabaya ya madaraka.

Ni nani katika Serikali ya Tanzania na mashirika ya umma hajawahi kutumia madaraka vibaya? unapotumia gari la wizara kwenda kukata majani wa ng'ombe wako au kuchukua chakula cha kuku, hiyo ni abuse pf power na wastage of tax payers money and resources!
 
Zakumi,
Mkuu wangu _ Uongozi bora unakuja na mengi na ajabu sana kusoma huo mfano wako wa kiongozi mwenye Kihotel chake..
Huyu mtu akitaka kugombea Uongozi sio favour kwetu ni ajira ambayo ina masharti yake, wala hatufanyii hisani yoyote sisi isipokuwa ni yeye anaye OMBA kazi..
Unapozungumzia Uongozi wa Siasa mkuu mimi huko sipo, nachozungumziwa mimi sio Siasa kina Mbowe au mbunge yeyote wa CCM au vyama, isipokuwa mwajiriwa wa serikali ya Tanzania iwe Rais, makamu, mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, wateule wote ktk Taasisi za serikali na kadhalika ndio wanaotakiwa kutojihusisha na biashara nje ya kazi waliyopewa..Utawala wa serikali mkuu sio wanasiasa..

Mfano wako wa Hotel, kama Hicho kiHotel chako ni muhimu basi kataa madaraka ya kuongoza serikali endelea na hicho Kihotel ambacho unaona ni haki yako, lakini kuongoza nchi sio haki yako binafsi isipokuwa inatazamwa maslahi ya Taifa zima kwani nchi yetu haina mmiliki kama hiyo Hotel. Hivyo masharti ya kuongoza nchi hayatazami haki ya mtu binafsi..

Jambo jingine umezungumzia kuhusu Azimio la Arusha.. nitarudia kusema hakuna mtu anayepongeza kuendelea kuwa na Azimio la Aruusha wala hakuna ukweli kuwa Azimio la Zanzibar ni pinzani la Azimio la Arusha isipokuwa ni marekebisho ya sheria iliyowakataza viongozi kuwa wafanya biashara. Kwangu mimi Azimio la Arusha kwa upeo mkubwa lilikufa siku ile Mwalimu alipotangaza kushindwa kwa siasa za UJAMAA..
Hii ndio ilikuwa sehemu kubwa ya Azimio la Arusha ambayo wengi wetu tulikubali kuondoka kwake kwa sababu Kisiasa na Kiuchumi nchi yetu ilikuwa ikididimia...
Sasa huwezi kuingia Ubepari kwa kutazama hali na nafasi ya viongozi ktk mapato yao badala ya kuangalia mbinu za kiuchumi zinazoweza kutuondoa sisi ktk hali ile mbaya ya Kiuchumi..
Mafanikio yote yaliyopatikana wakati wa Mwinyi na Mkapa hayatokani na kuwezeshwa viongozi kufanya biashara wala mikopo ya World bank na mataifa mengine makubwa haikupatikana kwa sababu viongozi wetu waliruhusiwa kufanya biashara..isipokuwa ni mageuzi ya mfumo mzima wa Kiuchumi ambao uliwawezesha Wafanya biashara na sio viongozi wa nchi kumiliki mali zao. Uongozi wa serikali una miiko yake na uongozi wa biashara una miiko yake ktk kuepuka conflict of interest..
Mkuu wangu sasa kama wewe umesomea mambo ya Hotel na umefungua Hotel kweli utamruhusu mpishi au mhudumu wako afungue pia kiji hotel pembeni ya Hotel yako akidai kuwa ni haki yake?...
 
Zakumi,

Umetunyooshea kidole kwa kuchanganya mambo, lakini naona nawe umessahau kitu kimoja ambacho nimekikumbuka bada ya kusoma maoni ya Kisumo kwenye gazeti la Rai.

CCM ni chama cha kijamaa na kimejijenga kwa kanuni za ujamaa. CCM bado inapiga baragumu la ujamaa na kujitegemea kwa wananchi na wanachama. Iweje viongozi wawe mabepari?

Mfano huo wa Dr. Mwinyi, inabidi ujiulize, yeye Dr. Mwinyi ni katika muda gani tangu aanze kazi ameweza kupata mshahara na malipo mengi ya kutosha kwa umri wake mdogo na kuweza kuwa na mali nyingi namna hiyo?

Si kuwa ni fisadi au kahujumu, lakini pindi inapokuwa kwamba kujipatia kwake mkopo, mali, nyumba na viwanja vimetokana na kuwa yeye ni nani kwa wasifu wa jina na mamlaka, huoni hapo kuna kasoro?

