Zakumi,
Mkuu nakuelewa sana lakini nakuomba pia unielewe upande wangu kuhusiana na Mila na Desturi labda itabidi nikae na kuchonga kitu kinachohusiana na hizi Mila na desturi..
* Ni vugumu sana kumwamsha mtu aliyelala, waswahili wanasema utalala wewe...
Ni hivi, Hao kina Yona, Mramba kweli wamesoma zamani na walitawala nchi kulingana watu na mazingira waliyoyakuta..Kuelimika kwa wananchi bado haijaondoa mila na desturi chafu ni sawa na mtu aliyeacha kula kwa mkono akatumia kisu na Umma lakini bado anakula ugali na nyama, nutrition anazopata bado ni zile zile tu.
Part one - Uchumi.
Vijana wetu wengi waliosoma bado kabisa maskini wa hali na mali na uwezekano mkubwa wa kutumia madaraka yao vibaya bado upo kutokana na kwamba bado chakula ni kile kile kile..Kina Mramba walitundika majoho yao ukutani, leo hii vjana wanatundika hati zao ukutani yote hii ni kuonyesha kile walichosomea wakati wenzewtu wazungu wanatundika vyeti vya accomplishment na sifa ama tuzo walizopewa kutokana na kazi waliyoifanya. Hapa tofauti ni kwamba wenzetu wanatundika matunda ya kazi zao sisi bado tunatundika matunda ya elimu tuliyokuwa nayo..
kazi ngumu inayotakiwa kutupiwa macho ni mageuzi ya Uchumi, Policy zetu zitazame uchumi zaidi ya Uongozi wa mtu ama chama kwa sababu hadi leo hii bado tunamchagua mtu kuongoza mbele ya mrengo wa Chama. Vyama vyetu vimeundwa kutokana na WATU badala ya mrengo na kama nilivyosema hapo awali kuna mchanganyiko wa Conservative, Liberal na Progressive ndani ya CCM na vyama vyote vya Upinzani kwa hiyo hawa vijana wetu wanpoingia ktk mazingira haya ya siasa huwa wanafuata yale waliyoyakuta..
Watu na Mazingira, mkuu bado inanipa shida sana ku introduce any changes ktk society zetu kwa sababu ni vugumu sana kumwambia Mhaya au Mchagga aache kulima Ndizi badala yake alime ngano kutokana na soko nchi za nje!.. hii kazi kubwa, kisha jambo jingine muhimu ni kutazama ewezekano wa ngano kustawi huko Bukoba..Na tunapotazama enlighnment, ni bora zaidi kumwelemisha Mhaya au Mchagga ktk kilimo cha zao hilo badala ya kutazama cheti chake ukutani wakati focus nzima ya maendeleo yetu inaanza na kilimo cha migomba..tunasoma kwa malengo ya kiuchumi, kufungua miradi na kuwa waajiri ktk kile kilichopo ama kinawezekana.
Hivyo hivyo ukienda ktk migodi yetu, Utalii utaona kwamba sio elimu inayotushinda leo hii, ila vijana wengi wamesoma (vyeti ukutani) lakini wanaozalisha ktk sehemu hizi ni wageni. Vijana wetu wengi wamekimbilia ktk services mijini nje ya utajiri tuliokuwa nao kwa sababu serikali yetu haikuandaa mipango ambayo itawawezesha hawa vijana kutumia elimu zao kuendeleza kilimo, Utalii ama madini sehemu zao...Hivyo tumeua kabisa shina la uti wa mgongo wa uchumi wetu kwa sababu hatukutazama WATU na MAZINGIRA ktk kukuza uchimi bali tunatazama Watu na Mazingira ktk kujenga Siasa za Utawala.
Akili yangu inanipa hivi ni bora kumsaidia kumwezesha Mhaya au Mchagga aweze kulima migomba ktk ukulima wa kisasa na jitihada kubwa iwekwe ktk kutafuta soko la ndizi nchi za nje ikiwa ni pamoja na kujenga policies zitakazowawezesha kutajirika na ukulima huo...Hivyo hivyo ktk sehemu zote focus kubwa itazame utajiri wa sehemu hiyo na kumwezesha mwananchi kuona faida yake..
Kwa hiyo sina maana tujaribu kubomoa mila na desturi za Mdanganyika isipokuwa tujaribu sana kuziboresha mila na desturi hizo kutokana na elimu tuliyopata ziweze kushindana ktk mazingira haya ya Kiuchumi.
Part 2 - Uongozi bora,
Tatizo kubwa linalonishika mimi kuhusiana na Uongozi bora ni hizo mila na desturi za Ubwana na Utumwa ambazo zimetokana na kutawaliwa miaka elfu!...Kweli haziwezi kuondoka lakini mkuu wangu unaweza kuwa huru kifikra lakini kama hutaweza kujikomboa Physically ukaondokana na utumwa ambao ndio Umaskini wenyewe, nachelea kusema hizo minimum requirement haziwezi kumkomboa Mtanzania bila kuondoa utawala dhalimu uliopo. Kumbuka Moses ilimbidi awachukue watu wake toka Misri kuondoka utumwani pamoja na kwamba tayari akili zao zilikwisha choka utumwa. Ukombozi wa nchi zetu na Mapinduzi ya nchi zote yametokana na Utumwa wa kimwili zaidi ya akili, hivyo maendeleo yetu hayawezi kuwa maendeleo ikiwa elimu na nguvu ya wananchi itatumika zaidi kujenga Pyramids. Ni hadi pale watawala watakapo ona kwamba maendeleo sio Pyramids isipokuwa hali na maisha ya hao watumwa wenyewe..
Where do we start!..binafsi naamini kabsia kwamba tukianza na kupiga vita Azimio la Zanzibar ambalo linawapa POWER viongozi kujitajirisha mkuu wangu hatuwezi kabisa kwenda kokote. Ufisadi wote umeanzia hapo hakuna sura nyingineyo.. trust me.
Siku zote nguvu na jeuri ya Binadamu huanza pale unapokuwa na FEDHA ambazo zitajenga hemaya yako - POWER. Toka kina Firaun, Julius caesar, Haile Selatse, Mobutu na majambazi wote kina Scarface, wote hawa sio kweli walilewa na madaraka yaliyowapewa,isipokuwa nguvu kubwa ilitokana na UTAJIRI waliojilimbikiza. Kwa kufahamu hivyo ndio maana napiga vita sana Azimio la Zanzibar!..
Trust me, enlightment ya wananchi kama viongozi wana nguvu ya FEDHA haiwezi kabisa kuleta mabadiliko isipokuwa maendeleo yatatokana na kutegemea maamuzi ya hao viongozi..unless tujikomboe kimwili yaani kuondoa serikali iliyopo madarakani..mmmmh!
Duh! inabidi nishushe pumzi kwanza yaani wee niache tu navyochukia hilo Azimio la Zanzibar!
* Naogopa kasi zangu zitakuja nilaza mimi kuhusiana na swala hili la Zanzibar!