Paul Chacha: Ukionekana au kubainika unapitapita kutoa rushwa, adhabu yake ni kukuondoa kwenye kinyang’anyiro

Paul Chacha: Ukionekana au kubainika unapitapita kutoa rushwa, adhabu yake ni kukuondoa kwenye kinyang’anyiro

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644

Katibu wa NEC, Idara ya Organaizesheni Ndg. Paul Matiko Chacha amewataka Viongozi na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa Uchaguzi na uteuzi wa wagombea, huku wakikumbushwa kuwa vitendo hivyo vinaweza kusababisha mhusika kuondolewa kwenye kinyang’anyiro.

Akizungumza na wanachama wa CCM, Ndg. Chacha amekemea vikali tabia ya baadhi ya wanachama kutumia fedha au njia nyingine zisizo halali ili kushawishi kupata nafasi za uongozi.

Chama Cha Mapinduzi hakitavumilia vitendo vya rushwa na kwamba kiongozi na mwanachama yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo atachukuliwa hatua, ikiwemo kuondolewa kwenye kinyang’anyiro.

“Ukionekana au kubainika unapita kutoa rushwa, adhabu yake ni kukuondoa kwenye kinyang’anyiro,” alisema Ndg. Chacha.

Aidha, amewataka wanachama kushiriki katika mchakato kwa kufuata Katiba, Kanuni,taratibu na miongozo ya Chama na Jumuiya zake,Ndg. Chacha amesisitiza kuwa nafasi za uongozi zinapatikana kwa kufuata utaratibu unaotambulika badala ya kutumia fedha kuwashawishi wapiga kura.

Kauli hiyo ameisema wakati wakati akihutubia Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa katika Ukumbi wa Ihemi.
 
Back
Top Bottom