Paul Chacha Makuri wa CCM achukua fomu ya kugombea Ubunge Serengeti

Paul Chacha Makuri wa CCM achukua fomu ya kugombea Ubunge Serengeti

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,


Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Chacha Makuri, ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Serengeti katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, akieleza kuwa hatua hiyo imesukumwa na dhamira ya kweli ya kulitumikia taifa kupitia jimbo hilo muhimu kwa maendeleo ya wananchi.

Akizungumza mjini Mugumu mbele ya wanachama wa CCM, viongozi wa chama na wananchi wa kada mbalimbali, Makuri amesema amefikia uamuzi huo baada ya kutafakari kwa kina na kusikiliza maoni ya watu wa Serengeti kuhusu mustakabali wa maendeleo ya jimbo hilo.

"Nimerudi nikiwa na nguvu mpya na moyo uleule wa kizalendo. Sitafuti nafasi kwa ajili ya jina au maslahi, bali kwa ajili ya watu," amesema.

Makuri amesema si mgeni katika harakati za kugombea, kwani aliwahi kuomba ridhaa ya chama mwaka 2020 bila mafanikio, lakini hakukata tamaa. Ameendelea kushiriki shughuli za kijamii na kujiimarisha katika uelewa wa changamoto na fursa zilizopo ndani ya jimbo. Kwa maelezo yake, anataka kurejesha sauti ya Serengeti kwenye ngazi ya kitaifa kwa hoja zenye uzito na zenye kujali maslahi ya wananchi.

Katika kueleza maono yake, amesisitiza kuwa anataka kushirikiana na jamii kuimarisha huduma za kijamii, hususan elimu, afya, barabara, maji na umeme. Vilevile, amesema atatoa msukumo kwa maendeleo ya vijana kupitia mafunzo ya ujuzi, mitaji na ushirikishwaji katika sekta binafsi.

IMG_1561.jpeg


Source: Jambo Tv
 
Back
Top Bottom