GE2025 Paul Chacha Makuri achukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Serengeti

GE2025 Paul Chacha Makuri achukua fomu kugombea ubunge Jimbo la Serengeti

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Chacha Makuri, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Serengeti kupitia tiketi ya chama hicho tawala, akiahidi kusukuma mbele ajenda nne kuu zinazolenga maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge mjini Mugumu, Makuri amesema: “Ninajitokeza si kwa ajili ya umaarufu wala kwa misukumo ya makundi, bali kwa wito wa ndani uliopimwa kwa muda mrefu”.

Kwa mujibu wa Makuri, azma yake ni kuleta mwelekeo mpya unaotokana na “sauti mpya” ya Serengeti, inayolenga kutatua changamoto zinazoikumba wilaya hiyo pamoja na kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo.

Katika maelezo yake, amebainisha wazi kuwa amejipanga kusukuma mbele ajenda nne kuu ambazo ni miundombinu ya barabara – kuunganisha Serengeti kwa lami na wilaya jirani kama Tarime, Bunda na Musoma. Afya na elimu – kuhakikisha vifaa, watumishi na mazingira bora vinapatikana hadi vijijini. Ajira na uwezeshaji wa vijana – kupitia elimu ya ujuzi na mifumo ya kifedha ya kijamii kama VICOBA na SACCOS, na mapambano dhidi ya umaskini wa vijijini – kwa kukuza kilimo cha kisasa na masoko ya uhakika.

Makuri pia ametumia jukwaa hilo kuomba ridhaa ya chama chake cha CCM na wananchi wa Serengeti.

“Kwa heshima kubwa, naomba CCM – chama changu cha maisha – kinikubali na kuniamini tena… Na kwa wananchi wangu… naomba mnipokee kama mtoto wenu, kama kijana wenu, na kama mzalendo miongoni mwenu,” amesema.

Akihitimisha kauli yake, Makuri amesema muda umefika wa kuandika historia mpya ya maendeleo ya kweli Serengeti, huku akiashiria kuwa maono yake yanajengwa juu ya “kazi na utu”.
1751193332697.png
 
Back
Top Bottom