Let say wamempa mkopo in good faith ajianzishie mradi, sawa na ule mkopo wa ANBEN wa $500000, je ni lini Zakumi na Mchungaji wanaweza kupewa mikopo au kupata viwanja "in good faith" ili kuwe na usawa?

Sikatai mtu kuwa tajiri au kujihusisha na siasa, lakini kkwa nchi kama Tanzania ambayo bado wananchi wake wengi ni wanyonge wa fikra na mali, executive priviledge kwa wanasiasa hugeuka kuwa abuse na greed!

Rev Kishoka:

Naomba fanya utafiti wa marupuru ya wabunge na ujue kuwa utajiri wengine tunawapa wenyewe. Sasa hizo pesa waziweke wapi?

Wakati vikao vya bunge vinafanyika DSM, walisema kuwa wabunge wana haki ya kulipwa posho ya kila siku (per diem) za kutosha kukaa kwenye hotel za kitalii. Na wengi tunaona wanaishi kwenye nyumba za kawaida tu wakati wa vikao vya bunge, je hizo pesa zao wanazipeleke wapi?

Hivyo kipindi cha Dr. Mwinyi yupo kama mbunge wa mkuranga na baba yake kama rais mstaafu alikuwa na uwezo wa kujenga hizo nyumba.

Dr. Mwinyi hawezi kuanza maisha kama mimi mtoto wa mkulima na hiyo ni fact.

Sio kwamba namtetea lakini kuna ukweli katika mbio za maisha kuna watakaoanza mita 10 kabla ya mstari wa kumaliza mbio. Na wengine wataanza mita mia moja. Wengine wataanza na viatu vya nike na wengine pekua.

Kuhusu mkopo wa ANBEN wa $500000. Hii kweli ni abuse. Lakini cha maana ni kukumbuka kuwa waanzilishi wa ANBEN, walikuwa ni masikini na waliojipatia pesa kwa kutumia nafasi zao. Na hii inakuonyesha dhahiri kuwa kiongozi masikini anaweza kuwa nambari one wa kukiuka maadili ya uongozi.
 
Nikirudi kwenye mada yenyewe ya upaukwa na upakawa, tunawaita Yona na Mramba Pwagu na Pwaguzi, lakini tuliwapa mamlaka kikatiba na kisheria kufanya maamuzi ambayo leo tunalalamika.

Adam Malima akimjibu Spika Sitta kuhusu mikataba, kasema kuwa mikataba ni siri ili mwekezaji alindwe.

Swali linakuja je Mtanzania ni nani anamlinda?

Karamagi alipokwenda Churchill hotel na kuangusha gumba kwenye Buzwagi II, alikuwa anatumia executive powers and priviledges kuingia mkataba. Sisi tumelipokea kama ni abuse of power na corruption kwa kuwa kwanza alikiuka tamko la wazi la Rais kusitisha mikataba ya madini na pili alifanya ni siri.

Lakini yeye Karamagi, kama vile Lowassa wanatumia kinga ya executive priviledge and powers. Sasa hii appearance ya abuse of power au corruption kama vile mwendesha mashtaka wa TAKUKURU na DPP wanavyotaka tuone kuhusiana na Yona na Mramba, itakuwa ni vigumu sana kwa Serikli kupata ushindi kwenye kesi hiyo.

Mbaya zaidi narudia kuwa Mramba alichofanya kiliandikwa na kuchapwa kwenye gazeti la Serikali kwa zaidi ya miaka mitano, swali ni kwa nini kama ilionekana kuna abuse of power mara ya kwanza tatizo hilo halikupatiwa ufumbuzi na utatuzi?

Tutasema kuwa alikuwa anaogopewa kama Waziri? kwa msingi upi? je Katiba inasema kuwa kiongozi analindwa na kufanyiwa upendeleo hata kuogopwa kwa kuwa kiongozi? au katiba inasema ni haki na ni lazima kulinda kila mtu kutoka na unyanyaswaji na uonevu?

Ndiyo maana Mchungaji anahoji mchakato mzima wa hawa jamaa kupelekwa mahakamani kwa kosa la "abuse of power' au maarufu kama matumizi mabaya ya madaraka.

Ni nani katika Serikali ya Tanzania na mashirika ya umma hajawahi kutumia madaraka vibaya? unapotumia gari la wizara kwenda kukata majani wa ng'ombe wako au kuchukua chakula cha kuku, hiyo ni abuse pf power na wastage of tax payers money and resources!

