"Rev Kishoka and other 'skepticists' ningependa kujua ni nini hasa mlitaka Rais afanye kwa sasa? Ajipeleke yeye mwenyewe mahakamani au? Nafikiri hata kama hatuamini sincerity ya Rais kwa sasa tutoe basi alternative wakati tunapom-critique! Inachukiza mtu aliyekuwa anapigania kwa nguvu zote mafisadi kupelekwa mahakamani, hadi kuamini kuwa kamwe hawatapelekwa mahakamani sasa anabadilika baada ya kuona wamepelekwa. Process inapoanza anadai hakubaliani na hilo kwa sababu anayeisimamia hiyo process naye ni muhusika katika ufisadi. Kwa hiyo afanyeje sasa! aache?"
Mkuu mchungaji,
analysis yako nzuri sana kwa kuisoma. Mkuu Nurujamii amekuuliza maswali hapo juu...Ningeomba kujua majibu yako Mkuu.
Binafsi mtazamo wangu ni kua pragmatic, sasa ntapokutana na idealists phylosophies (ambazo ndio zime shamiri hapa jamvini),...napata tabu kidogo kuelewa ni nini hasa mkuu unachotaka kifanyike, under the contemporary Tanzanian political environment ili ufurahi kuwa kuna kazi ya kupambana na ufisadi inafanyika?
Sober,
Nurujamii ni mmoja wa watu ambao hushabikia na kulipa uzito ninaloliandika. Katika hili la mashitaka, anaonelea kuwa mbona sifurahi kinachotokea ambacho sikutegemea kitokee?
Jibu langu kwake na kwako ni hili;
Nikipima na kusoma kilichofanyika na hata "nia" ya kufikisha Mramba, Yona, Patel na Lukaza, natatizwa na lilelinalojionesha kwangu kuwa hawa wamepelekwa mahakamani si kwa nia au madhumuni ya kweli kuwa wachukuliwe hatua, bali ni kutokana na mashinikizo na sababunyingine za kufanya kuonekane kuwa sasa Serikali inafanya kazi yake.
Tumeshajiuliza sana hapa kuhusu suala la EPA kuwa Deloitte and Touche walifanya audit, wakatoa ripoti moja mbaya sana kuhusu BOT. Ripoti hiyo, hata Utoah ambaye ni mdhibiti na mkaguzu mkuu wa Serikali aliafikiana nayo na kutoa tathmini kuwa BOT imefanya kwa makusudi au kwa uzembe wa kupindukia kuruhusu hujuma za EPA.
Dr. Slaa akatoa kauli bungeni na sis tukapiga kelele, lakini Serikali yetu kwanza ikatoa kauli kukanusha kuwepo hujuma kubwa kama hiyo. Ni mpaka pale mabalozi wa nchi tajiri walipoanza kupiga kelele wakiongozwa na Mark Green wa USA, yule jamaa wa Neatherlands, Norway na Ujerumani na mpaka nchi moja wafadhili walipotoa kitisho kusitisha misaada (unakumbuka Membe alvyojibu kwa kiburi kuwa sisi ni nchi huru tusiingiliwe?) ndipo taratibu Serikali na Bunge la CCM likakubali kuna tatizo nao wakaipa kazi ya uchunguzi kampuni ya Earnst and Young.
Kina E&Y wakaja na majibu yale yale ya Deloitte Touche na Utoah, wakawasilisha serikalini. Rais na Serikali, wakaundia tume chini ya IGP, DPP, AG na Takukuru ambao walikuwa wanalipwa laki moja kwa siku. Kamati hii teule, ikapewa muda, nayo ikashindwa kumaliza uchunguzi ikabidi iombe iongezewe muda.
Kamati ilipomaliza utafiti na uchunguzi wake, ikawasilisha ripoti ikulu na kusema inasubiri uamuzi wa Rais.
Wabunge wakahoji, ripoti iko wapi? Ikulu ikasukuma ripoti kwa Sitta na wabunge watoe maamuzi, Bunge likajivua jukumu hilo, hivyo faili likarudi Ikulu.
Sasa wakati wa danadana hizi, Mama Killango akatoa kauli hapendwi mtu, wakaja kina Serukamba, Kisumo na Kingung'e kutoa kauli kali na chafu na kudai kuwa hakuna la msingi kuhusu EPA. Zaidi, CCM ikabadilisha kibao na kuanza kuhodhi sakata lote la EPA kwa kudai kuwa eti, wao ndio walioliibua na si mtu mwingine.
Wakati E&Y wanafanya uchunguzi wao, Manumba ambaye ni DCI alitoa kauli kuwa wao Polisi hawawezi kuanza kufanya uchunguzi wowote mpaka E & Y wamalize uchunguzi wao.
Sasa najiuliza, ikiwa karibu miezi 18 tumekuwa tukiimba EPA, EPA, EPA na kwanza Serikali na Waziri wake Meghji wakakanusha hakuna wizi au hujuma, Manumba akasema anasubiri Ikulu impe maelekezo ya nini cha kufanya, unategemea kufikishwa kwa hawa jamaa Mahakamani kutanipa furaha zaidi ya kuhoji kwa kuangalia mashitaka waliyosomewa?
Zakumi anadai kuwa ni heri basi tuwafunge hata kwa hayo makosa madogo madogo, je hiyo ndiyo suluhisho na njia ya kuhakikisha kuwa hakuna tena uhujumu?
Sasa hivi, minong'oni ni kuwa ili CCM ishinde kwa kishindo, inabidi suala la EPA na ufisadi yapatiwe japo namna ya kufanana na ufumbuzi. Zaidi ni ukweli kuwa wahisani wamesema hawatoi pesa zao kusaidia bajeti yetu mpaka kieleweke.
Sasa kwa nini mnamkasirikia au kufadhaishwa na Mchungaji anaposema kuwa hili ni changa na hakuna nia ya kweli kutafuta ufumbuzi?
Ama nikupeni mfano mwingine. Lowassa, Karamagi, Chenge na Msabaha. Hawa walifanya uzembe na wanatuhumiwa kuwa wamekula mlungula. Lakini baada ya wao kujitoa kwenye madaraka, hata ndaniya CCM yenyewe hawajachukuliwa hatua, hawajapewa karipio badala yake wanafanywa ni wafalme, wamepewa maandamano kuwapokea, bado wananyenyekewa ndani ya chama na v=hivyo kuonyesha umma kuwa wao wana nguvu na Serikali haina nguvu.
Ni mpaka pale matatizo yetu yatakapotatuliwa kwa nia ya kweli na usahihi wa kutatua, ndipo nitapata faraja. kinyume na hapo, ni changa mbalo nimelivalia miwani.