Rev Kishoka:

Now you are talking. Executive powers and priviledges zote za viongozi wa ngazi zote zinatungiwa sheria na bunge (period).

Na kwa mantiki hiyo hakuna sababu kumbebesha mizigo rais kuwa afanye hivi au vile wakati chombo muhimu cha kuleta mabadiliko kimelala.

Kwa mfano kuitwa kutoa ushahidi au maelezo katika bunge la Marekani ni sawa na kuitwa mahakama. Ukitoa ushahidi wa uongo au kufisha ushahidi utapelekwa jela. Hivyo mtu akiitwa congress kwenye uchunguzi anakwenda na mawakili kama vile anakwenda mahakamani.

Hile kamati ya Mwakyembe, ingekuwa ni Marekani ingewapeleka watu ndani.
 
Zakumi, Rev. Kishoka..
Wakuu maneno mazito lakini tunasahau kwamba nchi tunayoizungumzia hapa ni Tanzania..tuifikirie Tanzania kama Tanzania tunayoifahamu, nchi tajiri yenye raia maskini wa kutupa na siasa ndiyo njia pekee ya Utajiri au kwa lugha nyingine ku- gain POWER. Hakuna short cut zaidi ya kuwa baba yako alikuwa Tajiri na umebahatika kurithi, laa sivyo elimu pekee haiwezi kumwondoa mtu ktk lindi la umaskini kwa sababu hizo kazi zenyewe ni za kukamatia..Mtu yuko radhi kukutoa roho ukianza kuzengea kazi yake au uje na ki Phd chako basi umejenga maadui kuliko marafiki..
Kisomi tunaweza kabisa kusema kinachowezekana Marekani kinashindikana vipi Tanzania!... hatuna jibu la kitabuni...lakini mara zote sababu ni WATU na MAZINGIRA...
Mara nyingi nimeona kuwa mila na desturi zetu sisi Wadanganyika huona rangi mbili tu ktk issues yaani Nyeusi (Black) na Nyeupe (white) hakuna katikati.. mara nyingi tumeshindwa kufanya maamuzi kwa sababu hatuna middle ground yaani color - Gray ambayo inatuwezesha kuona pande mbili kwa mazuri na mabaya yake.

Binafsi swala la kina Mramba na Yona hata kama ni changa la macho kwa desturi yetu nina hakika litapunguza sana moto huu wa Ufisadi..Kutofikishwa kwao mahakamni toka miaka ile iliyopita inatokana na mfumo mzima wa utawala wa Mkapa.. Viongozi ku abuse madaraka waliyopewa ilikuwa ndio somo, kila mmoja wao aliona sifa kujitajirisha..wakajenga taifa la untouchbles, hivyo sioni ajabu kabisa leo hii wao kufikishwa mahakamani kama mwanzo wa ufagio wa chuma.
Kila jambo lazima liwe na mwanzo, hata kama wangeanza na Mkapa kuna watu wangesema kwa nini kina Yona na Mramba wasifikishwe wao mahakamani kwanza...Nijuavyo mimi kesi zote zinazohusu kundi la Mafioso au Cartel huanza na watu wa chini yake kabla hujamfikia Don, na ukisha fika huko basi tayari una mlolongo mzima wa wahusika...
 
Mkandara, Zakumi,

Kama kuna nafasi murua kubadilisha business as usual Tanzania, ni hii.

Kesi ya Mramba na Yona inatupa nafasi kubwa sana hasa kwa wale CCM Mageuzi na Upinzani (Sitta, Mwakyembe, Makinda, Shelukindo, Seleli, Killango, Zitto, Slaa, Hamad, Maghimbi n.k.) kuleta msukumo ndani ya Bunge ya kutaka mhimili wa tatu yaani Bunge, liwe na mamlaka ya kupitia si mikataba tuu, bali kuwa na uwezo wa kuwakalisha kitako watu wa Serikali kuu na kuvua ile executive priviledge ambayo imetumika kama kinga.

Hili linawezekana kabisa na hata wale wa ndani ya CCM wakiweza kukaa upande mmoja na kupata baraka za Mwenyekiti, kunaweza kufanyika mabadiliko makubwa sana ya kisiasa ambayo yanaweza kutuondolea bugudha kama Taifa na hata pamoja na kuwa CCM inaweza kuendelea kutawala, lakini kunawezekana kukawa na uwiano mzuri ambao utatoa nafasi nzuri kwa upinzani kujijenga kwa makini na Wanasiasa waka wakifanya kazi kwa niaba ya Taifa kwa moyo na si kutuhadaa,

Yetu macho...!
 
Rev.Kishoka,
Nina wasiwasi na nguvu ya hawa watu kwa sasa hivi kwani mtu pekee ambaye nadhani - nitarudia kusema, nadhani yuko pamoja nao ni rais mwenyewe Kikwete..
Katika malezi yetu na mazingira tuliyokulia haiwezekani kabisa hawa kina Zitto, Sitta, Mwakyembe na wengine wapate nguvu na ubavu wa kusema wanayoyasema bila idhini toka juu ama kuwa mtu huku juu anayewalinda.
Ni mfumo wa kiamaisha wa Mwafrika kuwa, mkubwa hakosei na ukileta mdomo utapigwa bakora hata kama umesema ukweli..Na kibaya zaidi hata kama mzee kaja gundua ulikuwa right bado hawezi kuomba samahani kwa bakora alizokucharaza acha mbali kukubali alikuwa wrong, itachukuliwa tu kwamba wewe ndiye umefundishwa adabu - hutarudia kuuchonga!
I hope kuwa huu ni mwanzo mzuri wa mageuzi ya Utawala bora jambo ambalo limetushinda kwa miaka mingi sana..Na uongozi bora ni mwanzo wa kifo cha Mafisadi ambao pekee ndio wameturudisha nyuma ktk maendeleo ya nchi yetu..Nimesoma makala ya J.J. Mnyika akisema taifa limepoteza over 1.3 trillioni ktk awamu hii ya Kikwete, tukirudi nyuma toka Mwinyi hata sijui ni kiasi gani cha fedha tumeliwa.. Yaani ni aibu tupu kuhadithia mtu asiyekuwa Mtanzania..
 
Zakumi, Rev. Kishoka..
Wakuu maneno mazito lakini tunasahau kwamba nchi tunayoizungumzia hapa ni Tanzania..tuifikirie Tanzania kama Tanzania tunayoifahamu, nchi tajiri yenye raia maskini wa kutupa na siasa ndiyo njia pekee ya Utajiri au kwa lugha nyingine ku- gain POWER. Hakuna short cut zaidi ya kuwa baba yako alikuwa Tajiri na umebahatika kurithi, laa sivyo elimu pekee haiwezi kumwondoa mtu ktk lindi la umaskini kwa sababu hizo kazi zenyewe ni za kukamatia..Mtu yuko radhi kukutoa roho ukianza kuzengea kazi yake au uje na ki Phd chako basi umejenga maadui kuliko marafiki..
Kisomi tunaweza kabisa kusema kinachowezekana Marekani kinashindikana vipi Tanzania!... hatuna jibu la kitabuni...lakini mara zote sababu ni WATU na MAZINGIRA...
Mara nyingi nimeona kuwa mila na desturi zetu sisi Wadanganyika huona rangi mbili tu ktk issues yaani Nyeusi (Black) na Nyeupe (white) hakuna katikati.. mara nyingi tumeshindwa kufanya maamuzi kwa sababu hatuna middle ground yaani color - Gray ambayo inatuwezesha kuona pande mbili kwa mazuri na mabaya yake.

Binafsi swala la kina Mramba na Yona hata kama ni changa la macho kwa desturi yetu nina hakika litapunguza sana moto huu wa Ufisadi..Kutofikishwa kwao mahakamni toka miaka ile iliyopita inatokana na mfumo mzima wa utawala wa Mkapa.. Viongozi ku abuse madaraka waliyopewa ilikuwa ndio somo, kila mmoja wao aliona sifa kujitajirisha..wakajenga taifa la untouchbles, hivyo sioni ajabu kabisa leo hii wao kufikishwa mahakamani kama mwanzo wa ufagio wa chuma.
Kila jambo lazima liwe na mwanzo, hata kama wangeanza na Mkapa kuna watu wangesema kwa nini kina Yona na Mramba wasifikishwe wao mahakamani kwanza...Nijuavyo mimi kesi zote zinazohusu kundi la Mafioso au Cartel huanza na watu wa chini yake kabla hujamfikia Don, na ukisha fika huko basi tayari una mlolongo mzima wa wahusika...

Mkandara:

Nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa. Lakini inabidi tujiulize maswali ya kimsingi iwapo kweli tunataka maendeleo.

Swali la kwanza, je idadi ya watanzania waliosoma na mwenye mwamko inatosha kuleta mabadiliko?

Kipindi Uhuru, mapinduzi na muungano yanatokea ungetilia wasiwasi mkubwa kiwango cha watanzania ku-grasp uendeshaji wa nchi inayoweza kujikwamua kimatatizo.

Sasa hivi level ya mwamko wa mawazo ya kisasa (enlighnment) hupo, lakini viongozi wakubwa wa nchi na chama tawala kinaendesha nchi kama wakati nchi ilikuwa na madaktari 12 na wenye degree chini ya 20.

Yona, Mkapa, Mramba etc wamechukua degree wakati nchi haina wasomi. Kipindi hicho joho la graduation linatundikwa sebuleni kama pambo. Hivyo sehemu kubwa ya maisha yao kama wasomi, wameishi na watanzania wenye elimu ndogo. Na bado wanapicha hiyohiyo, wakati nchi imebadilika.

Kwa qualification za elimu za Yona na Mramba walizonazo, ukiweka tangazo la nafasi ya kazi unaweza kupata watanzania zaidi ya 2000 wenye elimu kama zao na zaidi. Sasa kwanini tuendelee kuendesha nchi kwa kujifichaficha kama vile uhuru tumepata jana? Na kwanini wao waendelee kufikiri kuwa nchi bado ni hilehile ya miaka ya 60?

Marekani ilipo kick-off maendeleo yake kwa wastani ilikuwa na wasomi wachache kuliko Tanzania.

Mkandara suala hapa lisiwe mila na desturi za watanzania. Hizi mila na desturi za watanzania zimejengwa kwa zaidi ya miaka elfu na huwezi kuzibomoa kwa siku moja au kizazi kimoja. Itakuchukua miaka mingi na resource nyingi na bado utawaacha watanzania kama ulivyowakuta.

Kwa upande wangu mimi naona tuachane na mambo ya mila na desturi za watanzania. Na tuangalie Minimum Requirements zinazohitajika ku-kick off maendeleo. Kwa maoni yangu minimum requirements zimetimia.
 
Mkandara, Zakumi,

Kama kuna nafasi murua kubadilisha business as usual Tanzania, ni hii.

Kesi ya Mramba na Yona inatupa nafasi kubwa sana hasa kwa wale CCM Mageuzi na Upinzani (Sitta, Mwakyembe, Makinda, Shelukindo, Seleli, Killango, Zitto, Slaa, Hamad, Maghimbi n.k.) kuleta msukumo ndani ya Bunge ya kutaka mhimili wa tatu yaani Bunge, liwe na mamlaka ya kupitia si mikataba tuu, bali kuwa na uwezo wa kuwakalisha kitako watu wa Serikali kuu na kuvua ile executive priviledge ambayo imetumika kama kinga.

Hili linawezekana kabisa na hata wale wa ndani ya CCM wakiweza kukaa upande mmoja na kupata baraka za Mwenyekiti, kunaweza kufanyika mabadiliko makubwa sana ya kisiasa ambayo yanaweza kutuondolea bugudha kama Taifa na hata pamoja na kuwa CCM inaweza kuendelea kutawala, lakini kunawezekana kukawa na uwiano mzuri ambao utatoa nafasi nzuri kwa upinzani kujijenga kwa makini na Wanasiasa waka wakifanya kazi kwa niaba ya Taifa kwa moyo na si kutuhadaa,

Yetu macho...!

Bunge lina nafasi kubwa sana. Kikatiba Rais wa Zanzibar alikuwa ni makamu wa rais iwapo rais anatoka Tanzania. Ni bunge lililobadilisha kifungu hicho.

Tatizo linalokuja hapa ni kuwa wabunge wengi wanafanyia kazi vitu wakati matatizo yametokea. Na wanafanyia kazi instance moja na kushindwa kuelewa kuwa instance nyingine yenye the same characteristics inaweza kutokea.

Kwani ununuzi wa rada, kivuko cha kigamboni, Richmond, ununuzi wa ndege za ATC, na aliyofanya Yona na Mramba zinatofautiana nini? Characteristcs ni sawa. Na kwanini tatizo la kwanza lilipotokea hatukuziba ufa na tunaamua kujenga ukuta?

Sijaona report ya Mwakyembe lakini nafikiri report hiyo ingezikatia kuwa suala hilo limeshajitokeza miaka ilitopita katika awamu zote na ufumbuzi uangalie suala lilopo na matatizo ya baadaye.
 
Zakumi,
Mkuu nakuelewa sana lakini nakuomba pia unielewe upande wangu kuhusiana na Mila na Desturi labda itabidi nikae na kuchonga kitu kinachohusiana na hizi Mila na desturi..
* Ni vugumu sana kumwamsha mtu aliyelala, waswahili wanasema utalala wewe...

Ni hivi, Hao kina Yona, Mramba kweli wamesoma zamani na walitawala nchi kulingana watu na mazingira waliyoyakuta..Kuelimika kwa wananchi bado haijaondoa mila na desturi chafu ni sawa na mtu aliyeacha kula kwa mkono akatumia kisu na Umma lakini bado anakula ugali na nyama, nutrition anazopata bado ni zile zile tu.

Part one - Uchumi.
Vijana wetu wengi waliosoma bado kabisa maskini wa hali na mali na uwezekano mkubwa wa kutumia madaraka yao vibaya bado upo kutokana na kwamba bado chakula ni kile kile kile..Kina Mramba walitundika majoho yao ukutani, leo hii vjana wanatundika hati zao ukutani yote hii ni kuonyesha kile walichosomea wakati wenzewtu wazungu wanatundika vyeti vya accomplishment na sifa ama tuzo walizopewa kutokana na kazi waliyoifanya. Hapa tofauti ni kwamba wenzetu wanatundika matunda ya kazi zao sisi bado tunatundika matunda ya elimu tuliyokuwa nayo..
kazi ngumu inayotakiwa kutupiwa macho ni mageuzi ya Uchumi, Policy zetu zitazame uchumi zaidi ya Uongozi wa mtu ama chama kwa sababu hadi leo hii bado tunamchagua mtu kuongoza mbele ya mrengo wa Chama. Vyama vyetu vimeundwa kutokana na WATU badala ya mrengo na kama nilivyosema hapo awali kuna mchanganyiko wa Conservative, Liberal na Progressive ndani ya CCM na vyama vyote vya Upinzani kwa hiyo hawa vijana wetu wanpoingia ktk mazingira haya ya siasa huwa wanafuata yale waliyoyakuta..
Watu na Mazingira, mkuu bado inanipa shida sana ku introduce any changes ktk society zetu kwa sababu ni vugumu sana kumwambia Mhaya au Mchagga aache kulima Ndizi badala yake alime ngano kutokana na soko nchi za nje!.. hii kazi kubwa, kisha jambo jingine muhimu ni kutazama ewezekano wa ngano kustawi huko Bukoba..Na tunapotazama enlighnment, ni bora zaidi kumwelemisha Mhaya au Mchagga ktk kilimo cha zao hilo badala ya kutazama cheti chake ukutani wakati focus nzima ya maendeleo yetu inaanza na kilimo cha migomba..tunasoma kwa malengo ya kiuchumi, kufungua miradi na kuwa waajiri ktk kile kilichopo ama kinawezekana.

Hivyo hivyo ukienda ktk migodi yetu, Utalii utaona kwamba sio elimu inayotushinda leo hii, ila vijana wengi wamesoma (vyeti ukutani) lakini wanaozalisha ktk sehemu hizi ni wageni. Vijana wetu wengi wamekimbilia ktk services mijini nje ya utajiri tuliokuwa nao kwa sababu serikali yetu haikuandaa mipango ambayo itawawezesha hawa vijana kutumia elimu zao kuendeleza kilimo, Utalii ama madini sehemu zao...Hivyo tumeua kabisa shina la uti wa mgongo wa uchumi wetu kwa sababu hatukutazama WATU na MAZINGIRA ktk kukuza uchimi bali tunatazama Watu na Mazingira ktk kujenga Siasa za Utawala.

Akili yangu inanipa hivi ni bora kumsaidia kumwezesha Mhaya au Mchagga aweze kulima migomba ktk ukulima wa kisasa na jitihada kubwa iwekwe ktk kutafuta soko la ndizi nchi za nje ikiwa ni pamoja na kujenga policies zitakazowawezesha kutajirika na ukulima huo...Hivyo hivyo ktk sehemu zote focus kubwa itazame utajiri wa sehemu hiyo na kumwezesha mwananchi kuona faida yake..

Kwa hiyo sina maana tujaribu kubomoa mila na desturi za Mdanganyika isipokuwa tujaribu sana kuziboresha mila na desturi hizo kutokana na elimu tuliyopata ziweze kushindana ktk mazingira haya ya Kiuchumi.

Part 2 - Uongozi bora,
Tatizo kubwa linalonishika mimi kuhusiana na Uongozi bora ni hizo mila na desturi za Ubwana na Utumwa ambazo zimetokana na kutawaliwa miaka elfu!...Kweli haziwezi kuondoka lakini mkuu wangu unaweza kuwa huru kifikra lakini kama hutaweza kujikomboa Physically ukaondokana na utumwa ambao ndio Umaskini wenyewe, nachelea kusema hizo minimum requirement haziwezi kumkomboa Mtanzania bila kuondoa utawala dhalimu uliopo. Kumbuka Moses ilimbidi awachukue watu wake toka Misri kuondoka utumwani pamoja na kwamba tayari akili zao zilikwisha choka utumwa. Ukombozi wa nchi zetu na Mapinduzi ya nchi zote yametokana na Utumwa wa kimwili zaidi ya akili, hivyo maendeleo yetu hayawezi kuwa maendeleo ikiwa elimu na nguvu ya wananchi itatumika zaidi kujenga Pyramids. Ni hadi pale watawala watakapo ona kwamba maendeleo sio Pyramids isipokuwa hali na maisha ya hao watumwa wenyewe..
Where do we start!..binafsi naamini kabsia kwamba tukianza na kupiga vita Azimio la Zanzibar ambalo linawapa POWER viongozi kujitajirisha mkuu wangu hatuwezi kabisa kwenda kokote. Ufisadi wote umeanzia hapo hakuna sura nyingineyo.. trust me.
Siku zote nguvu na jeuri ya Binadamu huanza pale unapokuwa na FEDHA ambazo zitajenga hemaya yako - POWER. Toka kina Firaun, Julius caesar, Haile Selatse, Mobutu na majambazi wote kina Scarface, wote hawa sio kweli walilewa na madaraka yaliyowapewa,isipokuwa nguvu kubwa ilitokana na UTAJIRI waliojilimbikiza. Kwa kufahamu hivyo ndio maana napiga vita sana Azimio la Zanzibar!..
Trust me, enlightment ya wananchi kama viongozi wana nguvu ya FEDHA haiwezi kabisa kuleta mabadiliko isipokuwa maendeleo yatatokana na kutegemea maamuzi ya hao viongozi..unless tujikomboe kimwili yaani kuondoa serikali iliyopo madarakani..mmmmh!
Duh! inabidi nishushe pumzi kwanza yaani wee niache tu navyochukia hilo Azimio la Zanzibar!
* Naogopa kasi zangu zitakuja nilaza mimi kuhusiana na swala hili la Zanzibar!
 
Phew Mkandara. I bet you can write.

Mkandara. Kusoma na kuishi kwangu nje ya nchi kumenisaidia kufuta ujinga fulani au kunipa exposure ambayo nisingeipata kama ningebaki Tanzania.

Na vilevile nilipata bahati ya kusoma katika vyuo vya Tanzania. Lakini matarajio yangu yalikuwa ni tofauti.

Nikiwa Tanzania niliona kuwa ngazi ya elimu itaongeza kipato changu. Hivyo juhudi zilikuwa katika kupata cheti cha juu zaidi ili niongeze mapato yangu.

Hapa mtoni shule nazisoma ili kuondoa weakeness zangu lakini mshahara kazini unaongezeka kutokana na kile ninachoangizwa kufanya.

Tukirudi kwenye mada. Expectations za watu katika jamii zinajengwa na kizazi kilichowatangulia. Kwa sasa hivi, ninaogopa kusema kuwa kizazi cha watanzania wasomi kinafikiri kuwa serikali au kazi za umma ni sehemu ya kuchota. Na hii sio kwa sababu ya Azimio la Zanzibar kuruhusu au Azimio la Arusha kukataza bali ni expectations zetu.

Kama expectations zako ni kuiba. Ni lazima utapata njia hiyo bila kujali kuwepo kwa Azimio lolote.

Mfanyakazi TRA sio mwanasiasa na abanwi na Azimio lolote lile lakini anaiba kwa sababu hiyo ni expetation yake.

Hivyo suala la kusema kuwa Azimio la Zanzibar linawafanya viongozi waibe sikubaliani nao. Mwizi hafanyi recitation wakati anaiba. Kama angekuwa, basi angekumbuka kuwa Biblia na Koran inamkumbusha kuwa wizi si mzuri.

Njia moja ya kuondoa mambo ya hujuma ni kuwa Transparent. Na mtu akifanya makosa kwa makusudi basi rekodi zake zimsute maishani mwake. Si unajua mtoni ukiomba kazi kuna background check. Basi tuanze kuzitumia.

Kama sikosehi Mramba aliwahi kuenguliwa ubunge kwa sababu kwenye uchaguzi alitumia faulo. Kama kufanya faulo za kisiasa kungehesabika kama ku-commit political suicide, yaani Mramba angekuwa nje ya siasa miaka zaidi ya ishirini uliyopita.
 
Hapo umenena mkuu.

Kwenye Biblia kua sentenso inayosema "mwanadamu siku zake ni miaka 70"!

Sasa unajiuliza, je ukishajipatia kila kitu kama Johnson Lukaza alivyojichumia kabla hata ya kuwa na miaka 35, je ile mingine 35 iliyobakia atafanya nini?

Zaidi Uchotaji huu laiti ungekuw ani mara moja na utumike kama mtaji au msingi, bali huendelea milele.

Sasa kwenye uchotaji, kunakuja rushwa na kuvunja sheria nyingine ambako hufikisha kupotea au kutoweka kwa ushahidi muhimu.

Nikirudi kwenye nia halisi ya kusema kuwa hili ni changa la macho, kwa kina Jeetu Patel na Lukaza, sijui ni vipi tunaweza kuwashikisha adabu. Je hatuwezi kuwashitaki kwa kutumia ile sheria ya uhujumu uchumi na hata kuwafilisi?

Inapokuja kwa Yona na Mramba, hata ukiwaingiza kina Chenge, Lowassa, Karamagi, Meghji, Msabaha, Mgonja, Mboma na wengine, inakuwa kama ni tosha kuwamaliza kisiasa kwa kuwashitaki kwa uzembe, matumizi mabaya ya madaraka na kupotea kwa mali za umma kutokana na maamuzi mabovu na uongozi mbaya.

Nafikiri doa hili litanata kama gundi kuliko kutafuta wapi walificha hela!
 
Mkandara:

Nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa. Lakini inabidi tujiulize maswali ya kimsingi iwapo kweli tunataka maendeleo.

Swali la kwanza, je idadi ya watanzania waliosoma na mwenye mwamko inatosha kuleta mabadiliko?

Kipindi Uhuru, mapinduzi na muungano yanatokea ungetilia wasiwasi mkubwa kiwango cha watanzania ku-grasp uendeshaji wa nchi inayoweza kujikwamua kimatatizo.

Sasa hivi level ya mwamko wa mawazo ya kisasa (enlighnment) hupo, lakini viongozi wakubwa wa nchi na chama tawala kinaendesha nchi kama wakati nchi ilikuwa na madaktari 12 na wenye degree chini ya 20.

Yona, Mkapa, Mramba etc wamechukua degree wakati nchi haina wasomi. Kipindi hicho joho la graduation linatundikwa sebuleni kama pambo. Hivyo sehemu kubwa ya maisha yao kama wasomi, wameishi na watanzania wenye elimu ndogo. Na bado wanapicha hiyohiyo, wakati nchi imebadilika.

Kwa qualification za elimu za Yona na Mramba walizonazo, ukiweka tangazo la nafasi ya kazi unaweza kupata watanzania zaidi ya 2000 wenye elimu kama zao na zaidi. Sasa kwanini tuendelee kuendesha nchi kwa kujifichaficha kama vile uhuru tumepata jana? Na kwanini wao waendelee kufikiri kuwa nchi bado ni hilehile ya miaka ya 60?

Marekani ilipo kick-off maendeleo yake kwa wastani ilikuwa na wasomi wachache kuliko Tanzania.

Mkandara suala hapa lisiwe mila na desturi za watanzania. Hizi mila na desturi za watanzania zimejengwa kwa zaidi ya miaka elfu na huwezi kuzibomoa kwa siku moja au kizazi kimoja. Itakuchukua miaka mingi na resource nyingi na bado utawaacha watanzania kama ulivyowakuta.

Kwa upande wangu mimi naona tuachane na mambo ya mila na desturi za watanzania. Na tuangalie Minimum Requirements zinazohitajika ku-kick off maendeleo. Kwa maoni yangu minimum requirements zimetimia.

You nailed it Zakumi...Hata Mwinyi alishawahi kuwaambia wenzie lakini naona wanayapuuzia na kudhani ni uswahili as usual...Lakini ndo ukweli huo...Tanzania ya sasa imebadilika na hivyo wasitegemee ufisadi kuendelea kwa urahisi kama ilivyokuwa before.
 
Back
Top Bottom